Rukia maudhui

circa 1900–1700 BC

Jacob, Joseph & Egypt

Jacob wrestles with God and becomes Israel; Joseph is sold into slavery yet rises to save the world from famine.

840 mistari · 1 kitabu kimehusishwa

Mistari ya kipindi hiki

  1. Mwanzo 33:8takriban 1739 KK

    Esau akauliza, “Una maana gani kuhusu makundi hayo yote niliyokutana nayo?” Akasema, “Ni ili kupata kibali machoni pako, bwana wangu.”

  2. Mwanzo 33:9takriban 1739 KK

    Lakini Esau akamwambia, “Ndugu yangu, tayari nina wingi wa mali. Ulivyo navyo viwe vyako mwenyewe.”

  3. Mwanzo 33:10takriban 1739 KK

    Yakobo akasema, “La hasha! Tafadhali, kama nimepata kibali machoni pako, upokee zawadi hii kutoka kwangu. Kwa maana kuuona uso wako, ni kama kuuona uso wa Mungu, kwa kuwa umenipokea kwa takabali kubwa.

  4. Mwanzo 33:11takriban 1739 KK

    Tafadhali ukubali zawadi iliyoletwa kwako, kwa kuwa Mungu amenineemesha na ninavyo vyote ninavyohitaji.” Kwa sababu Yakobo alisisitiza, Esau akapokea.

  5. Mwanzo 33:12takriban 1739 KK

    Ndipo Esau akasema, “Na tuendelee na safari, nitakuwa pamoja nawe.”

  6. Mwanzo 33:13takriban 1739 KK

    Lakini Yakobo akamwambia, “Bwana wangu unajua kwamba watoto ni wachanga na kwamba ni lazima nitunze hawa kondoo wake na ngʼombe wanaonyonyesha. Wakipelekwa kwa haraka hata kama ni kwa siku moja tu, wanyama wote watakufa.

  7. Mwanzo 33:14takriban 1739 KK

    Hivyo bwana wangu umtangulie mtumishi wako, wakati mimi nikija polepole kwa mwendo wa makundi yaliyo mbele yangu na mwendo wa watoto, mpaka nifike kwa bwana wangu huko Seiri.”

  8. Mwanzo 33:15takriban 1739 KK

    Esau akamwambia, “Basi na niwaache baadhi ya watu wangu pamoja nawe.” Yakobo akauliza, “Lakini kwa nini ufanye hivyo, niache tu nipate kibali machoni pa bwana wangu.”

  9. Mwanzo 33:16takriban 1739 KK

    Hivyo siku hiyo Esau akashika njia akarudi Seiri.

  10. Mwanzo 33:17takriban 1739 KK

    Pamoja na hayo, Yakobo akaenda Sukothi, mahali alipojijengea makazi kwa ajili yake na mabanda kwa ajili ya mifugo yake. Hii ndiyo sababu sehemu ile inaitwa Sukothi.

  11. Mwanzo 33:18takriban 1739 KK

    Baada ya Yakobo kutoka Padan-Aramu, alifika salama katika mji wa Shekemu huko Kanaani na kuweka kambi yake karibu na mji.

  12. Mwanzo 33:19takriban 1739 KK

    Akanunua kiwanja kutoka kwa wana wa Hamori, baba wa Shekemu, kwa bei ya vipande mia vya fedha, ambapo alipiga hema lake.

  13. Mwanzo 33:20takriban 1739 KK

    Pale akajenga madhabahu na kupaita El-Elohe-Israeli.

  14. Mwanzo 34:1takriban 1732 KK

    Basi Dina, binti wa Yakobo aliyezaliwa na Lea, akatoka nje kuwatembelea wanawake wa nchi ile.

  15. Mwanzo 34:2takriban 1732 KK

    Ikawa Shekemu mwana wa Hamori Mhivi, mtawala wa eneo lile alipomwona, akamchukua na kumnajisi.

  16. Mwanzo 34:3takriban 1732 KK

    Moyo wake ukavutwa sana kwa Dina binti Yakobo, akampenda huyu msichana na akazungumza naye kwa kumbembeleza.

  17. Mwanzo 34:4takriban 1732 KK

    Shekemu akamwambia baba yake Hamori, “Nipatie msichana huyu awe mke wangu.”

  18. Mwanzo 34:5takriban 1732 KK

    Yakobo aliposikia kwamba binti yake Dina amenajisiwa, wanawe walikuwa mashambani wakichunga mifugo yake, kwa hiyo akalinyamazia jambo hilo mpaka waliporudi nyumbani.

  19. Mwanzo 34:6takriban 1732 KK

    Kisha Hamori baba yake Shekemu akaenda kuzungumza na Yakobo.

  20. Mwanzo 34:7takriban 1732 KK

    Basi wana wa Yakobo walikuwa wamerudi kutoka mashambani mara tu waliposikia kilichotokea. Walikuwa wamejawa na huzuni na ghadhabu, kwa sababu Shekemu alikuwa amefanya jambo la aibu katika Israeli kwa kukutana kimwili na binti wa Yakobo, kitu ambacho hakingepasa kufanyika.

  21. Mwanzo 34:8takriban 1732 KK

    Lakini Hamori akawaambia, “Moyo wa mwanangu Shekemu umeelekea kwa binti yenu. Tafadhali mpeni awe mke wake.

  22. Mwanzo 34:9takriban 1732 KK

    Oaneni na sisi, tupeni binti zenu, nanyi mchukue binti zetu.

  23. Mwanzo 34:10takriban 1732 KK

    Mwaweza kuishi katikati yetu, nchi ni wazi kwenu. Ishini ndani yake, fanyeni biashara humu na mjipatie mali.”

  24. Mwanzo 34:11takriban 1732 KK

    Kisha Shekemu akamwambia baba yake Dina pamoja na ndugu zake, “Na nipate kibali machoni penu, nami nitawapa chochote mtakachosema.

  25. Mwanzo 34:12takriban 1732 KK

    Niambieni kiasi cha mahari na zawadi nitakayoileta, hata iwe kubwa kiasi gani, nami nitawalipa chochote mtakachodai. Nipeni tu huyu msichana awe mke wangu.”