Rukia maudhui

Mistari ya Biblia kuhusu God

662 mistari · 46 vipengele

Mistari muhimu ya Biblia

Chuja kwa kitabu
  1. Ee Bwana, jinsi matendo yako yalivyo mengi! Kwa hekima ulizifanya zote, dunia imejaa viumbe vyako.

  2. Pale kuna bahari, kubwa na yenye nafasi tele, imejaa viumbe visivyo na idadi, vitu vyenye uhai vikubwa na vidogo.

  3. Huko meli huenda na kurudi, pia Lewiathani, uliyemuumba acheze ndani yake.

  4. Hawa wote wanakutazamia wewe, uwape chakula chao kwa wakati wake.

  5. Wakati unapowapa, wanakikusanya, unapofumbua mkono wako, wao wanashibishwa mema.

  6. Unapoficha uso wako, wanapata hofu, unapoondoa pumzi yao, wanakufa na kurudi mavumbini.

  7. Unapopeleka Roho wako, wanaumbwa, nawe huufanya upya uso wa dunia.

  8. Utukufu wa Bwana na udumu milele, Bwana na azifurahie kazi zake:

  9. yeye aitazamaye dunia, nayo ikatetemeka, aigusaye milima, nayo ikatoa moshi.

  10. Wengine walisafiri baharini kwa meli, walikuwa wafanyabiashara kwenye maji makuu.

  11. Waliziona kazi za Bwana, matendo yake ya ajabu kilindini.

  12. Kwa maana alisema na kuamsha tufani iliyoinua mawimbi juu.

  13. Yakainuka juu mbinguni, yakashuka chini hadi vilindini, katika hatari hii ujasiri wao uliyeyuka.

  14. Kazi za mikono yake ni za uaminifu na haki, mausia yake yote ni ya kuaminika.

  15. Zinadumu milele na milele, zikifanyika kwa uaminifu na unyofu.

  16. Aliwapa watu wake ukombozi, aliamuru agano lake milele: jina lake ni takatifu na la kuogopwa.

  17. Ee Bwana, neno lako ni la milele, linasimama imara mbinguni.

  18. Uaminifu wako unaendelea kwa vizazi vyote, umeiumba dunia, nayo inadumu.

  19. Sheria zako zinadumu hadi leo, kwa kuwa vitu vyote vinakutumikia.

  20. Hatauacha mguu wako uteleze, yeye akulindaye hatasinzia,

  21. hakika, yeye alindaye Israeli hatasinzia wala hatalala usingizi.

  22. Bwana hufanya lolote apendalo, mbinguni na duniani, katika bahari na vilindi vyake vyote.

  23. Hufanya mawingu kupanda kutoka miisho ya dunia; hupeleka umeme wa radi pamoja na mvua na huleta upepo kutoka ghala zake.

  24. Ambaye kwa ufahamu wake aliziumba mbingu, Fadhili zake zadumu milele.

  25. Ambaye aliitandaza dunia juu ya maji, Fadhili zake zadumu milele.