Skip to content

Mistari ya Biblia kuhusu Praise

490 mistari · 106 vipengele

Mistari muhimu ya Biblia

Chuja kwa kitabu
  1. Zaburi. Wimbo wa siku ya Sabato. Ni vyema kumshukuru Bwana na kuliimbia jina lako, Ee Uliye Juu Sana,

  2. kuutangaza upendo wako asubuhi, na uaminifu wako wakati wa usiku,

  3. kwa zeze yenye nyuzi kumi na kwa sauti ya kinubi.

  4. Njooni, tumwimbie Bwana kwa furaha; tumfanyie kelele za shangwe Mwamba wa wokovu wetu.

  5. Tuje mbele zake kwa shukrani, tumtukuze kwa vinanda na nyimbo.

  6. Njooni, tusujudu, tumwabudu, tupige magoti mbele za Bwana Muumba wetu,

  7. kwa maana yeye ndiye Mungu wetu, na sisi ni watu wa malisho yake, kondoo chini ya utunzaji wake. Kama mkiisikia sauti yake leo,

  8. Mwimbieni Bwana wimbo mpya; mwimbieni Bwana dunia yote.

  9. Mwimbieni Bwana, lisifuni jina lake; tangazeni wokovu wake siku baada ya siku.

  10. Tangazeni utukufu wake katikati ya mataifa, matendo yake ya ajabu miongoni mwa mataifa yote.

  11. Kwa kuwa Bwana ni mkuu mwenye kustahili kusifiwa kuliko wote; yeye ni wa kuogopwa kuliko miungu yote.

  12. Fahari na enzi viko mbele yake; nguvu na utukufu vimo patakatifu pake.

  13. Mpeni Bwana, enyi jamaa za mataifa, mpeni Bwana utukufu na nguvu.

  14. Mpeni Bwana utukufu unaostahili jina lake; leteni sadaka na mje katika nyua zake.

  15. Mwabuduni Bwana katika uzuri wa utakatifu wake; dunia yote na itetemeke mbele zake.

  16. Furahini katika Bwana, ninyi mlio wenye haki, lisifuni jina lake takatifu.

  17. Mpigieni Bwana kelele za shangwe, dunia yote, ipaze sauti kwa nyimbo za shangwe na vinanda;

  18. mwimbieni Bwana kwa kinubi, kwa kinubi na sauti za kuimba,

  19. kwa tarumbeta na mvumo wa baragumu za pembe za kondoo dume: shangilieni kwa furaha mbele za Bwana, aliye Mfalme.

  20. Wanalisifu jina lako ambalo ni kuu na la kuogopwa: yeye ni mtakatifu!

  21. Mtukuzeni Bwana Mungu wetu, na mkaabudu katika mahali pa kuwekea miguu yake; yeye ni mtakatifu.

  22. Mtukuzeni Bwana Mungu wetu, mwabuduni kwenye mlima wake mtakatifu, kwa maana Bwana Mungu wetu ni mtakatifu.

  23. Zaburi ya shukrani. Mpigieni Bwana kelele za shangwe, dunia yote.

  24. Mwabuduni Bwana kwa furaha; njooni mbele zake kwa nyimbo za shangwe.

  25. Jueni kwamba Bwana ndiye Mungu. Yeye ndiye alituumba, sisi tu mali yake; sisi tu watu wake, kondoo wa malisho yake.