Rukia maudhui

circa AD 48–96

Letters to the Churches

Paul and other apostles write to strengthen, correct, and encourage the scattered churches across the Roman world.

2,767 mistari · 21 vitabu vimehusishwa

Mistari ya kipindi hiki

Chuja kwa kitabu
  1. 1 Wakorintho 6:14takriban 59 BK

    Naye Mungu aliyemfufua Bwana kutoka kwa wafu atatufufua sisi pia kwa uweza wake.

  2. 1 Wakorintho 6:15takriban 59 BK

    Je, hamjui kwamba miili yenu ni viungo vya Kristo mwenyewe? Je, nichukue viungo vya mwili wa Kristo na kuviunganisha na mwili wa kahaba? La hasha!

  3. 1 Wakorintho 6:16takriban 59 BK

    Hamjui kwamba aliyeungwa na kahaba anakuwa mwili mmoja naye? Kwa kuwa imenenwa, “Hao wawili watakuwa mwili mmoja.”

  4. 1 Wakorintho 6:17takriban 59 BK

    Lakini mtu aliyeungwa na Bwana anakuwa roho moja naye.

  5. 1 Wakorintho 6:18takriban 59 BK

    Ikimbieni zinaa. Dhambi zingine zote atendazo mtu ziko nje ya mwili wake, lakini yeye aziniye hutenda dhambi ndani ya mwili wake mwenyewe.

  6. 1 Wakorintho 6:19takriban 59 BK

    Je, hamjui ya kwamba miili yenu ni hekalu la Roho Mtakatifu akaaye ndani yenu, ambaye mmepewa na Mungu? Ninyi si mali yenu wenyewe,

  7. 1 Wakorintho 6:20takriban 59 BK

    kwa maana mmenunuliwa kwa gharama. Kwa hiyo mtukuzeni Mungu katika miili yenu.

  8. 1 Wakorintho 7:1takriban 59 BK

    Basi kuhusu mambo yale mliyoyaandika: Ni vyema mwanaume asimguse mwanamke.

  9. 1 Wakorintho 7:2takriban 59 BK

    Lakini ili kuepuka zinaa, kila mwanaume na awe na mke wake mwenyewe na kila mwanamke awe na mume wake mwenyewe.

  10. 1 Wakorintho 7:3takriban 59 BK

    Mume atimize wajibu wake wa ndoa kwa mkewe, naye vivyo hivyo mke kwa mumewe.

  11. 1 Wakorintho 7:4takriban 59 BK

    Mwanamke hana mamlaka juu ya mwili wake bali mumewe, wala mume hana mamlaka juu ya mwili wake bali mkewe.

  12. 1 Wakorintho 7:5takriban 59 BK

    Msinyimane, isipokuwa mmekubaliana kufanya hivyo kwa muda fulani ili mweze kujitoa kwa maombi, kisha mrudiane tena ili Shetani asije akapata nafasi ya kuwajaribu kwa sababu ya kutokuwa na kiasi.

  13. 1 Wakorintho 7:6takriban 59 BK

    Nasema haya kama ushauri na si amri.

  14. 1 Wakorintho 7:7takriban 59 BK

    Laiti watu wangekuwa kama mimi nilivyo. Lakini kila mtu amepewa kipawa chake kutoka kwa Mungu, mmoja ana kipawa cha namna hii na mwingine ana cha namna ile.

  15. 1 Wakorintho 7:8takriban 59 BK

    Kwa wale wasiooa na kwa wajane, nasema hivi, ingekuwa vizuri wasioe.

  16. 1 Wakorintho 7:9takriban 59 BK

    Lakini kama hawawezi kujizuia, basi waoe na kuolewa, kwa maana ni afadhali kuoa au kuolewa kuliko kuwaka tamaa.

  17. 1 Wakorintho 7:10takriban 59 BK

    Kwa wale waliooana nawapa amri (si mimi ila ni Bwana): Mke asitengane na mumewe.

  18. 1 Wakorintho 7:11takriban 59 BK

    Lakini akitengana, ni lazima akae bila kuolewa, ama sivyo apatane tena na mumewe. Wala mume asimpe mkewe talaka.

  19. 1 Wakorintho 7:12takriban 59 BK

    Lakini kwa wengine nasema (si Bwana ila ni mimi): Kama ndugu ana mke asiyeamini, naye huyo mke anakubali kuishi pamoja naye, basi asimwache.

  20. 1 Wakorintho 7:13takriban 59 BK

    Naye mwanamke aaminiye kama ameolewa na mwanaume asiyeamini na huyo mume anakubali kuishi naye, basi huyo mwanamke asimwache.

  21. 1 Wakorintho 7:14takriban 59 BK

    Kwa maana huyo mume asiyeamini anatakaswa kupitia mkewe, naye mke asiyeamini anatakaswa kupitia mumewe anayeamini. Kama isingalikuwa hivyo watoto wenu wangalikuwa si safi, lakini ilivyo sasa wao ni watakatifu.

  22. 1 Wakorintho 7:15takriban 59 BK

    Lakini kama yule asiyeamini akijitenga, basi afanye hivyo. Katika hali kama hiyo mwanamke au mwanaume aaminiye hafungwi, kwa sababu Mungu ametuita tuishi kwa amani.

  23. 1 Wakorintho 7:16takriban 59 BK

    Wewe mke, unajuaje kama utamwokoa mumeo? Au wewe mume unajuaje kama utamwokoa mkeo?

  24. 1 Wakorintho 7:17takriban 59 BK

    Lakini kila mtu na aishi maisha aliyopangiwa na Bwana, yale Mungu aliyomwitia. Hii ni sheria ninayoiweka kwa makanisa yote.

  25. 1 Wakorintho 7:18takriban 59 BK

    Je, mtu alikuwa tayari ametahiriwa alipoitwa? Asijifanye asiyetahiriwa. Je, mtu alikuwa hajatahiriwa alipoitwa? Asitahiriwe.