Rukia maudhui

circa AD 48–96

Letters to the Churches

Paul and other apostles write to strengthen, correct, and encourage the scattered churches across the Roman world.

2,767 mistari · 21 vitabu vimehusishwa

Mistari ya kipindi hiki

Chuja kwa kitabu
  1. 1 Wakorintho 7:19takriban 59 BK

    Kutahiriwa si kitu, na kutokutahiriwa si kitu. Lakini kuzitii amri za Mungu ndilo jambo muhimu.

  2. 1 Wakorintho 7:20takriban 59 BK

    Basi kila mmoja wenu na abaki katika hali aliyoitwa nayo.

  3. 1 Wakorintho 7:21takriban 59 BK

    Je, wewe ulipoitwa ulikuwa mtumwa? Jambo hilo lisikusumbue. Ingawaje unaweza kupata uhuru, tumia nafasi uliyo nayo sasa kuliko wakati mwingine wowote.

  4. 1 Wakorintho 7:22takriban 59 BK

    Kwa maana yeyote aliyeitwa katika Bwana akiwa mtumwa yeye ni mtu huru kwa Bwana, kama vile yeyote aliyekuwa huru alipoitwa yeye ni mtumwa wa Kristo.

  5. 1 Wakorintho 7:23takriban 59 BK

    Mlinunuliwa kwa gharama; msiwe watumwa wa wanadamu.

  6. 1 Wakorintho 7:24takriban 59 BK

    Ndugu zangu, kama kila mtu alivyoitwa, akae katika wito wake alioitiwa na Mungu.

  7. 1 Wakorintho 7:25takriban 59 BK

    Basi, kuhusu wale walio bikira, mimi sina amri kutoka kwa Bwana, lakini mimi natoa shauri kama mtu ambaye ni mwaminifu kwa rehema za Bwana.

  8. 1 Wakorintho 7:26takriban 59 BK

    Kwa sababu ya shida iliyoko kwa sasa, naona ni vyema mkibaki kama mlivyo.

  9. 1 Wakorintho 7:27takriban 59 BK

    Je, umeolewa? Basi usitake talaka. Je, hujaoa? Usitafute mke.

  10. 1 Wakorintho 7:28takriban 59 BK

    Lakini kama ukioa, hujatenda dhambi; na kama bikira akiolewa, hajatenda dhambi. Lakini wale wanaooa watakabiliana na matatizo mengi katika maisha haya, nami nataka kuwazuilia hayo.

  11. 1 Wakorintho 7:29takriban 59 BK

    Lakini ndugu zangu, nina maana kwamba muda uliobaki ni mfupi. Tangu sasa wale waliooa waishi kama wasio na wake;

  12. 1 Wakorintho 7:30takriban 59 BK

    nao wanaoomboleza, kama ambao hawaombolezi; wenye furaha kama wasiokuwa nayo; wale wanaonunua, kama vile vitu walivyonunua si mali yao;

  13. 1 Wakorintho 7:31takriban 59 BK

    nao wale wanaoshughulika na vitu vya dunia hii, kama ambao hawahusiki navyo. Kwa maana dunia hii kama tunavyoiona sasa inapita.

  14. 1 Wakorintho 7:32takriban 59 BK

    Ningetaka msiwe na masumbufu. Mwanaume ambaye hajaoa anajishughulisha na mambo ya Bwana, jinsi ya kumpendeza Bwana.

  15. 1 Wakorintho 7:33takriban 59 BK

    Lakini mwanaume aliyeoa anajishughulisha na mambo ya dunia, jinsi ya kumfurahisha mkewe,

  16. 1 Wakorintho 7:34takriban 59 BK

    na mawazo yake yamegawanyika. Mwanamke asiyeolewa hujishughulisha na mambo ya Bwana: lengo lake ni awe mtakatifu kimwili na kiroho. Lakini yule aliyeolewa hujishughulisha na mambo ya dunia, jinsi atakavyoweza kumfurahisha mumewe.

  17. 1 Wakorintho 7:35takriban 59 BK

    Ninasema haya kwa faida yenu wenyewe, sio ili kuwawekea vizuizi bali mpate kuishi kwa jinsi ilivyo vyema bila kuvutwa pengine katika kujitoa kwenu kwa Bwana.

  18. 1 Wakorintho 7:36takriban 59 BK

    Kama mtu yeyote anadhani kwamba hamtendei ilivyo sawa mwanamwali ambaye amemposa, naye akiwa umri wake unazidi kuendelea na mtu huyo anajisikia kwamba inampasa kuoa, afanye kama atakavyo. Yeye hatendi dhambi. Yawapasa waoane.

  19. 1 Wakorintho 7:37takriban 59 BK

    Lakini mwanaume ambaye ameamua moyoni mwake kutooa bila kulazimishwa na mtu yeyote, bali anaweza kuzitawala tamaa zake kutomwoa huyo mwanamwali, basi anafanya ipasavyo.

  20. 1 Wakorintho 7:38takriban 59 BK

    Hivyo basi, mwanaume amwoaye mwanamwali afanya vyema, lakini yeye asiyemwoa afanya vyema zaidi.

  21. 1 Wakorintho 7:39takriban 59 BK

    Mwanamke aliyeolewa amefungwa na sheria maadamu mumewe yu hai. Lakini mumewe akifa, basi mwanamke huyo yuko huru kuolewa na mume mwingine ampendaye, lakini lazima awe katika Bwana.

  22. 1 Wakorintho 7:40takriban 59 BK

    Lakini kwa maoni yangu, angekuwa na furaha zaidi akibaki alivyo. Nami nadhani pia nina Roho wa Mungu.

  23. 1 Wakorintho 8:1takriban 59 BK

    Sasa kuhusu chakula kilichotolewa sadaka kwa sanamu, tunajua kwamba “sisi sote tuna ujuzi.” Lakini ujuzi hujivuna, bali upendo hujenga.

  24. 1 Wakorintho 8:2takriban 59 BK

    Mtu yeyote anayedhani kwamba anajua kitu, bado hajui kama impasavyo kujua.

  25. 1 Wakorintho 8:3takriban 59 BK

    Lakini mtu ampendaye Mungu, hujulikana naye Mungu.