Rukia maudhui

Mistari ya Biblia kuhusu Prayer

720 mistari · 120 vipengele

Mistari muhimu ya Biblia

Chuja kwa kitabu
  1. Watu na wafahamu kuwa ni mkono wako, kwamba wewe, Ee Bwana, umetenda hili.

  2. Wanaweza kulaani, lakini wewe utabariki, watakaposhambulia wataaibishwa, lakini mtumishi wako atashangilia.

  3. Washtaki wangu watavikwa fedheha, na kufunikwa na aibu kama joho.

  4. Watoto wake watakuwa wenye uwezo katika nchi, kizazi cha watu waadilifu kitabarikiwa.

  5. Sio kwetu sisi, Ee Bwana, sio kwetu sisi, bali utukufu ni kwa jina lako, kwa sababu ya upendo na uaminifu wako.

  6. Kwa nini mataifa waseme, “Yuko wapi Mungu wao?”

  7. Ninampenda Bwana kwa maana amesikia sauti yangu; amesikia kilio changu ili anihurumie.

  8. Kwa sababu amenitegea sikio lake, nitamwita siku zote za maisha yangu.

  9. Ndipo nikaliitia jina la Bwana: “Ee Bwana, niokoe!”

  10. Wakati wa maumivu yangu makuu nilimlilia Bwana, naye akanijibu kwa kuniweka huru.

  11. Nitakushukuru, kwa kuwa ulinijibu, umekuwa wokovu wangu.

  12. Nilikueleza njia zangu ukanijibu, nifundishe sheria zako.

  13. Mtimizie mtumishi wako ahadi yako, ili upate kuogopwa.

  14. ndipo nitakapomjibu anayenidhihaki, kwa kuwa ninalitumainia neno lako.

  15. Usilinyakue neno la kweli kutoka kinywani mwangu, kwa kuwa nimeweka tumaini langu katika amri zako.

  16. Kumbuka neno lako kwa mtumishi wako, kwa sababu umenipa tumaini.

  17. Nimetafuta uso wako kwa moyo wangu wote, nihurumie sawasawa na ahadi yako.

  18. Mikono yako ilinifanya na kuniumba, nipe ufahamu niweze kujifunza amri zako.

  19. Wenye majivuno na waaibishwe kwa kunikosea mimi bila sababu, lakini mimi nitatafakari juu ya mausia yako.

  20. Mtumishi wako itampasa angoje mpaka lini? Ni lini utawaadhibu washtaki wangu?

  21. Uniokoe, kwa maana mimi ni wako, kwa kuwa nimetafuta mausia yako.

  22. Nihifadhi sawasawa na ahadi yako, nami nitaishi; usiache matumaini yangu yakavunjwa.

  23. Mfanyie mtumishi wako kulingana na upendo wako na unifundishe maagizo yako.

  24. Ee Bwana, ninakuita kwa moyo wangu wote, nami nitayatii maagizo yako.

  25. Ninakuita; niokoe nami nitazishika sheria zako.