Rukia maudhui

Mistari ya Biblia kuhusu Journey of Israel Through The Desert

759 mistari · 177 vipengele

Mistari muhimu ya Biblia

Chuja kwa kitabu
  1. Sasa waue wavulana wote. Pia muue kila mwanamke ambaye alikwisha fanya tendo la ndoa,

  2. lakini mwacheni hai kwa ajili yenu kila msichana ambaye kamwe hajawahi kuzini na mwanaume.

  3. “Ninyi nyote ambao mmeua mtu yeyote au kumgusa mtu yeyote ambaye ameuawa, lazima mkae nje ya kambi kwa muda wa siku saba. Katika siku ya tatu na ya saba lazima mjitakase wenyewe pamoja na wafungwa wenu.

  4. Takaseni kila vazi pamoja na kila kitu kilichotengenezwa kwa ngozi, kwa singa za mbuzi au kwa mti.”

  5. Kisha kuhani Eleazari aliwaambia askari waliokuwa wamekwenda vitani, “Haya ndiyo matakwa ya sheria ambayo Bwana alimpa Mose:

  6. Dhahabu, fedha, shaba, chuma, bati, risasi,

  7. na kitu kingine chochote ambacho kinaweza kuhimili moto lazima mkipitishe kwenye moto, kisha kitakuwa safi. Lakini ni lazima pia kitakaswe kwa maji ya utakaso. Kitu chochote kisichoweza kuhimili moto lazima kipitishwe kwenye yale maji ya utakaso.

  8. Katika siku ya saba fueni nguo zenu, nanyi mtakuwa safi. Kisha mtaweza kuingia kambini.”

  9. Bwana akamwambia Mose,

  10. “Wewe na kuhani Eleazari pamoja na viongozi wa jamaa ya jumuiya mtahesabu watu wote na wanyama ambao walitekwa.

  11. Gawanyeni hizo nyara kati ya askari ambao walishiriki katika vita na kwa jumuiya.

  12. Kutoka fungu la wale waliokwenda kupigana vitani, tenga kama ushuru kwa ajili ya Bwana kitu kimoja kati ya kila mia tano, ikiwa ni wanadamu, ngʼombe, punda, kondoo au mbuzi.

  13. Chukua ushuru huu kutoka fungu lao, umpe kuhani Eleazari kama sehemu ya Bwana.

  14. Kutoka fungu la Waisraeli, chukua kitu kimoja kati ya kila hamsini, ikiwa ni wanadamu, ngʼombe, punda, kondoo, mbuzi au wanyama wengine. Hivyo uwape Walawi, ambao wanawajibika kutunza Maskani ya Bwana.”

  15. Kwa hiyo Mose na kuhani Eleazari wakafanya kama Bwana alivyomwagiza Mose.

  16. Nyara zilizobaki kutoka mateka ambayo askari walichukua ni kondoo 675,000,

  17. ngʼombe 72,000,

  18. punda 61,000,

  19. na wanawake 32,000 ambao hawakumjua mume kwa kufanya tendo la ndoa.

  20. Nusu ya fungu la wale waliokwenda kupigana vitani lilikuwa: Kondoo 337,500

  21. ambayo ushuru kwa ajili ya Bwana ilikuwa kondoo 675;

  22. ngʼombe 36,000 ambao ushuru kwa ajili ya Bwana ulikuwa ngʼombe 72;

  23. punda 30,500 ambao ushuru kwa ajili ya Bwana ulikuwa punda 61;

  24. Watu 16,000 ambao ushuru kwa ajili ya Bwana ulikuwa watu 32.

  25. Mose alimpa kuhani Eleazari ushuru kama sehemu ya Bwana, kama Bwana alivyomwagiza Mose.