Rukia maudhui

Mistari ya Biblia kuhusu Praise

490 mistari · 106 vipengele

Mistari muhimu ya Biblia

Chuja kwa kitabu
  1. Kinywa changu kitazinena sifa za Bwana. Kila kiumbe na kilisifu jina lake takatifu milele na milele.

  2. Msifuni Bwana! Ee nafsi yangu, umsifu Bwana,

  3. Nitamsifu Bwana maisha yangu yote; nitamwimbia Mungu wangu sifa wakati wote niishipo.

  4. Usiweke tumaini lako kwa wakuu, kwa wanadamu ambao hufa, ambao hawawezi kuokoa.

  5. Roho yao itokapo hurudi mavumbini, siku hiyo hiyo mipango yao yote hukoma.

  6. Heri yeye ambaye Mungu wa Yakobo ni msaada wake, ambaye tumaini lake ni katika Bwana, Mungu wake,

  7. Muumba wa mbingu na nchi, na bahari na vyote vilivyomo ndani yake: Bwana anayedumu kuwa mwaminifu milele na milele.

  8. Naye huwapatia haki walioonewa na kuwapa wenye njaa chakula. Bwana huwaweka wafungwa huru,

  9. Bwana huwafumbua vipofu macho, Bwana huwainua waliolemewa na mizigo yao, Bwana huwapenda wenye haki.

  10. Bwana huwalinda wageni na kuwategemeza yatima na wajane, lakini hupinga njia za waovu.

  11. Bwana atamiliki milele, Mungu wako, ee Sayuni, kwa vizazi vyote. Msifuni Bwana.

  12. Msifuni Bwana. Tazama jinsi ilivyo vyema kumwimbia Mungu wetu sifa, jinsi inavyopendeza na kustahili kumsifu yeye!

  13. Bwana hujenga Yerusalemu, huwakusanya Israeli walio uhamishoni.

  14. Anawaponya waliovunjika mioyo na kuvifunga vidonda vyao.

  15. Huzihesabu nyota na huipa kila moja jina lake.

  16. Bwana wetu ni mkuu na mwenye uwezo mwingi, ufahamu wake hauna kikomo.

  17. Bwana huwahifadhi wanyenyekevu lakini huwashusha waovu mpaka mavumbini.

  18. Mwimbieni Bwana kwa shukrani, mpigieni Mungu wetu kinubi.

  19. Yeye huzifunika anga kwa mawingu, huinyeshea ardhi mvua, na kuzifanya nyasi kuota juu ya vilima.

  20. Huwapa chakula mifugo na pia makinda ya kunguru yanapolia.

  21. Furaha yake haipo katika nguvu za farasi, wala furaha yake kwenye miguu ya mwanadamu.

  22. Bwana hupendezwa na wale wamchao, wale wanaoweka tumaini lao katika upendo wake usiokoma.

  23. Mtukuze Bwana, ee Yerusalemu, msifu Mungu wako, ee Sayuni,

  24. kwa maana huimarisha makomeo ya malango yako na huwabariki watu wako walio ndani yako.

  25. Huwapa amani mipakani mwenu na kukushibisha kwa ngano safi kabisa.