Rukia maudhui

Mistari ya Biblia kuhusu God

662 mistari · 46 vipengele

Mistari muhimu ya Biblia

Chuja kwa kitabu
  1. Mkononi mwake mna vilindi vya dunia, na vilele vya milima ni mali yake.

  2. Bahari ni yake, kwani ndiye aliifanya, na mikono yake iliumba nchi kavu.

  3. Ee nafsi yangu, umhimidi Bwana. Ee Bwana Mungu wangu, wewe ni mkuu sana, umejivika utukufu na enzi.

  4. Amejifunika katika nuru kama vile kwa vazi, amezitandaza mbingu kama hema

  5. na kuziweka nguzo za orofa yake juu ya maji. Huyafanya mawingu kuwa gari lake, na hupanda kwenye mbawa za upepo.

  6. Huzifanya pepo kuwa wajumbe wake, miali ya moto watumishi wake.

  7. Ameiweka dunia kwenye misingi yake, haiwezi kamwe kuondoshwa.

  8. Uliifunika kwa kilindi kama kwa vazi, maji yalisimama juu ya milima.

  9. Lakini kwa kukemea kwako maji yalikimbia, kwa sauti ya radi yako yakatoroka,

  10. yakapanda milima, yakateremka mabondeni, hadi mahali pale ulipoyakusudia.

  11. Uliyawekea mpaka ambao hayawezi kuuvuka, kamwe hayataifunika dunia tena.

  12. Huzifanya chemchemi zimwage maji mabondeni, hutiririka kati ya milima.

  13. Huwapa maji wanyama wote wa kondeni, punda-mwitu huzima kiu yao.

  14. Ndege wa angani hufanya viota kando ya maji, huimba katikati ya matawi.

  15. Huinyeshea milima kutoka orofa zake, dunia inatoshelezwa kwa matunda ya kazi yake.

  16. Huyafanya majani ya mifugo yaote, na mimea kwa watu kulima, wajipatie chakula kutoka ardhini:

  17. divai ya kuufurahisha moyo wa mwanadamu, mafuta kwa ajili ya kungʼarisha uso wake, na mkate wa kutia mwili nguvu.

  18. Miti ya Bwana inanyeshewa vizuri, mierezi ya Lebanoni aliyoipanda.

  19. Humo ndege hufanya viota vyao, korongo ana nyumba yake kwenye msunobari.

  20. Milima mirefu ni makao ya mbuzi-mwitu, majabali ni kimbilio la pelele.

  21. Mwezi hugawanya majira, na jua hutambua wakati wake wa kutua.

  22. Unaleta giza, kunakuwa usiku, wanyama wote wa mwituni huzurura.

  23. Simba hunguruma kwa mawindo yao, na kutafuta chakula chao kutoka kwa Mungu.

  24. Jua huchomoza, nao huondoka, hurudi na kulala katika mapango yao.

  25. Kisha mwanadamu huenda kazini mwake, katika kazi yake mpaka jioni.