Rukia maudhui

circa 1900–1700 BC

Jacob, Joseph & Egypt

Jacob wrestles with God and becomes Israel; Joseph is sold into slavery yet rises to save the world from famine.

840 mistari · 1 kitabu kimehusishwa

Mistari ya kipindi hiki

  1. Mwanzo 32:15takriban 1739 KK

    Ngamia wake thelathini pamoja na ndama zao, ngʼombe wake arobaini na mafahali kumi, punda wake ishirini na punda waume kumi.

  2. Mwanzo 32:16takriban 1739 KK

    Akaviweka chini ya uangalizi wa watumishi wake, kila kundi peke yake na kuwaambia, “Nitangulieni na kuacha nafasi kati ya makundi.”

  3. Mwanzo 32:17takriban 1739 KK

    Akamwagiza yule aliyetangulia kuwa, “Ndugu yangu Esau atakapokutana nawe na kukuuliza, ‘Wewe ni wa nani? Unakwenda wapi? Wanyama hawa wote mbele yako ni mali ya nani?’

  4. Mwanzo 32:18takriban 1739 KK

    Ndipo utakaposema, ‘Ni mali ya mtumishi wako Yakobo. Ni zawadi ambazo zimetumwa kwa bwana wangu Esau, naye anakuja nyuma yetu.’ ”

  5. Mwanzo 32:19takriban 1739 KK

    Akamwagiza pia yule mtumishi wa kundi la pili, la tatu na yale mengine yote yaliyofuata akiwaambia, “Mtamwambia Esau maneno hayo hayo mtakapokutana naye.

  6. Mwanzo 32:20takriban 1739 KK

    Hakikisheni mmesema, ‘Mtumishi wako Yakobo anakuja nyuma yetu.’ ” Kwa kuwa alifikiri, “Nitaweza kumtuliza kwa zawadi hizi ninazotanguliza, hatimaye, nitakapomwona, huenda atanikubali.”

  7. Mwanzo 32:21takriban 1739 KK

    Kwa hiyo zawadi za Yakobo zilitangulia mbele yake, lakini yeye mwenyewe alilala kambini usiku ule.

  8. Mwanzo 32:22takriban 1739 KK

    Usiku ule Yakobo akaamka akawachukua wake zake wawili, watumishi wake wawili wa kike na wanawe kumi na mmoja na akavuka kivuko cha Yaboki.

  9. Mwanzo 32:23takriban 1739 KK

    Baada ya kuwavusha ngʼambo ya kijito, alivusha pia mali zake zote.

  10. Mwanzo 32:24takriban 1739 KK

    Kwa hiyo Yakobo akaachwa peke yake na mtu mmoja akashikana naye mweleka mpaka mapambazuko.

  11. Mwanzo 32:25takriban 1739 KK

    Yule mtu alipoona kuwa hawezi kumshinda, aligusa kiungio cha nyonga ya Yakobo kwa hiyo nyonga yake ikateguka wakati alipokuwa akishikana mweleka na yule mtu.

  12. Mwanzo 32:26takriban 1739 KK

    Ndipo yule mtu akasema, “Niache niende, kwa kuwa ni mapambazuko.” Lakini Yakobo akajibu, “Sitakuacha uende usiponibariki.”

  13. Mwanzo 32:27takriban 1739 KK

    Yule mtu akamuuliza, “Jina lako nani?” Akajibu, “Yakobo.”

  14. Mwanzo 32:28takriban 1739 KK

    Ndipo yule mtu akasema, “Jina lako halitakuwa tena Yakobo, bali Israeli, kwa sababu umeshindana na Mungu na watu pia, nawe umeshinda.”

  15. Mwanzo 32:29takriban 1739 KK

    Yakobo akasema, “Tafadhali niambie jina lako.” Lakini akajibu, “Kwa nini kuniuliza Jina langu?” Ndipo akambariki huko.

  16. Mwanzo 32:30takriban 1739 KK

    Kwa hiyo Yakobo akapaita mahali pale Penieli, akasema, “Ni kwa sababu nimemwona Mungu uso kwa uso na bado maisha yangu yameokoka.”

  17. Mwanzo 32:31takriban 1739 KK

    Jua lilikuwa linachomoza Yakobo alipoondoka Penueli, naye alikuwa akichechemea kwa sababu ya nyonga yake.

  18. Mwanzo 32:32takriban 1739 KK

    Kwa hiyo mpaka leo Waisraeli hawali mshipa ulioungana na kiungio cha nyonga, kwa sababu kiungio cha nyonga ya Yakobo kiliteguliwa karibu na mshipa huo.

  19. Mwanzo 33:1takriban 1739 KK

    Yakobo akainua macho akamwona Esau akija na watu wake 400, kwa hiyo akawagawanya watoto kati ya Lea, Raheli na wale watumishi wake wawili wa kike.

  20. Mwanzo 33:2takriban 1739 KK

    Akawaweka wale watumishi wa kike na watoto wao mbele, Lea na watoto wake wakafuata, Raheli na Yosefu wakaja nyuma.

  21. Mwanzo 33:3takriban 1739 KK

    Yeye mwenyewe akatangulia mbele na kusujudu mara saba alipomkaribia ndugu yake.

  22. Mwanzo 33:4takriban 1739 KK

    Lakini Esau akamkimbilia Yakobo kumlaki na kumkumbatia, akamwangukia shingoni na kumbusu. Nao wakalia.

  23. Mwanzo 33:5takriban 1739 KK

    Esau akainua macho akawaona wale wanawake na watoto. Akauliza, “Hawa uliofuatana nao ni nani?” Yakobo akamjibu, “Ni watoto ambao Mungu amempa mtumishi wako kwa neema.”

  24. Mwanzo 33:6takriban 1739 KK

    Kisha wale watumishi wa kike na watoto wao wakakaribia na kusujudu.

  25. Mwanzo 33:7takriban 1739 KK

    Kisha Lea na watoto wake wakaja na kusujudu. Mwisho wa wote wakaja Yosefu na Raheli, nao pia wakasujudu.