Rukia maudhui

circa 1010–970 BC

The Reign of David

David unites the tribes, conquers Jerusalem, and establishes Israel's golden age—even through deep personal failure.

1,230 mistari · 2 vitabu vimehusishwa

Mistari ya kipindi hiki

Chuja kwa kitabu
  1. 1 Nyakati 11:17takriban 1055 KK

    Daudi akatamani maji, akasema, “Laiti mtu angenipatia maji ya kunywa kutoka kisima kilichoko karibu na lango la Bethlehemu!”

  2. 1 Nyakati 11:18takriban 1055 KK

    Kwa hivyo wale watatu, wakapita katikati ya safu za Wafilisti, wakachota maji kutoka kwa kisima kilicho karibu na lango la Bethlehemu, wakamletea Daudi. Lakini yeye akakataa kuyanywa. Badala yake, aliyamimina mbele za Bwana.

  3. 1 Nyakati 11:19takriban 1055 KK

    Akasema, “Mungu apishie mbali kwamba nifanye hivi! Je kweli, niinywe damu ya watu hawa waliohatarisha maisha yao?” Kwa sababu walihatarisha maisha yao kuyaleta yale maji, Daudi hakukubali kuyanywa. Huo ndio uliokuwa ujasiri wa wale mashujaa watatu.

  4. 1 Nyakati 11:20takriban 1055 KK

    Abishai, ndugu yake Yoabu ndiye alikuwa kiongozi wa hao Watatu. Aliinua mkuki wake dhidi ya watu 300, ambao aliwaua, kwa hiyo naye akawa na sifa kama hao Watatu.

  5. 1 Nyakati 11:21takriban 1055 KK

    Alitunukiwa heshima maradufu ya wale Watatu, akawa jemadari wao, ingawa hakuhesabiwa miongoni mwao.

  6. 1 Nyakati 11:22takriban 1055 KK

    Benaya, mwana wa Yehoyada alikuwa mpiganaji hodari kutoka Kabseeli ambaye alifanya mambo makubwa ya ujasiri. Aliwaua mashujaa wawili waliokuwa hodari kuliko wote wa Moabu. Pia alishuka shimoni kulipokuwa na theluji na kumuua simba.

  7. 1 Nyakati 11:23takriban 1055 KK

    Alimuua Mmisri aliyekuwa na urefu kama dhiraa tano. Ingawa Mmisri alikuwa na mkuki kama mti wa mfumaji mkononi mwake, Benaya alimwendea na rungu. Akamnyangʼanya Mmisri mkuki wake na kumuua nao.

  8. 1 Nyakati 11:24takriban 1055 KK

    Haya yalikuwa mambo ya ushujaa ya Benaya mwana wa Yehoyada; naye pia alikuwa maarufu kama wale mashujaa watatu.

  9. 1 Nyakati 11:25takriban 1055 KK

    Yeye aliheshimiwa zaidi ya wale Thelathini, lakini hakujumuishwa miongoni mwa wale Watatu: Daudi akamweka kuwa kiongozi wa walinzi wake.

  10. 1 Nyakati 11:26takriban 1055 KK

    Wale watu mashujaa walikuwa: Asaheli nduguye Yoabu, Elhanani mwana wa Dodo kutoka Bethlehemu,

  11. 1 Nyakati 11:27takriban 1055 KK

    Shamothi Mharori, Helesi Mpeloni,

  12. 1 Nyakati 11:28takriban 1055 KK

    Ira mwana wa Ikeshi kutoka Tekoa, Abiezeri kutoka Anathothi,

  13. 1 Nyakati 11:29takriban 1055 KK

    Sibekai Mhushathi, Ilai Mwahohi,

  14. 1 Nyakati 11:30takriban 1055 KK

    Maharai Mnetofathi, Heledi mwana wa Baana, Mnetofathi,

  15. 1 Nyakati 11:31takriban 1055 KK

    Itai mwana wa Ribai kutoka Gibea ya Benyamini, Benaya Mpirathoni,

  16. 1 Nyakati 11:32takriban 1055 KK

    Hurai kutoka mabonde ya Gaashi, Abieli Mwaribathi,

  17. 1 Nyakati 11:33takriban 1055 KK

    Azmawethi Mbaharumi, Eliaba Mshaalboni,

  18. 1 Nyakati 11:34takriban 1055 KK

    wana wa Hashemu Mgiloni, Yonathani mwana wa Shagee Mharari,

  19. 1 Nyakati 11:35takriban 1055 KK

    Ahiamu mwana wa Sakari Mharari, Elifale mwana wa Uru,

  20. 1 Nyakati 11:36takriban 1055 KK

    Heferi Mmekerathi, Ahiya Mpeloni,

  21. 1 Nyakati 11:37takriban 1055 KK

    Hezro Mkarmeli, Naarai mwana wa Ezbai,

  22. 1 Nyakati 11:38takriban 1055 KK

    Yoeli nduguye Nathani, Mibhari mwana wa Hagri,

  23. 1 Nyakati 11:39takriban 1055 KK

    Seleki Mwamoni, Naharai Mbeerothi, mbeba silaha wa Yoabu mwana wa Seruya,

  24. 1 Nyakati 11:40takriban 1055 KK

    Ira Mwithiri, Garebu Mwithiri,

  25. 1 Nyakati 11:41takriban 1055 KK

    Uria Mhiti, Zabadi mwana wa Alai,