Rukia maudhui

Mistari ya Biblia kuhusu Praise

490 mistari · 106 vipengele

Mistari muhimu ya Biblia

Chuja kwa kitabu
  1. Hutuma amri yake duniani, neno lake hukimbia kasi.

  2. Anatandaza theluji kama sufu na kutawanya umande kama majivu.

  3. Huvurumisha mvua yake ya mawe kama changarawe. Ni nani awezaye kustahimili ukali wa baridi yake?

  4. Hutuma neno lake na kuviyeyusha, huvumisha upepo wake, nayo maji hutiririka.

  5. Amemfunulia Yakobo neno lake, sheria zake na maagizo yake kwa Israeli.

  6. Hajafanya hivyo kwa taifa lingine lolote, hawazijui sheria zake. Msifuni Bwana.

  7. Msifuni Bwana. Msifuni Bwana kutoka mbinguni, msifuni juu vileleni.

  8. Msifuni, enyi malaika wake wote, msifuni yeye, enyi jeshi lake lote la mbinguni.

  9. Msifuni yeye, enyi jua na mwezi, msifuni yeye, enyi nyota zote zingʼaazo.

  10. Msifuni yeye, enyi mbingu zilizo juu sana, na ninyi maji juu ya anga.

  11. Vilisifu jina la Bwana kwa maana aliamuru navyo vikaumbwa.

  12. Aliviweka mahali pake milele na milele, alitoa amri ambayo haibadiliki milele.

  13. Mtukuzeni Bwana kutoka duniani, ninyi viumbe vikubwa vya baharini na vilindi vyote vya bahari,

  14. umeme wa radi na mvua ya mawe, theluji na mawingu, pepo za dhoruba zinazofanya amri zake,

  15. ninyi milima na vilima vyote, miti ya matunda na mierezi yote,

  16. wanyama wa mwituni na mifugo yote, viumbe vidogo na ndege warukao,

  17. wafalme wa dunia na mataifa yote, ninyi wakuu na watawala wote wa dunia,

  18. wanaume vijana na wanawali, wazee na watoto.

  19. Wote na walisifu jina la Bwana, kwa maana jina lake pekee limetukuka, utukufu wake uko juu ya nchi na mbingu.

  20. Amewainulia watu wake pembe, sifa ya watakatifu wake wote, ya Israeli, watu walio karibu na moyo wake. Msifuni Bwana.

  21. Msifuni Bwana. Mwimbieni Bwana wimbo mpya, sifa zake katika kusanyiko la watakatifu.

  22. Israeli na washangilie katika Muumba wao, watu wa Sayuni na wafurahi katika Mfalme wao.

  23. Na walisifu jina lake kwa kucheza na wampigie muziki kwa matari na kinubi.

  24. Kwa maana Bwana anapendezwa na watu wake, anawavika wanyenyekevu taji ya wokovu.

  25. Watakatifu washangilie katika heshima hii, na waimbe kwa shangwe vitandani mwao.