Rukia maudhui

circa 2100–1900 BC

Abraham: The Covenant

God calls Abram from Ur, establishes an everlasting covenant, and promises a son through whom all nations will be blessed.

394 mistari · 1 kitabu kimehusishwa

Mistari ya kipindi hiki

  1. Mwanzo 17:27takriban 1897 KK

    Kila mwanaume nyumbani mwa Abrahamu, pamoja na wote waliozaliwa nyumbani mwake au aliyenunuliwa kwa fedha kutoka kwa mgeni, alitahiriwa pamoja naye.

  2. Mwanzo 18:1takriban 1897 KK

    Bwana akamtokea Abrahamu karibu na mialoni ya Mamre wakati alipokuwa ameketi kwenye ingilio la hema lake wakati wa adhuhuri.

  3. Mwanzo 18:2takriban 1897 KK

    Abrahamu akainua macho akaona watu watatu wamesimama karibu naye. Alipowaona, aliharakisha kutoka kwenye ingilio la hema lake kuwalaki na kuwasujudia hadi nchi.

  4. Mwanzo 18:3takriban 1897 KK

    Akasema, “Kama nimepata kibali machoni penu, ee bwana wangu, usimpite mtumishi wako.

  5. Mwanzo 18:4takriban 1897 KK

    Acha yaletwe maji kidogo, kisha ninyi nyote mnawe miguu yenu na mpumzike chini ya mti huu.

  6. Mwanzo 18:5takriban 1897 KK

    Niruhusuni niwapatie chakula kidogo mle, ili mpate nguvu mwendelee na safari yenu, kwa kuwa mmekuja kwa mtumishi wenu.” Nao wakamjibu, “Vema sana, fanya kama unavyosema.”

  7. Mwanzo 18:6takriban 1897 KK

    Hivyo Abrahamu akaharakisha akaingia hemani kwa Sara, akamwambia, “Chukua vipimo vitatu vya unga laini haraka, ukande na uoke mikate.”

  8. Mwanzo 18:7takriban 1897 KK

    Kisha Abrahamu akakimbia kwenda kwenye kundi, akachagua ndama mzuri, laini na akampa mtumishi, ambaye aliharakisha kumtayarisha.

  9. Mwanzo 18:8takriban 1897 KK

    Kisha akaleta jibini, maziwa na nyama ya yule ndama iliyoandaliwa, akaviweka mbele ya wageni. Walipokuwa wakila, alisimama karibu nao chini ya mti.

  10. Mwanzo 18:9takriban 1897 KK

    Wakamuuliza, “Yuko wapi Sara mkeo?” Akasema, “Yuko huko, ndani ya hema.”

  11. Mwanzo 18:10takriban 1897 KK

    Kisha Bwana akasema, “Hakika nitakurudia tena majira kama haya mwakani na Sara mkeo atakuwa ana mwana.” Sara alikuwa akiwasikiliza kwenye ingilio la hema, lililokuwa nyuma yake.

  12. Mwanzo 18:11takriban 1897 KK

    Abrahamu na Sara walikuwa wazee tena waliosogea miaka, naye Sara alikuwa amekoma katika desturi ya wanawake.

  13. Mwanzo 18:12takriban 1897 KK

    Hivyo Sara akacheka kimoyomoyo alipokuwa akiwaza, “Baada ya mimi kuwa mkongwe hivi na bwana wangu amezeeka, je, nitaweza kufurahia jambo hili?”

  14. Mwanzo 18:13takriban 1897 KK

    Ndipo Bwana akamwambia Abrahamu, “Kwa nini Sara amecheka na kusema, ‘Kweli nitazaa mtoto nami sasa ni mzee?’

  15. Mwanzo 18:14takriban 1897 KK

    Je, kuna jambo lolote gumu lisilowezekana kwa Bwana? Nitakurudia mwakani majira kama haya, naye Sara atakuwa na mwana.”

  16. Mwanzo 18:15takriban 1897 KK

    Sara akaogopa kwa kuwa alidanganya na kusema, “Mimi sikucheka.” Lakini Bwana akasema, “Ndiyo, ulicheka!”

  17. Mwanzo 18:16takriban 1897 KK

    Wakati watu hao waliposimama ili waondoke, walielekeza nyuso zao Sodoma, Abrahamu akawatoa kitambo kidogo ili awasindikize.

  18. Mwanzo 18:17takriban 1897 KK

    Ndipo Bwana akasema, “Je, nimfiche Abrahamu jambo ninalokusudia kufanya?

  19. Mwanzo 18:18takriban 1897 KK

    Hakika Abrahamu atakuwa taifa kubwa na lenye nguvu, kupitia kwake mataifa yote ya dunia yatabarikiwa.

  20. Mwanzo 18:19takriban 1897 KK

    Kwa maana nimemchagua yeye, ili awaongoze watoto wake na jamaa yake kufuata njia ya Bwana, kwa kuwa waadilifu na kutenda haki, ili Bwana atimize ahadi yake kwa Abrahamu.”

  21. Mwanzo 18:20takriban 1897 KK

    Basi Bwana akasema, “Kilio dhidi ya Sodoma na Gomora ni kikubwa sana na dhambi yao inasikitisha sana,

  22. Mwanzo 18:21takriban 1897 KK

    kwamba nitashuka nione kama waliyoyatenda ni mabaya kiasi cha kilio kilichonifikia. Kama sivyo, nitajua.”

  23. Mwanzo 18:22takriban 1897 KK

    Basi wale watu wakageuka wakaenda kuelekea Sodoma, lakini Abrahamu akabaki amesimama mbele za Bwana.

  24. Mwanzo 18:23takriban 1897 KK

    Ndipo Abrahamu akamsogelea akasema: “Je, utawaangamiza wenye haki na waovu?

  25. Mwanzo 18:24takriban 1897 KK

    Je, ikiwa watakuwepo watu wenye haki hamsini katika mji huo, hivi kweli utauangamiza na wala hutauacha kwa ajili ya hao watu hamsini wenye haki waliomo ndani yake?