Rukia maudhui

circa 2100–1900 BC

Abraham: The Covenant

God calls Abram from Ur, establishes an everlasting covenant, and promises a son through whom all nations will be blessed.

394 mistari · 1 kitabu kimehusishwa

Mistari ya kipindi hiki

  1. Mwanzo 22:2takriban 1872 KK

    Kisha Mungu akamwambia, “Umchukue mwanao, mwana wako wa pekee, Isaki umpendaye, uende katika nchi ya Moria. Mtoe huko kama sadaka ya kuteketezwa juu ya mlima mmojawapo nitakaokuambia.”

  2. Mwanzo 22:3takriban 1872 KK

    Abrahamu akaamka asubuhi na mapema siku iliyofuata, akamtayarisha punda wake. Akawachukua watumishi wake wawili pamoja na Isaki mwanawe. Baada ya kuchanja kuni za kutosha kwa ajili ya hiyo sadaka ya kuteketezwa, akaondoka kuelekea mahali Mungu alipokuwa amemwambia.

  3. Mwanzo 22:4takriban 1872 KK

    Siku ya tatu Abrahamu akainua macho, akapaona mahali pale kwa mbali.

  4. Mwanzo 22:5takriban 1872 KK

    Akawaambia watumishi wake, “Kaeni hapa pamoja na punda, wakati mimi na kijana tunakwenda kule. Tutakwenda kuabudu na kisha tutawarudia.”

  5. Mwanzo 22:6takriban 1872 KK

    Abrahamu akachukua kuni kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa, akamtwika Isaki mwanawe, yeye mwenyewe akachukua moto na kisu. Walipokuwa wakienda pamoja,

  6. Mwanzo 22:7takriban 1872 KK

    Isaki akanena akamwambia Abrahamu baba yake, “Baba yangu!” Abrahamu akaitika, “Mimi hapa, mwanangu.” Isaki akasema, “Moto na kuni zipo, Je, yuko wapi mwana-kondoo kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa?”

  7. Mwanzo 22:8takriban 1872 KK

    Abrahamu akajibu, “Mwanangu, Mungu mwenyewe atajipatia mwana-kondoo kwa ajili ya hiyo sadaka ya kuteketezwa.” Nao hawa wawili wakaendelea mbele pamoja.

  8. Mwanzo 22:9takriban 1872 KK

    Walipofika mahali pale alipokuwa ameambiwa na Mungu, Abrahamu akajenga madhabahu hapo, akaziweka kuni juu yake. Akamfunga Isaki mwanawe na akamlaza kwenye madhabahu, juu ya zile kuni.

  9. Mwanzo 22:10takriban 1872 KK

    Kisha akanyoosha mkono wake na akachukua kisu ili amchinje mwanawe.

  10. Mwanzo 22:11takriban 1872 KK

    Lakini malaika wa Bwana akamwita kutoka mbinguni, akamwambia, “Abrahamu! Abrahamu!” Akajibu, “Mimi hapa.”

  11. Mwanzo 22:12takriban 1872 KK

    Akamwambia, “Usimdhuru kijana, wala usimtendee jambo lolote. Sasa ninajua kwamba unamcha Mungu, kwa sababu hukunizuilia mwanao, mwana wako wa pekee.”

  12. Mwanzo 22:13takriban 1872 KK

    Abrahamu akainua macho yake, akaona kondoo dume amenaswa pembe zake nyuma yake katika kichaka. Akaenda akamchukua huyo kondoo dume, akamtoa awe sadaka ya kuteketezwa badala ya mwanawe.

  13. Mwanzo 22:14takriban 1872 KK

    Abrahamu akapaita mahali pale Yehova-Yire. Mpaka siku ya leo inasemekana, “Katika mlima wa Bwana itapatikana.”

  14. Mwanzo 22:15takriban 1872 KK

    Basi malaika wa Bwana akamwita Abrahamu kutoka mbinguni mara ya pili,

  15. Mwanzo 22:16takriban 1872 KK

    akasema, “Ninaapa kwa nafsi yangu, asema Bwana, kwamba kwa sababu umefanya jambo hili na hukunizuilia mwanao, mwana wako wa pekee,

  16. Mwanzo 22:17takriban 1872 KK

    hakika nitakubariki, na nitauzidisha uzao wako kama nyota za angani na kama mchanga ulioko pwani. Wazao wako watamiliki miji ya adui zao,

  17. Mwanzo 22:18takriban 1872 KK

    na kupitia uzao wako mataifa yote duniani yatabarikiwa, kwa sababu umenitii.”

  18. Mwanzo 22:19takriban 1872 KK

    Ndipo Abrahamu akawarudia watumishi wake, wakaondoka wakaenda wote pamoja mpaka Beer-Sheba. Abrahamu akaishi huko Beer-Sheba.

  19. Mwanzo 22:20takriban 1862 KK

    Baada ya muda, Abrahamu akaambiwa, “Milka pia amepata watoto, amemzalia ndugu yako Nahori wana:

  20. Mwanzo 22:21takriban 1862 KK

    Usi mzaliwa wake wa kwanza, Buzi nduguye, Kemueli (baba wa Aramu),

  21. Mwanzo 22:22takriban 1862 KK

    Kesedi, Hazo, Pildashi, Yidlafu na Bethueli.”

  22. Mwanzo 22:23takriban 1862 KK

    Bethueli akamzaa Rebeka. Milka alimzalia Nahori nduguye Abrahamu hao wana wanane.

  23. Mwanzo 22:24takriban 1862 KK

    Suria wake Nahori aliyeitwa Reuma pia alikuwa na wana: Teba, Gahamu, Tahashi na Maaka.

  24. Mwanzo 23:1takriban 1860 KK

    Sara aliishi akawa na umri wa miaka mia na ishirini na saba.

  25. Mwanzo 23:2takriban 1860 KK

    Sara akafa huko Kiriath-Arba (yaani Hebroni) katika nchi ya Kanaani, Abrahamu akamwombolezea na kumlilia Sara.