Rukia maudhui

circa 6 BC – AD 30

The Life of Jesus

The eternal Son of God enters history: born in Bethlehem, baptized in the Jordan, crucified at Golgotha, raised on the third day.

3,779 mistari · 4 vitabu vimehusishwa

Mistari ya kipindi hiki

Chuja kwa kitabu
  1. Yohana 14:27takriban 33 BK

    Amani nawaachia, amani yangu nawapa, amani hii niwapayo si kama ile ulimwengu utoayo. Msifadhaike mioyoni mwenu, wala msiogope.

  2. Yohana 14:28takriban 33 BK

    “Mlinisikia nikisema, ‘Ninakwenda zangu, lakini nitarudi tena.’ Kama kweli mngelinipenda mngelifurahi kwa kuwa naenda kwa Baba, kwani Baba ni mkuu kuniliko mimi.

  3. Yohana 14:29takriban 33 BK

    Nimewaambia mambo haya kabla hayajatukia, ili yatakapotukia mpate kuamini.

  4. Yohana 14:30takriban 33 BK

    Sitasema nanyi zaidi, kwa sababu yule mkuu wa ulimwengu huu anakuja, naye hana kitu kwangu,

  5. Yohana 14:31takriban 33 BK

    lakini ulimwengu upate kujua kuwa ninampenda Baba, nami hufanya vile Baba alivyoniamuru. “Haya inukeni; twendeni zetu.

  6. Yohana 15:1takriban 33 BK

    “Mimi ndimi mzabibu wa kweli na Baba yangu ndiye mkulima.

  7. Yohana 15:2takriban 33 BK

    Kila tawi ndani yangu lisilozaa matunda, Baba yangu hulikata, nalo kila tawi lizaalo, hulisafisha ili lipate kuzaa matunda zaidi.

  8. Yohana 15:3takriban 33 BK

    Ninyi mmekwisha kuwa safi kwa sababu ya lile neno nililonena nanyi.

  9. Yohana 15:4takriban 33 BK

    Kaeni ndani yangu, nami nikae ndani yenu. Kama vile tawi lisivyoweza kuzaa matunda lisipokaa ndani ya mzabibu, vivyo hivyo ninyi msipokaa ndani yangu hamwezi kuzaa matunda.

  10. Yohana 15:5takriban 33 BK

    “Mimi ni mzabibu, ninyi ni matawi. Akaaye ndani yangu, nami ndani yake, huyo huzaa sana, maana pasipo mimi ninyi hamwezi kufanya jambo lolote.

  11. Yohana 15:6takriban 33 BK

    Mtu yeyote asipokaa ndani yangu, hutupwa nje kama tawi na kunyauka. Matawi kama hayo hukusanywa na kutupwa motoni, yakateketea.

  12. Yohana 15:7takriban 33 BK

    Ninyi mkikaa ndani yangu na maneno yangu yakikaa ndani yenu, ombeni lolote mtakalo, nanyi mtatendewa.

  13. Yohana 15:8takriban 33 BK

    Kwa hiyo Baba yangu hutukuzwa, kwa vile mzaavyo matunda mengi, nanyi mtakuwa wanafunzi wangu.

  14. Yohana 15:9takriban 33 BK

    “Kama vile Baba alivyonipenda mimi, hivyo ndivyo mimi nilivyowapenda ninyi. Basi kaeni katika pendo langu.

  15. Yohana 15:10takriban 33 BK

    Mkizishika amri zangu mtakaa katika pendo langu, kama mimi nilivyozishika amri za Baba yangu na kukaa katika pendo lake.

  16. Yohana 15:11takriban 33 BK

    Nimewaambia mambo haya ili furaha yangu iwe ndani yenu na furaha yenu iwe kamili.

  17. Yohana 15:12takriban 33 BK

    Amri yangu ndiyo hii: Mpendane kama mimi nilivyowapenda ninyi.

  18. Yohana 15:13takriban 33 BK

    Hakuna mtu mwenye upendo mkuu kuliko huu, mtu kuutoa uhai wake kwa ajili ya rafiki zake.

  19. Yohana 15:14takriban 33 BK

    Ninyi ni rafiki zangu mkifanya ninayowaamuru.

  20. Yohana 15:15takriban 33 BK

    Siwaiti ninyi watumishi tena, kwa sababu watumishi hawajui bwana wao analofanya, bali nimewaita ninyi rafiki, kwa maana nimewajulisha mambo yote niliyoyasikia kutoka kwa Baba yangu.

  21. Yohana 15:16takriban 33 BK

    Si ninyi mlionichagua, bali mimi ndiye niliyewachagua ninyi na kuwaweka mwende mkazae matunda, na matunda yenu yapate kudumu. Ili nalo lolote mtakalomwomba Baba katika Jina langu, awape ninyi.

  22. Yohana 15:17takriban 33 BK

    Amri yangu ndiyo hii: Mpendane.

  23. Yohana 15:18takriban 33 BK

    “Kama ulimwengu ukiwachukia ninyi, kumbukeni kwamba ulinichukia mimi kabla yenu.

  24. Yohana 15:19takriban 33 BK

    Kama mngekuwa wa ulimwengu, ulimwengu ungeliwapenda kama vile unavyowapenda walio wake. Kwa sababu ninyi si wa ulimwengu, lakini mimi nimewachagua kutoka ulimwengu, hii ndiyo sababu ulimwengu unawachukia.

  25. Yohana 15:20takriban 33 BK

    Kumbukeni lile neno nililowaambia, ‘Hakuna mtumishi aliye mkuu kuliko bwana wake.’ Kama wamenitesa mimi, nanyi pia watawatesa. Kama wamelishika neno langu, watalishika na neno lenu pia.