- English
- King James KJV
- Complete Jewish CJB
- World English WEBM
- Berean Standard BSB
- American Standard ASV
- Geneva GNV
- Young's Literal YLT
- Douay-Rheims DRC
- International
- Shqip ALB
- العربية SVD
- বাংলা BN-IRV
- မြန်မာ Judson
- 简体文 CUV-S
- 繁體中文 CUV-T
- Čeština BKR
- Nederlands STVE
- Français LSG
- Deutsch SCH
- Ελληνικά Vamvas
- ગુજરાતી GU-IRV
- Hausa HCB
- עברית Hebrew
- हिन्दी HCV
- Magyar KAROLI
- Bahasa Indonesia INDO-TB
- Italiano Diodati
- 日本語 Kougo
- 한국어 Korean
- മലയാളം MAL
- मराठी MRCV
- Norsk DNB
- فارسی OPV
- Polski BG
- Português Almeida
- Română Cornilescu
- Русский Synodal
- Español RVG
- Kiswahili Neno
- Svenska SV1917
- Tagalog TAG-ADB
- தமிழ் TCV
- తెలుగు TSA
- ภาษาไทย THAI-KJV
- Українська Ohienko
- Tiếng Việt CADMAN
- Yorùbá YCB
Mistari ya Biblia kuhusu God
Mistari muhimu ya Biblia
Ni nani awezaye kumvua gamba lake la nje? Ni nani awezaye kumsogelea na lijamu?
Nani athubutuye kuufungua mlango wa kinywa chake, kilichozungukwa na meno yake ya kutisha pande zote?
Mgongo wake una safu za ngao zilizoshikamanishwa imara pamoja;
kila moja iko karibu sana na mwenzake, wala hakuna hewa iwezayo kupita kati yake.
Zimeunganishwa imara kila moja na nyingine; zimengʼangʼaniana pamoja wala haziwezi kutenganishwa.
Akipiga chafya mwanga humetameta; macho yake ni kama mionzi ya mapambazuko.
Mienge iwakayo humiminika kutoka kinywani mwake; cheche za moto huruka nje.
Moshi hufuka kutoka puani mwake, kama kutoka kwenye chungu kinachotokota kwa moto wa matete.
Pumzi yake huwasha makaa ya mawe, nayo miali ya moto huruka kutoka kinywani mwake.
Nguvu hukaa katika shingo yake; utisho hutangulia mbele yake.
Mikunjo ya nyama yake imeshikamana imara pamoja; iko imara na haiwezi kuondolewa.
Kifua chake ni kigumu kama mwamba, kigumu kama jiwe la chini la kusagia.
Ainukapo, mashujaa wanaogopa; hurudi nyuma mbele yake anapokwenda kwa kishindo.
Upanga unaomfikia haumdhuru, wala mkuki au mshale wala fumo.
Chuma hukiona kama unyasi, na shaba kama mti uliooza.
Mishale haimfanyi yeye akimbie; mawe ya kombeo kwake ni kama makapi.
Rungu kwake huwa kama kipande cha jani kavu; hucheka sauti za kugongana kwa mkuki.
Sehemu zake za chini kwenye tumbo zina menomeno na mapengo kama vigae vya chungu, zikiacha mburuzo kwenye matope kama chombo chenye meno cha kupuria.
Huvisukasuka vilindi kama sufuria kubwa ichemkayo, na kukoroga bahari kama chungu cha marhamu.
Anapopita nyuma yake huacha mkondo unaometameta; mtu angedhani vilindi vilikuwa na mvi.
Hakuna chochote duniani kinacholingana naye: yeye ni kiumbe kisicho na woga.
Yeye huwatazama chini wale wote wenye kujivuna; yeye ni mfalme juu ya wote wenye kiburi.”
Ndipo Ayubu akamjibu Bwana:
“Ninajua ya kuwa unaweza kufanya mambo yote, wala hakuna mpango wako unaoweza kuzuilika.
Uliuliza, ‘Ni nani huyu afichaye mashauri yangu bila maarifa?’ Hakika nilisema juu ya mambo niliyokuwa siyaelewi, mambo ya ajabu mno kwangu mimi kuyajua.