Rukia maudhui

circa 1446 BC

Moses & The Exodus

God raises up Moses to confront Pharaoh; the ten plagues culminate in Israel's dramatic deliverance from four centuries of bondage.

415 mistari · 1 kitabu kimehusishwa

Mistari ya kipindi hiki

  1. Kutoka 12:42takriban 1491 KK

    Kwa sababu Bwana aliutenga usiku ule ili kuwatoa Waisraeli katika nchi ya Misri, katika usiku huu Waisraeli wote wanapaswa kuadhimisha kwa kukesha ili kumheshimu Bwana katika vizazi vijavyo.

  2. Kutoka 12:43takriban 1491 KK

    Bwana akamwambia Mose na Aroni, “Haya ndiyo masharti kwa ajili ya Pasaka: “Mgeni hataruhusiwa kula Pasaka.

  3. Kutoka 12:44takriban 1491 KK

    Mtumwa yeyote ambaye mmemnunua aweza kuila kama mmemtahiri,

  4. Kutoka 12:45takriban 1491 KK

    lakini kibarua yeyote au msafiri haruhusiwi kula.

  5. Kutoka 12:46takriban 1491 KK

    “Sharti iliwe ndani ya nyumba; msichukue nyama yoyote nje ya nyumba hiyo. Msiuvunje mfupa wowote.

  6. Kutoka 12:47takriban 1491 KK

    Jumuiya yote ya Israeli ni lazima waiadhimishe Pasaka hiyo.

  7. Kutoka 12:48takriban 1491 KK

    “Mgeni aishiye miongoni mwenu ambaye anataka kuadhimisha Pasaka ya Bwana ni lazima wanaume wote waliomo nyumbani mwake wawe wametahiriwa, ndipo aweze kushiriki kama mzawa. Mwanaume yeyote asiyetahiriwa haruhusiwi kuila.

  8. Kutoka 12:49takriban 1491 KK

    Sheria iyo hiyo itamuhusu mzawa na mgeni anayeishi miongoni mwenu.”

  9. Kutoka 12:50takriban 1491 KK

    Waisraeli wote walifanya kama vile Bwana alivyomwagiza Mose na Aroni.

  10. Kutoka 12:51takriban 1491 KK

    Siku ile ile Bwana akawatoa Waisraeli katika nchi ya Misri kwa vikosi vyao.

  11. Kutoka 13:1takriban 1491 KK

    Bwana akamwambia Mose,

  12. Kutoka 13:2takriban 1491 KK

    “Niwekeeni wakfu kila mzaliwa wa kwanza wa kiume. Kila mtoto wa kwanza aliye kifungua tumbo miongoni mwa Waisraeli ni mali yangu, akiwa wa mwanadamu au wa mnyama.”

  13. Kutoka 13:3takriban 1491 KK

    Ndipo Mose akawaambia watu, “Ikumbukeni siku hii, siku ambayo mlitoka katika nchi ya Misri, katika nchi ya utumwa, kwa sababu Bwana aliwatoa humo kwa mkono wenye nguvu. Msile chochote kilichotiwa chachu.

  14. Kutoka 13:4takriban 1491 KK

    Leo, katika mwezi wa Abibu, mnatoka.

  15. Kutoka 13:5takriban 1491 KK

    Bwana atakapokuleta katika nchi ya Wakanaani, Wahiti, Waamori, Wahivi na Wayebusi, nchi aliyowaapia baba zako kukupa, nchi itiririkayo maziwa na asali, utaiadhimisha sikukuu hii katika mwezi huu:

  16. Kutoka 13:6takriban 1491 KK

    Kwa siku saba utakula mikate isiyotiwa chachu na katika siku ya saba utamfanyia Bwana sikukuu.

  17. Kutoka 13:7takriban 1491 KK

    Kwa muda wa siku saba utakula mikate isiyotiwa chachu, pasionekane kitu chochote kilicho na chachu miongoni mwako, wala chachu yoyote isionekane popote ndani ya mipaka yako.

  18. Kutoka 13:8takriban 1491 KK

    Siku ile utamwambia mwanao, ‘Nafanya hivi kwa sababu ya jambo ambalo Bwana alinitendea nilipotoka katika nchi ya Misri.’

  19. Kutoka 13:9takriban 1491 KK

    Adhimisho hili, litakuwa kama alama kwenye mkono wako na ukumbusho katika paji lako la uso, kwamba sheria ya Bwana inapaswa iwe kinywani mwako. Kwa kuwa Bwana alikutoa katika nchi ya Misri kwa mkono wake wenye nguvu.

  20. Kutoka 13:10takriban 1491 KK

    Ni lazima uishike amri hii kwa wakati uliopangwa mwaka baada ya mwaka.

  21. Kutoka 13:11takriban 1491 KK

    “Baada ya Bwana kukuingiza katika nchi ya Wakanaani na kukupa nchi hiyo, kama alivyokuahidi kwa kiapo na kwa baba zako,

  22. Kutoka 13:12takriban 1491 KK

    inakupasa kumtolea Bwana mzaliwa wa kwanza wa kila tumbo. Wazaliwa wote wa kwanza wa kiume wa mifugo yako ni mali ya Bwana.

  23. Kutoka 13:13takriban 1491 KK

    Kila mzaliwa wa kwanza wa punda utamkomboa kwa mwana-kondoo, lakini kama hukumkomboa, utamvunja shingo yake. Kila mzaliwa wa kwanza mwanaume miongoni mwa wana wenu utamkomboa.

  24. Kutoka 13:14takriban 1491 KK

    “Katika siku zijazo, mwanao akikuuliza, ‘Hii ina maana gani?’ Mwambie, ‘Kwa mkono wenye nguvu Bwana alitutoa katika nchi ya Misri, kutoka nchi ya utumwa.

  25. Kutoka 13:15takriban 1491 KK

    Farao alipokataa kwa ukaidi kuturuhusu kuondoka, Bwana aliua kila mzaliwa wa kwanza wa Wamisri, mwanadamu na wa mnyama. Hii ndiyo sababu ninatoa dhabihu kwa Bwana mzaliwa wa kwanza wa kiume, wa kila tumbo na kumkomboa kila mzaliwa wa kwanza wa wana wangu.’