Skip to content

Mistari ya Biblia kuhusu Prayer: Answered

58 mistari · 120 vipengele

Mistari kuhusu Answered

Chuja kwa kitabu
  1. Wamesababisha kilio cha maskini kifike mbele zake, hivyo akasikia kilio cha wahitaji.

  2. Ninamlilia Bwana kwa sauti kuu, naye ananijibu kutoka mlima wake mtakatifu.

  3. Kwa mwimbishaji. Kwa ala za nyuzi za muziki. Zaburi ya Daudi. Nijibu nikuitapo, Ee Mungu wangu mwenye haki! Nipumzishe katika shida zangu; nirehemu, usikie ombi langu.

  4. Kaeni mbali nami, ninyi nyote mtendao mabaya, kwa maana Bwana amesikia kulia kwangu.

  5. Bwana amesikia kilio changu kwa huruma, Bwana amekubali sala yangu.

  6. Katika shida yangu nalimwita Bwana, nilimlilia Mungu wangu anisaidie. Kutoka hekaluni mwake alisikia sauti yangu, kilio changu kikafika mbele zake, masikioni mwake.

  7. Umempa haja ya moyo wake na hukumzuilia maombi ya midomo yake.

  8. Alikuomba maisha, nawe ukampa, wingi wa siku milele na milele.

  9. Kwako wewe baba zetu waliweka tumaini lao, walikutumaini nawe ukawaokoa.

  10. Walikulilia wewe na ukawaokoa, walikutegemea wewe nao hawakuaibika.

  11. Kwa maana hakupuuza wala kudharau mateso ya aliyeonewa; hakumficha uso wake bali alisikiliza kilio chake ili amsaidie.

  12. Bwana asifiwe, kwa maana amesikia kilio changu nikimwomba anihurumie.

  13. Ee Bwana, Mungu wangu, nilikuita unisaidie na wewe umeniponya.

  14. Ee Bwana, umenitoa Kuzimu, umeniokoa nisishuke kwenye shimo la mauti.

  15. Katika hofu yangu nilisema, “Nimekatiliwa mbali na macho yako!” Hata hivyo ulisikia kilio changu ukanihurumia nilipokuita unisaidie.

  16. Nilimtafuta Bwana naye akanijibu, akaniokoa kwenye hofu zangu zote.

  17. Wale wamtazamao hutiwa nuru, nyuso zao hazifunikwi na aibu kamwe.

  18. Maskini huyu alimwita Bwana, naye akamsikia, akamwokoa katika taabu zake zote.

  19. Kwa mwimbishaji. Zaburi ya Daudi. Nilimngoja Bwana kwa saburi, naye akaniinamia, akasikia kilio changu.

  20. lakini hakika Mungu amenisikiliza na amesikia sauti yangu katika maombi.

  21. Sifa apewe Mungu, ambaye hakulikataa ombi langu wala kunizuilia upendo wake!

  22. Kwa mwimbishaji. Mtindo wa Yeduthuni. Zaburi ya Asafu. Nilimlilia Mungu ili anisaidie, nilimlilia Mungu ili anisikie.

  23. Nilipokuwa katika taabu, nilimtafuta Bwana, usiku nilinyoosha mikono bila kuchoka na nafsi yangu ilikataa kufarijika.

  24. Katika shida yako uliniita nami nikakuokoa, nilikujibu katika mawingu yenye ngurumo; nilikujaribu katika maji ya Meriba.

  25. Mose na Aroni walikuwa miongoni mwa makuhani wake, Samweli alikuwa miongoni mwa walioliitia jina lake; walimwita Bwana, naye aliwajibu.