Rukia maudhui

Mistari ya Biblia kuhusu Journey of Israel Through The Desert: Second numbering of the people

46 mistari · 177 vipengele

Mistari kuhusu Second numbering of the people

  1. Bwana alisema na Mose katika Jangwa la Sinai, katika Hema la Kukutania, siku ya kwanza ya mwezi wa pili, katika mwaka wa pili baada ya Waisraeli kutoka nchi ya Misri. Akamwambia,

  2. “Hesabu watu wa jumuiya yote ya Waisraeli kwa kufuata koo zao na jamaa zao, ukiorodhesha kila mwanaume kwa jina lake, mmoja mmoja.

  3. Wewe na Aroni mtawahesabu kwa migawanyo yao wanaume wote katika Israeli wenye miaka ishirini na kuendelea ambao wanaweza kutumika katika jeshi.

  4. Mwanaume mmoja kutoka kila kabila, kila aliye kiongozi wa jamaa yake, atawasaidia.

  5. Haya ndiyo majina ya wanaume watakaowasaidia: “kutoka Reubeni, ni Elisuri mwana wa Shedeuri;

  6. kutoka Simeoni, ni Shelumieli mwana wa Surishadai;

  7. kutoka Yuda, ni Nashoni mwana wa Aminadabu;

  8. kutoka Isakari, ni Nethaneli mwana wa Suari;

  9. kutoka Zabuloni, ni Eliabu mwana wa Heloni;

  10. kutoka wana wa Yosefu: kutoka Efraimu, ni Elishama mwana wa Amihudi; kutoka Manase, ni Gamalieli mwana wa Pedasuri;

  11. kutoka Benyamini, ni Abidani mwana wa Gideoni;

  12. kutoka Dani, ni Ahiezeri mwana wa Amishadai;

  13. kutoka Asheri, ni Pagieli mwana wa Okrani;

  14. kutoka Gadi, ni Eliasafu mwana wa Deueli;

  15. kutoka Naftali, ni Ahira mwana wa Enani.”

  16. Hawa walikuwa wanaume walioteuliwa kutoka jumuiya, viongozi wa makabila ya baba zao. Walikuwa wakuu wa koo za Israeli.

  17. Mose na Aroni wakawachukua wanaume hao waliokuwa wamepewa majina yao,

  18. wakaita jumuiya yote pamoja katika siku ya kwanza ya mwezi wa pili. Watu wakaonyesha nasaba zao kwa koo zao na jamaa zao, nao wanaume waliokuwa na miaka ishirini au zaidi waliorodheshwa kwa majina, mmoja mmoja,

  19. kama Bwana alivyomwagiza Mose. Hivyo aliwahesabu katika Jangwa la Sinai:

  20. Kutoka wazao wa Reubeni, mzaliwa wa kwanza wa kiume wa Israeli: Wanaume wote waliokuwa na miaka ishirini au zaidi ambao waliweza kutumika katika jeshi waliorodheshwa kwa majina, mmoja mmoja, kufuatana na kumbukumbu za koo zao na jamaa zao.

  21. Idadi kutoka kabila la Reubeni ilikuwa watu 46,500.

  22. Kutoka wazao wa Simeoni: Wanaume wote waliokuwa na miaka ishirini au zaidi ambao waliweza kutumika katika jeshi walihesabiwa na kuorodheshwa kwa majina, mmoja mmoja, kufuatana na kumbukumbu za koo zao na jamaa zao.

  23. Idadi kutoka kabila la Simeoni walikuwa watu 59,300.

  24. Kutoka wazao wa Gadi: Wanaume wote waliokuwa na miaka ishirini au zaidi ambao waliweza kutumika katika jeshi waliorodheshwa kwa majina, kufuatana na kumbukumbu za koo zao na jamaa zao.

  25. Idadi kutoka kabila la Gadi walikuwa watu 45,650.