Rukia maudhui

Mistari ya Biblia kuhusu God

662 mistari · 46 vipengele

Mistari muhimu ya Biblia

Chuja kwa kitabu
  1. mwangalie kila mtu mwenye kiburi na umnyenyekeze, waponde waovu mahali wasimamapo.

  2. Wazike wote mavumbini pamoja; wafunge nyuso zao kaburini.

  3. Ndipo mimi mwenyewe nitakukubalia kuwa mkono wako mwenyewe wa kuume unaweza kukuokoa.

  4. “Mwangalie mnyama aitwaye Behemothi, niliyemuumba kama nilivyokuumba wewe, anayekula majani kama ngʼombe.

  5. Tazama basi nguvu alizo nazo kwenye viuno vyake, uwezo alio nao kwenye misuli ya tumbo lake!

  6. Mkia wake hutikisika kama mwerezi; mishipa ya mapaja yake imesukwa pamoja.

  7. Mifupa yake ni bomba za shaba, maungo yake ni kama fito za chuma.

  8. Yeye ni wa kwanza miongoni mwa kazi za Mungu, lakini Muumba wake anaweza kumsogelea kwa upanga wake.

  9. Vilima humletea yeye mazao yake, nao wanyama wote wa porini hucheza karibu naye.

  10. Hulala chini ya mimea ya yungiyungi, katika maficho ya matete kwenye matope.

  11. Hiyo mimea ya yungiyungi humficha kwenye vivuli vyake; miti mirefu karibu na kijito humzunguka.

  12. Wakati mto ufurikapo, yeye hapati mshtuko wa hofu; yeye yu salama, hata kama Yordani ingefurika hadi kwenye kinywa chake.

  13. Je, mtu yeyote anaweza kumkamata yeye akiwa macho, au kumnasa kwa mtego na kutoboa pua yake?

  14. “Je, waweza kumvua Lewiathani kwa ndoano ya samaki, au kufunga ulimi wake kwa kamba?

  15. Waweza kupitisha kamba puani mwake, au kutoboa taya lake kwa kulabu?

  16. Je, ataendelea kukuomba umhurumie? Atasema nawe maneno ya upole?

  17. Je, atafanya agano nawe ili umtwae awe mtumishi wako maisha yake yote?

  18. Je, utamfuga na kumfanya rafiki kama ndege, au kumfunga kamba kwa ajili ya wasichana wako?

  19. Je, wafanyabiashara watabadilishana bidhaa kwa ajili yake? Watamgawanya miongoni mwa wafanyao biashara?

  20. Je, waweza kuijaza ngozi yake kwa vyuma vyenye ncha kali, au kichwa chake kwa mkuki wa kuvulia samaki?

  21. Kama ukiweka mkono wako juu yake, utavikumbuka hivyo vita na kamwe hutarudia tena!

  22. Tumaini lolote la kumtiisha ni kujidanganya; kule kumwona tu kunamwangusha mtu chini.

  23. Hakuna yeyote aliye mkali athubutuye kumchokoza. Ni nani basi awezaye kusimama dhidi yangu?

  24. Ni nani mwenye madai dhidi yangu ili nipate kumlipa? Kila kitu kilicho chini ya mbingu ni mali yangu.

  25. “Sitashindwa kunena juu ya maungo yake, nguvu zake na umbo lake zuri.