Rukia maudhui

circa 2100–1900 BC

Abraham: The Covenant

God calls Abram from Ur, establishes an everlasting covenant, and promises a son through whom all nations will be blessed.

394 mistari · 1 kitabu kimehusishwa

Mistari ya kipindi hiki

  1. Mwanzo 15:14takriban 1911 KK

    Lakini nitaliadhibu taifa lile watakalolitumikia kama watumwa, na baadaye watatoka huko na mali nyingi.

  2. Mwanzo 15:15takriban 1911 KK

    Wewe, hata hivyo utakwenda kwa baba zako kwa amani na kuzikwa katika uzee mwema.

  3. Mwanzo 15:16takriban 1911 KK

    Katika kizazi cha nne wazao wako watarudi hapa, kwa maana dhambi ya Waamori bado haijafikia kipimo kilichojaa.”

  4. Mwanzo 15:17takriban 1911 KK

    Wakati jua lilipokuwa limezama na giza limeingia, tanuru la moshi na mwali wa moto unaowaka vikatokea na kupita kati ya vile vipande vya nyama.

  5. Mwanzo 15:18takriban 1911 KK

    Siku hiyo Bwana akafanya Agano na Abramu, na kumwambia, “Nitawapa wazao wako nchi hii, kuanzia Kijito cha Misri hadi mto ule mkubwa, Frati,

  6. Mwanzo 15:19takriban 1911 KK

    yaani nchi ya Wakeni, Wakenizi, Wakadmoni,

  7. Mwanzo 15:20takriban 1911 KK

    Wahiti, Waperizi, Warefai,

  8. Mwanzo 15:21takriban 1911 KK

    Waamori, Wakanaani, Wagirgashi na Wayebusi.”

  9. Mwanzo 16:1takriban 1912 KK

    Basi Sarai, mkewe Abramu, alikuwa hajamzalia watoto. Lakini alikuwa na mtumishi wa kike Mmisri jina lake Hagari,

  10. Mwanzo 16:2takriban 1912 KK

    hivyo Sarai akamwambia Abramu, “Bwana amenizuilia kupata watoto. Nenda, ukakutane kimwili na mtumishi wangu wa kike, huenda nitaweza kupata watoto kupitia kwake.” Abramu akakubaliana na lile Sarai alilosema.

  11. Mwanzo 16:3takriban 1911 KK

    Hivyo baada ya Abramu kuishi katika nchi ya Kanaani miaka kumi, Sarai akamchukua mtumishi wake wa kike wa Kimisri, Hagari na kumpa mumewe awe mke wake.

  12. Mwanzo 16:4takriban 1911 KK

    Akakutana kimwili na Hagari, naye akapata mimba. Hagari alipojua kuwa ana mimba, alianza kumdharau Sarai.

  13. Mwanzo 16:5takriban 1911 KK

    Ndipo Sarai akamwambia Abramu, “Unawajibika na manyanyaso ninayoyapata. Nilimweka mtumishi wangu mikononi mwako, sasa kwa vile anajua kwamba ana mimba, ananidharau mimi. Bwana na aamue kati yako na mimi.”

  14. Mwanzo 16:6takriban 1911 KK

    Abramu akamwambia, “Mtumishi wako yuko mikononi mwako. Mtendee lolote unalofikiri ni bora zaidi.” Ndipo Sarai akamtesa Hagari, hivyo akamtoroka.

  15. Mwanzo 16:7takriban 1911 KK

    Malaika wa Bwana akamkuta Hagari karibu na chemchemi huko jangwani; ilikuwa chemchemi ile iliyokuwa kando ya barabara iendayo Shuri.

  16. Mwanzo 16:8takriban 1911 KK

    Malaika akamwambia, “Hagari, mtumishi wa Sarai, umetokea wapi, na unakwenda wapi?” Akamjibu, “Ninamkimbia bibi yangu Sarai.”

  17. Mwanzo 16:9takriban 1911 KK

    Ndipo malaika wa Bwana akamwambia, “Rudi kwa bibi yako ukajishushe chini yake.”

  18. Mwanzo 16:10takriban 1911 KK

    Malaika akaendelea akasema, “Nitazidisha wazao wako, hivi kwamba watakuwa wengi mno wasiohesabika.”

  19. Mwanzo 16:11takriban 1911 KK

    Pia malaika wa Bwana akamwambia: “Wewe sasa una mimba nawe utamzaa mwana. Utamwita jina lake Ishmaeli, kwa sababu Bwana amesikia juu ya huzuni yako.

  20. Mwanzo 16:12takriban 1911 KK

    Atakuwa punda-mwitu katikati ya wanadamu, mkono wake utakuwa dhidi ya kila mtu na mkono wa kila mtu dhidi yake, naye ataishi kwa uhasama na ndugu zake wote.”

  21. Mwanzo 16:13takriban 1911 KK

    Hagari akampa Bwana aliyezungumza naye jina hili: “Wewe ndiwe Mungu unionaye mimi,” kwa maana alisema, “Sasa nimemwona yeye anayeniona mimi.”

  22. Mwanzo 16:14takriban 1911 KK

    Ndiyo sababu kisima kile kikaitwa Beer-Lahai-Roi, ambacho bado kipo huko hata leo kati ya Kadeshi na Beredi.

  23. Mwanzo 16:15takriban 1910 KK

    Hivyo Hagari akamzalia Abramu mwana, naye Abramu akamwita huyo mwana Hagari aliyemzalia, Ishmaeli.

  24. Mwanzo 16:16takriban 1910 KK

    Abramu alikuwa na umri wa miaka themanini na sita wakati Hagari alipomzalia Ishmaeli.

  25. Mwanzo 17:1takriban 1897 KK

    Abramu alipokuwa na miaka tisini na tisa, Bwana akamtokea akamwambia, “Mimi ndimi Mungu Mwenyezi; enenda mbele zangu na uishi kwa unyofu.