Rukia maudhui

circa 2100–1900 BC

Abraham: The Covenant

God calls Abram from Ur, establishes an everlasting covenant, and promises a son through whom all nations will be blessed.

394 mistari · 1 kitabu kimehusishwa

Mistari ya kipindi hiki

  1. Mwanzo 21:11takriban 1893 KK

    Jambo hili lilimhuzunisha sana Abrahamu kwa sababu lilimhusu mwanawe.

  2. Mwanzo 21:12takriban 1893 KK

    Lakini Mungu akamwambia, “Usihuzunike hivyo kwa sababu ya kijana na mtumishi wako wa kike. Sikiliza lolote Sara analokuambia, kwa sababu uzao wako utahesabiwa kupitia kwake Isaki.

  3. Mwanzo 21:13takriban 1893 KK

    Nitamfanya huyu mwana wa mtumishi wako wa kike kuwa taifa pia, kwa sababu naye ni uzao wako.”

  4. Mwanzo 21:14takriban 1892 KK

    Kesho yake asubuhi na mapema, Abrahamu akachukua chakula na kiriba cha maji, akampa Hagari. Akaviweka mabegani mwa Hagari, akamwondoa pamoja na kijana. Hagari akashika njia, akatangatanga katika jangwa la Beer-Sheba.

  5. Mwanzo 21:15takriban 1892 KK

    Maji yalipokwisha kwenye kiriba, akamwacha kijana chini ya mojawapo ya vichaka.

  6. Mwanzo 21:16takriban 1892 KK

    Kisha akajiendea zake akaketi karibu, umbali wa kutupa mshale, akawaza, “Siwezi kumwangalia kijana akifa.” Ikawa alipokuwa ameketi pale karibu, akaanza kulia kwa huzuni.

  7. Mwanzo 21:17takriban 1892 KK

    Mungu akamsikia kijana akilia, malaika wa Mungu akamwita Hagari kutoka mbinguni na kumwambia, “Kuna nini Hagari? Usiogope, Mungu amesikia kijana analia akiwa amelala pale.

  8. Mwanzo 21:18takriban 1892 KK

    Mwinue kijana na umshike mkono, kwa maana nitamfanya kuwa taifa kubwa.”

  9. Mwanzo 21:19takriban 1892 KK

    Ndipo Mungu akamfumbua Hagari macho yake naye akaona kisima cha maji. Hivyo akaenda akajaza kiriba maji na kumpa kijana anywe.

  10. Mwanzo 21:20takriban 1892 KK

    Mungu akawa pamoja na huyu kijana alipokuwa akiendelea kukua. Aliishi jangwani na akawa mpiga upinde.

  11. Mwanzo 21:21takriban 1892 KK

    Alipokuwa akiishi katika Jangwa la Parani, mama yake akampatia mke kutoka Misri.

  12. Mwanzo 21:22takriban 1886 KK

    Wakati huo Abimeleki na Fikoli mkuu wa majeshi yake wakamwambia Abrahamu, “Mungu yu pamoja nawe katika kila kitu unachofanya.

  13. Mwanzo 21:23takriban 1886 KK

    Sasa niapie hapa mbele za Mungu kwamba hutanitenda hila mimi, watoto wangu wala wazao wangu. Nitendee mimi na nchi ambayo unaishi kama mgeni wema ule ule ambao nimekutendea.”

  14. Mwanzo 21:24takriban 1886 KK

    Abrahamu akasema, “Ninaapa hivyo.”

  15. Mwanzo 21:25takriban 1886 KK

    Ndipo Abrahamu akalalamika kwa Abimeleki kuhusu kisima cha maji ambacho watumishi wa Abimeleki walikuwa wamekinyangʼanya.

  16. Mwanzo 21:26takriban 1886 KK

    Lakini Abimeleki akasema, “Sijui ni nani ambaye amefanya hili. Hukuniambia, leo tu ndipo ninasikia habari zake.”

  17. Mwanzo 21:27takriban 1886 KK

    Hivyo Abrahamu akaleta kondoo na ngʼombe, akampa Abimeleki, nao watu hawa wawili wakafanya mapatano.

  18. Mwanzo 21:28takriban 1886 KK

    Abrahamu akatenga kondoo wa kike saba kutoka kwenye kundi,

  19. Mwanzo 21:29takriban 1886 KK

    Abimeleki akamuuliza Abrahamu, “Ni nini maana ya hawa kondoo wa kike saba uliowatenga peke yao?”

  20. Mwanzo 21:30takriban 1886 KK

    Abrahamu akamjibu, “Upokee hawa kondoo wa kike saba kutoka mkononi mwangu kama ushahidi kuwa nilichimba kisima hiki.”

  21. Mwanzo 21:31takriban 1886 KK

    Hivyo mahali pale pakaitwa Beer-Sheba, kwa sababu watu wawili waliapiana hapo.

  22. Mwanzo 21:32takriban 1886 KK

    Baada ya mapatano kufanyika huko Beer-Sheba, Abimeleki na Fikoli mkuu wa majeshi yake wakarudi katika nchi ya Wafilisti.

  23. Mwanzo 21:33takriban 1886 KK

    Abrahamu akapanda mti wa mkwaju huko Beer-Sheba, na hapo akaliitia jina la Bwana, Mungu wa milele.

  24. Mwanzo 21:34takriban 1886 KK

    Naye Abrahamu akakaa katika nchi ya Wafilisti kwa muda mrefu.

  25. Mwanzo 22:1takriban 1872 KK

    Baadaye Mungu akamjaribu Abrahamu. Akamwambia, “Abrahamu!” Abrahamu akajibu, “Mimi hapa.”