Rukia maudhui

circa 6 BC – AD 30

The Life of Jesus

The eternal Son of God enters history: born in Bethlehem, baptized in the Jordan, crucified at Golgotha, raised on the third day.

3,779 mistari · 4 vitabu vimehusishwa

Mistari ya kipindi hiki

Chuja kwa kitabu
  1. Yohana 14:2takriban 33 BK

    Nyumbani kwa Baba yangu kuna makao mengi. Kama sivyo, ningeliwaambia. Naenda kuwaandalia makao.

  2. Yohana 14:3takriban 33 BK

    Nami nikienda na kuwaandalia makao, nitarudi tena na kuwachukua mkae pamoja nami, ili mahali nilipo, nanyi mpate kuwepo.

  3. Yohana 14:4takriban 33 BK

    Ninyi mnajua njia ya kufika ninakokwenda.”

  4. Yohana 14:5takriban 33 BK

    Tomaso akamwambia, “Bwana, sisi hatujui unakokwenda, tutaijuaje njia?”

  5. Yohana 14:6takriban 33 BK

    Yesu akawaambia, “Mimi ndimi njia na kweli na uzima. Mtu hawezi kuja kwa Baba isipokuwa kwa kupitia kwangu.

  6. Yohana 14:7takriban 33 BK

    Kama mngenijua mimi, mngemjua na Baba pia. Tangu sasa, mnamjua Baba yangu, tena mmemwona.”

  7. Yohana 14:8takriban 33 BK

    Filipo akamwambia, “Bwana, tuonyeshe Baba yako yatosha.”

  8. Yohana 14:9takriban 33 BK

    Yesu akamjibu, “Filipo, nimekaa nanyi muda huu wote hata usinijue? Mtu yeyote aliyeniona mimi, amemwona Baba. Sasa wawezaje kusema, ‘Tuonyeshe Baba’?

  9. Yohana 14:10takriban 33 BK

    Je, huamini ya kuwa mimi niko ndani ya Baba, naye Baba yuko ndani yangu? Maneno ninayowaambia siyasemi kwa ajili yangu mwenyewe, bali Baba akaaye ndani yangu ndiye atendaye hizi kazi.

  10. Yohana 14:11takriban 33 BK

    Nisadiki mimi kwamba niko ndani ya Baba na Baba yuko ndani yangu, la sivyo, niaminini kwa sababu ya zile kazi nizitendazo.

  11. Yohana 14:12takriban 33 BK

    Amin, amin nawaambia, yeyote aniaminiye mimi, kazi nizifanyazo yeye atazifanya, naam na kubwa kuliko hizi atazifanya, kwa sababu mimi ninakwenda kwa Baba.

  12. Yohana 14:13takriban 33 BK

    Nanyi mkiomba lolote kwa Jina langu, hilo nitalifanya, ili Baba apate kutukuzwa katika Mwana.

  13. Yohana 14:14takriban 33 BK

    Kama mkiniomba lolote kwa Jina langu nitalifanya.

  14. Yohana 14:15takriban 33 BK

    “Kama mnanipenda, mtazishika amri zangu.

  15. Yohana 14:16takriban 33 BK

    Nami nitamwomba Baba, naye atawapa Msaidizi mwingine akae nanyi milele.

  16. Yohana 14:17takriban 33 BK

    Huyo ndiye Roho wa kweli ambaye ulimwengu hauwezi kumpokea, kwa sababu haumwoni wala haumjui. Ninyi mnamjua kwa kuwa yuko pamoja nanyi naye anakaa ndani yenu.

  17. Yohana 14:18takriban 33 BK

    Sitawaacha ninyi yatima, naja kwenu.

  18. Yohana 14:19takriban 33 BK

    Bado kitambo kidogo ulimwengu hautaniona tena, ila ninyi mtaniona, kwa kuwa mimi ni hai, ninyi nanyi mtakuwa hai.

  19. Yohana 14:20takriban 33 BK

    Wakati huo mtajua ya kuwa mimi niko ndani ya Baba na ninyi mko ndani yangu na mimi niko ndani yenu.

  20. Yohana 14:21takriban 33 BK

    Yeyote mwenye amri zangu na kuzishika ndiye anipendaye, naye anipendaye atapendwa na Baba yangu, nami nitampenda na kujidhihirisha kwake.”

  21. Yohana 14:22takriban 33 BK

    Ndipo Yuda, siyo Iskariote, akamwambia, “Bwana, itakuwaje kwamba utajidhihirisha kwetu na si kwa ulimwengu?”

  22. Yohana 14:23takriban 33 BK

    Yesu akamjibu, “Mtu yeyote akinipenda atalishika neno langu na Baba yangu atampenda, nasi tutakuja kwake na kufanya makao yetu kwake.

  23. Yohana 14:24takriban 33 BK

    Mtu yeyote asiyenipenda hayashiki maneno yangu na maneno niliyowapa si yangu bali ni ya Baba aliyenituma.

  24. Yohana 14:25takriban 33 BK

    “Nimewaambia mambo haya yote wakati bado niko pamoja nanyi.

  25. Yohana 14:26takriban 33 BK

    Lakini huyo Msaidizi, yaani, huyo Roho Mtakatifu, ambaye Baba atamtuma kwenu kwa Jina langu, atawafundisha mambo yote na kuwakumbusha yote niliyowaambia.