Rukia maudhui

circa 1900–1700 BC

Jacob, Joseph & Egypt

Jacob wrestles with God and becomes Israel; Joseph is sold into slavery yet rises to save the world from famine.

840 mistari · 1 kitabu kimehusishwa

Mistari ya kipindi hiki

  1. Mwanzo 31:45takriban 1739 KK

    Hivyo Yakobo akachukua jiwe, akalisimamisha kama nguzo.

  2. Mwanzo 31:46takriban 1739 KK

    Akawaambia jamaa yake, “Kusanyeni mawe.” Hivyo wakachukua mawe na kuyakusanya yakawa lundo, wakala chakula hapo karibu na hilo lundo.

  3. Mwanzo 31:47takriban 1739 KK

    Labani akaliita Yegar-Sahadutha na Yakobo akaliita Galeedi.

  4. Mwanzo 31:48takriban 1739 KK

    Labani akasema, “Lundo hili ni shahidi kati yako na mimi leo.” Ndiyo maana likaitwa Galeedi.

  5. Mwanzo 31:49takriban 1739 KK

    Pia liliitwa Mispa, kwa sababu alisema, “Bwana na aweke ulinzi kati yako na mimi wakati kila mmoja akiwa mbali na mwingine.

  6. Mwanzo 31:50takriban 1739 KK

    Kama ukiwatenda mabaya binti zangu au ukioa wake wengine zaidi ya binti zangu, hata ingawa hakuna hata mmoja aliye pamoja nasi, kumbuka kwamba Mungu ni shahidi kati yako na mimi.”

  7. Mwanzo 31:51takriban 1739 KK

    Pia Labani akamwambia Yakobo, “Hili ndilo lundo, na hii ndiyo nguzo niliyoisimamisha kati yako na mimi.

  8. Mwanzo 31:52takriban 1739 KK

    Lundo hili ni shahidi na nguzo hii ni shahidi, kwamba sitavuka lundo hili kuja upande wako kukudhuru, nawe kwamba hutavuka lundo hili na nguzo hii kuja upande wangu kunidhuru.

  9. Mwanzo 31:53takriban 1739 KK

    Mungu wa Abrahamu na Mungu wa Nahori, Mungu wa baba zao, aamue kati yetu.” Hivyo Yakobo akaapa kwa jina la Hofu ya baba yake Isaki.

  10. Mwanzo 31:54takriban 1739 KK

    Yakobo akatoa dhabihu juu ya kilima na akawaalika jamaa zake kula chakula. Baada ya kula, wakalala huko.

  11. Mwanzo 31:55takriban 1739 KK

    Kesho yake asubuhi na mapema, Labani akawabusu wajukuu zake, binti zake na kuwabariki. Kisha akaondoka, akarudi nyumbani.

  12. Mwanzo 32:1takriban 1739 KK

    Yakobo pia akaondoka akaenda zake, nao malaika wa Mungu wakakutana naye.

  13. Mwanzo 32:2takriban 1739 KK

    Yakobo alipowaona, akasema, “Hii ni kambi ya Mungu!” Kwa hiyo akapaita mahali pale Mahanaimu.

  14. Mwanzo 32:3takriban 1739 KK

    Yakobo akatuma wajumbe kumtangulia kwa Esau ndugu yake huko Seiri, katika nchi ya Edomu.

  15. Mwanzo 32:4takriban 1739 KK

    Akawaagiza akisema: “Hili ndilo mtakalomwambia bwana wangu Esau: ‘Mtumishi wako Yakobo anasema, nimekuwa nikiishi pamoja na Labani na nimekuwako huko mpaka sasa.

  16. Mwanzo 32:5takriban 1739 KK

    Ninao ngʼombe na punda, kondoo na mbuzi, watumishi wa kiume na wa kike. Sasa ninatuma ujumbe huu kwa bwana wangu, ili nipate kibali machoni pako.’ ”

  17. Mwanzo 32:6takriban 1739 KK

    Wajumbe waliporudi kwa Yakobo, wakamwambia, “Tulikwenda kuonana na ndugu yako Esau, naye sasa anakuja kukulaki akifuatana na wanaume 400.”

  18. Mwanzo 32:7takriban 1739 KK

    Kwa hofu kuu na huzuni, Yakobo akagawanya watu aliokuwa nao katika makundi mawili, pia akagawanya makundi ya kondoo na mbuzi, na vilevile ngʼombe na ngamia.

  19. Mwanzo 32:8takriban 1739 KK

    Yakobo alifikiri, “Kama Esau akija na kushambulia kundi moja, kundi lililobaki litaweza likanusurika.”

  20. Mwanzo 32:9takriban 1739 KK

    Ndipo Yakobo akaomba, “Ee Mungu wa baba yangu Abrahamu, Mungu wa baba yangu Isaki, Ee Bwana, ambaye uliniambia, ‘Rudi katika nchi yako na jamaa yako, nami nitakufanya ustawi,’

  21. Mwanzo 32:10takriban 1739 KK

    mimi sistahili fadhili na uaminifu wako wote ulionitendea mimi mtumishi wako. Nilikuwa na fimbo tu mkononi mwangu nilipovuka mto huu wa Yordani, lakini sasa ninayo makundi mawili.

  22. Mwanzo 32:11takriban 1739 KK

    Nakuomba, uniokoe na mkono wa ndugu yangu Esau, kwa maana ninaogopa kuwa atakuja kunishambulia, pia mama pamoja na watoto wao.

  23. Mwanzo 32:12takriban 1739 KK

    Lakini umeshasema, ‘Hakika nitakufanya ustawi na kuufanya uzao wako kuwa mwingi kama mchanga wa baharini ambao hauwezi kuhesabika!’ ”

  24. Mwanzo 32:13takriban 1739 KK

    Akalala pale usiku ule, miongoni mwa vitu alivyokuwa navyo, akachagua zawadi kwa ajili ya Esau ndugu yake:

  25. Mwanzo 32:14takriban 1739 KK

    Mbuzi waume ishirini na mbuzi wake 200, kondoo dume ishirini na kondoo wake 200.