Rukia maudhui

circa 2100–1900 BC

Abraham: The Covenant

God calls Abram from Ur, establishes an everlasting covenant, and promises a son through whom all nations will be blessed.

394 mistari · 1 kitabu kimehusishwa

Mistari ya kipindi hiki

  1. Mwanzo 23:3takriban 1860 KK

    Ndipo Abrahamu akainuka kutoka pale penye maiti ya mke wake. Akazungumza na Wahiti, akasema,

  2. Mwanzo 23:4takriban 1860 KK

    “Mimi ni mpitaji na mgeni miongoni mwenu. Niuzieni sehemu ya ardhi yenu ili niweze kumzika maiti wangu.”

  3. Mwanzo 23:5takriban 1860 KK

    Wahiti wakamjibu Abrahamu,

  4. Mwanzo 23:6takriban 1860 KK

    “Bwana, tusikilize. Wewe ni mtawala mkuu sana miongoni mwetu. Zika maiti wako katika kaburi unalolipenda kati ya makaburi yetu. Hakuna mtu wa kwetu atakayekuzuia kaburi lake ili kuzika maiti wako.”

  5. Mwanzo 23:7takriban 1860 KK

    Abrahamu akainuka na akasujudu mbele ya wenyeji wa nchi, yaani Wahiti.

  6. Mwanzo 23:8takriban 1860 KK

    Akawaambia, “Kama mnaniruhusu kumzika maiti wangu, basi nisikilizeni mkamsihi Efroni mwana wa Sohari kwa niaba yangu

  7. Mwanzo 23:9takriban 1860 KK

    ili aniuzie pango la Makpela, lililo mali yake, nalo liko mwisho wa shamba lake. Mwambieni aniuzie kwa bei kamili atakayosema ili liwe mahali pangu pa kuzikia miongoni mwenu.”

  8. Mwanzo 23:10takriban 1860 KK

    Efroni Mhiti alikuwa ameketi miongoni mwa watu wake, akamjibu Abrahamu mbele ya Wahiti wote waliokuwepo katika lango la mji.

  9. Mwanzo 23:11takriban 1860 KK

    “La hasha, bwana wangu, nisikilize, nakupa shamba, pia nakupa pango lililomo ndani yake. Nakupa mbele ya watu wangu. Uzike maiti wako.”

  10. Mwanzo 23:12takriban 1860 KK

    Abrahamu akasujudu tena, mbele ya wenyeji wa nchi,

  11. Mwanzo 23:13takriban 1860 KK

    akamwambia Efroni wale watu wakiwa wanasikia, “Tafadhali nisikilize. Nitakulipa fedha za hilo shamba. Kubali kuzipokea ili niweze kumzika maiti wangu.”

  12. Mwanzo 23:14takriban 1860 KK

    Efroni akamjibu Abrahamu,

  13. Mwanzo 23:15takriban 1860 KK

    “Nisikilize, bwana wangu, thamani ya ardhi hiyo ni shekeli 400 za fedha, lakini hiyo ni nini kati yako na mimi? Mzike maiti wako.”

  14. Mwanzo 23:16takriban 1860 KK

    Abrahamu akakubali masharti ya Efroni, akampimia ile fedha aliyotaja masikioni mwa Wahiti: Shekeli 400 za fedha kulingana na viwango vya uzito vilivyokuwa vikitumika wakati huo na wafanyabiashara.

  15. Mwanzo 23:17takriban 1860 KK

    Hivyo shamba la Efroni huko Makpela karibu na Mamre, yaani shamba pamoja na pango lililokuwamo, nayo miti yote iliyokuwamo ndani ya mipaka ya shamba hilo, vilikabidhiwa,

  16. Mwanzo 23:18takriban 1860 KK

    kwa Abrahamu kuwa mali yake mbele ya Wahiti wote waliokuwa wamekuja kwenye lango la mji.

  17. Mwanzo 23:19takriban 1860 KK

    Baada ya hayo Abrahamu akamzika Sara mkewe kwenye pango ndani ya shamba la Makpela karibu na Mamre (huko Hebroni) katika nchi ya Kanaani.

  18. Mwanzo 23:20takriban 1860 KK

    Hivyo Wahiti wakamkabidhi Abrahamu shamba pamoja na pango lililokuwa humo kuwa mahali pa kuzikia.

  19. Mwanzo 24:1takriban 1857 KK

    Wakati huu Abrahamu alikuwa mzee mwenye miaka mingi, naye Bwana alikuwa amembariki katika kila njia.

  20. Mwanzo 24:2takriban 1857 KK

    Akamwambia mtumishi wake mkuu wa vitu vyote katika nyumba yake, yule aliyekuwa msimamizi wa vitu vyote alivyokuwa navyo, “Weka mkono wako chini ya paja langu,

  21. Mwanzo 24:3takriban 1857 KK

    Ninataka uape kwa Bwana, Mungu wa mbingu na Mungu wa nchi, kwamba hutamtwalia mwanangu mke kutoka binti za Wakanaani, ambao ninaishi miongoni mwao,

  22. Mwanzo 24:4takriban 1857 KK

    bali utakwenda katika nchi yangu na jamaa zangu umpatie Isaki mwanangu mke.”

  23. Mwanzo 24:5takriban 1857 KK

    Yule mtumishi akamuuliza, “Je, kama huyo mwanamke atakataa kuja nami katika nchi hii? Je, nimpeleke mwanao katika hiyo nchi uliyotoka?”

  24. Mwanzo 24:6takriban 1857 KK

    Abrahamu akasema, “Hakikisha kwamba hutamrudisha mwanangu huko.

  25. Mwanzo 24:7takriban 1857 KK

    Bwana, Mungu wa mbingu, aliyenitoa nyumbani kwa baba yangu na nchi yangu niliyozaliwa na aliyesema nami na akaniahidi kwa kiapo, akisema, ‘Nitawapa watoto wako nchi hii,’ atatuma malaika wake akutangulie ili umpatie mwanangu mke kutoka huko.