Rukia maudhui

Mistari ya Biblia kuhusu God

662 mistari · 46 vipengele

Mistari muhimu ya Biblia

Chuja kwa kitabu
  1. “Ulisema, ‘Sikiliza sasa, nami nitanena; nitakuuliza swali, nawe yakupasa kunijibu.’

  2. Masikio yangu yalikuwa yamesikia habari zako, lakini sasa macho yangu yamekuona.

  3. Kwa hiyo najidharau mwenyewe, na kutubu katika mavumbi na majivu.”

  4. Nikiziangalia mbingu zako, kazi ya vidole vyako, mwezi na nyota, ulizoziratibisha,

  5. mwanadamu ni kitu gani hata unamfikiria, binadamu ni nani hata unamjali?

  6. Umemfanya chini kidogo kuliko viumbe wa mbinguni, ukamvika taji ya utukufu na heshima.

  7. Umemfanya mtawala juu ya kazi za mikono yako; umeweka vitu vyote chini ya miguu yake.

  8. Zaburi ya Daudi. Dunia ni mali ya Bwana, na vyote vilivyomo ndani yake, ulimwengu, na wote waishio ndani yake,

  9. maana aliiwekea misingi yake baharini na kuifanya imara juu ya maji.

  10. Kwa neno la Bwana mbingu ziliumbwa, jeshi lao la angani kwa pumzi ya kinywa chake.

  11. Ameyakusanya maji ya bahari kama kwenye chungu; vilindi vya bahari ameviweka katika ghala.

  12. Mchana ni wako, nao usiku ni wako pia, uliziweka jua na mwezi.

  13. Ni wewe uliyeiweka mipaka yote ya dunia, ulifanya kiangazi na masika.

  14. Akalipeleka Sanduku la nguvu zake utumwani, utukufu wake mikononi mwa adui.

  15. Aliachia watu wake wauawe kwa upanga, akaukasirikia sana urithi wake.

  16. Utenzi wa Ethani Mwezrahi. Nitaimba juu ya upendo mkuu wa Bwana milele; kwa kinywa changu nitajulisha uaminifu wako ujulikane kwa vizazi vyote.

  17. Nitatangaza kuwa upendo wako unasimama imara milele na uaminifu wako umeuthibitisha mbinguni.

  18. Mbingu ni zako, nayo nchi pia ni yako, uliuwekea ulimwengu msingi pamoja na vyote vilivyomo.

  19. Uliumba kaskazini na kusini; Tabori na Hermoni wanaliimbia jina lako kwa furaha.

  20. lakini sitauondoa upendo wangu kwake, wala sitausaliti uaminifu wangu kamwe.

  21. Mimi sitavunja agano langu wala sitabadili lile ambalo midomo yangu imelitamka.

  22. Zaburi. Wimbo wa siku ya Sabato. Ni vyema kumshukuru Bwana na kuliimbia jina lako, Ee Uliye Juu Sana,

  23. kuutangaza upendo wako asubuhi, na uaminifu wako wakati wa usiku,

  24. Wakati wa uzee watakuwa bado wanazaa matunda, watakuwa wabichi tena wamejaa nguvu,

  25. wakitangaza, “Bwana ni mkamilifu; yeye ni Mwamba wangu, na ndani yake hamna uovu.”