Rukia maudhui

circa 2100–1900 BC

Abraham: The Covenant

God calls Abram from Ur, establishes an everlasting covenant, and promises a son through whom all nations will be blessed.

394 mistari · 1 kitabu kimehusishwa

Mistari ya kipindi hiki

  1. Mwanzo 13:6takriban 1918 KK

    Lakini nchi haikuwatosha kukaa pamoja kwa ajili ya wingi wa mali zao.

  2. Mwanzo 13:7takriban 1918 KK

    Ukazuka ugomvi kati ya wachunga mifugo wa Abramu na wale wa Loti. Wakati huo, Wakanaani na Waperizi ndio waliokuwa wenyeji wa nchi hiyo.

  3. Mwanzo 13:8takriban 1918 KK

    Hivyo Abramu akamwambia Loti, “Pasiwe na ugomvi wowote kati yangu na wewe, wala kati ya wachungaji wangu na wako, kwa kuwa sisi ni ndugu.

  4. Mwanzo 13:9takriban 1918 KK

    Je, nchi yote haiko mbele yako? Tutengane. Kama ukielekea kushoto, nitakwenda kulia; kama ukielekea kulia, mimi nitakwenda kushoto.”

  5. Mwanzo 13:10takriban 1918 KK

    Loti akatazama akaona lile bonde lote la Yordani kuwa lilikuwa na maji tele, kama bustani ya Bwana, kama nchi ya Misri, kuelekea Soari. (Hii ilikuwa kabla Bwana hajaharibu Sodoma na Gomora.)

  6. Mwanzo 13:11takriban 1917 KK

    Hivyo Loti akajichagulia bonde lote la Yordani, akaelekea upande wa mashariki. Watu hao wawili wakatengana:

  7. Mwanzo 13:12takriban 1917 KK

    Abramu akaishi katika nchi ya Kanaani, wakati Loti aliishi miongoni mwa miji ya lile bonde na kupiga mahema yake karibu na Sodoma.

  8. Mwanzo 13:13takriban 1917 KK

    Basi watu wa Sodoma walikuwa waovu, wakifanya sana dhambi dhidi ya Bwana.

  9. Mwanzo 13:14takriban 1917 KK

    Baada ya Loti kuondoka Bwana akamwambia Abramu, “Ukiwa hapo ulipo, inua macho yako utazame kaskazini na kusini, mashariki na magharibi.

  10. Mwanzo 13:15takriban 1917 KK

    Nchi yote unayoiona nitakupa wewe na uzao wako hata milele.

  11. Mwanzo 13:16takriban 1917 KK

    Nitaufanya uzao wako uwe mwingi kama mavumbi ya nchi, hivyo kama kuna yeyote awezaye kuhesabu mavumbi, basi uzao wako utahesabika.

  12. Mwanzo 13:17takriban 1917 KK

    Ondoka, tembea katika marefu na mapana ya nchi, kwa maana ninakupa wewe.”

  13. Mwanzo 13:18takriban 1917 KK

    Basi Abramu akaondoa mahema yake, akaenda kuishi karibu na mialoni ya Mamre huko Hebroni, huko akamjengea Bwana madhabahu.

  14. Mwanzo 14:1takriban 1913 KK

    Wakati huu Amrafeli mfalme wa Shinari, Arioko mfalme wa Elasari, Kedorlaoma mfalme wa Elamu, na Tidali mfalme wa Goimu

  15. Mwanzo 14:2takriban 1913 KK

    kwa pamoja walikwenda kupigana vita dhidi ya Bera mfalme wa Sodoma, Birsha mfalme wa Gomora, Shinabu mfalme wa Adma, Shemeberi mfalme wa Seboimu, na mfalme wa Bela (yaani Soari).

  16. Mwanzo 14:3takriban 1913 KK

    Hawa wote waliotajwa mwishoni waliunganisha majeshi yao kutoka Bonde la Sidimu (yaani Bahari ya Chumvi).

  17. Mwanzo 14:4takriban 1913 KK

    Walikuwa wametawaliwa na Mfalme Kedorlaoma kwa miaka kumi na miwili, lakini mwaka wa kumi na tatu waliasi.

  18. Mwanzo 14:5takriban 1913 KK

    Mnamo mwaka wa kumi na nne, Mfalme Kedorlaoma na wafalme waliojiunga naye walikwenda kupigana na kuwashinda Warefai katika Ashtaroth-Kanaimu, Wazuzi katika Hamu, Waemi katika Shawe-Kiriathaimu,

  19. Mwanzo 14:6takriban 1913 KK

    na Wahori katika nchi ya kilima cha Seiri, hadi El-Parani karibu na jangwa.

  20. Mwanzo 14:7takriban 1913 KK

    Kisha wakarudi wakaenda En-Misfati (yaani Kadeshi), wakashinda nchi yote ya Waamaleki, pamoja na Waamori waliokuwa wakiishi Hasason-Tamari.

  21. Mwanzo 14:8takriban 1913 KK

    Ndipo mfalme wa Sodoma, mfalme wa Gomora, mfalme wa Adma, mfalme wa Seboimu, na mfalme wa Bela (yaani Soari) wakatoka kupanga majeshi yao kwenye Bonde la Sidimu

  22. Mwanzo 14:9takriban 1913 KK

    dhidi ya Kedorlaoma, mfalme wa Elamu, Tidali mfalme wa Goimu, Amrafeli mfalme wa Shinari, na Arioko mfalme wa Elasari, yaani wafalme wanne dhidi ya wafalme watano.

  23. Mwanzo 14:10takriban 1913 KK

    Basi Bonde la Sidimu lilikuwa limejaa mashimo ya lami, nao wafalme wa Sodoma na wa Gomora walipokimbia, baadhi ya watu walitumbukia huko na wengine wakakimbilia vilimani.

  24. Mwanzo 14:11takriban 1913 KK

    Wale wafalme wanne wakateka mali yote ya Sodoma na Gomora pamoja na vyakula vyao vyote, kisha wakaenda zao.

  25. Mwanzo 14:12takriban 1913 KK

    Pia walimteka Loti mwana wa ndugu yake Abramu pamoja na mali zake, kwa kuwa alikuwa akiishi Sodoma.