Rukia maudhui

Mistari ya Biblia kuhusu Journey of Israel Through The Desert

759 mistari · 177 vipengele

Mistari muhimu ya Biblia

Chuja kwa kitabu
  1. Wakajinajisi wenyewe kwa yale waliyotenda; kwa matendo yao wenyewe wakajifanyia ukahaba.

  2. Mara nyingi aliwaokoa lakini walikuwa wamezama kwenye uasi, nao wakajiharibu katika dhambi zao.

  3. Lakini akaangalia mateso yao wakati aliposikia kilio chao;

  4. kwa ajili yao akakumbuka agano lake, na kutokana na upendo wake mkuu akapooza hasira yake.

  5. Akawafanya wahurumiwe na wote waliowashikilia mateka.

  6. Ndipo watu wake wakazikumbuka siku zilizopita, siku za Mose na watu wake: yuko wapi yeye aliyewaleta kupitia katikati ya bahari, pamoja na wachungaji wa kundi lake? Yuko wapi yule aliyeweka Roho wake Mtakatifu katikati yao,

  7. aliyetuma mkono wake uliotukuka wenye nguvu kuwa katika mkono wa kuume wa Mose, aliyegawa maji ya bahari mbele yao, ili kujipatia jina milele,

  8. aliyewaongoza kupitia kwenye vilindi? Kama farasi katika nchi iliyo wazi, wao hawakujikwaa,

  9. kama ngʼombe washukao bondeni kwenye malisho, walipewa pumziko na Roho wa Bwana. Hivi ndivyo ulivyowaongoza watu wako ili kujipatia mwenyewe jina tukufu.