Rukia maudhui

Mistari ya Biblia kuhusu Prayer

720 mistari · 120 vipengele

Mistari muhimu ya Biblia

Chuja kwa kitabu
  1. Bwana kumbuka jinsi mtumishi wako amesimangwa, jinsi ninavyovumilia moyoni mwangu dhihaka za mataifa yote,

  2. dhihaka ambazo kwazo adui zako wamenisimanga, Ee Bwana, ambazo kwazo wamesimanga kila hatua ya mpakwa mafuta wako.

  3. Ataniita, nami nitamjibu; nitakuwa pamoja naye katika taabu, nitamwokoa na kumheshimu.

  4. Ee Mhukumu wa dunia, inuka, uwalipize wenye kiburi kama wanavyostahili.

  5. Njooni, tusujudu, tumwabudu, tupige magoti mbele za Bwana Muumba wetu,

  6. Mose na Aroni walikuwa miongoni mwa makuhani wake, Samweli alikuwa miongoni mwa walioliitia jina lake; walimwita Bwana, naye aliwajibu.

  7. Alizungumza nao kutoka nguzo ya wingu; walizishika sheria zake na amri alizowapa.

  8. Ee Bwana, wetu, ndiwe uliyewajibu, kwa Israeli ulikuwa Mungu mwenye kusamehe, ingawa uliadhibu matendo yao mabaya.

  9. Maombi ya mtu aliyechoka. Anapoteseka na kumimina malalamiko yake kwa Bwana. Ee Bwana, usikie maombi yangu, kilio changu cha kuomba msaada kikufikie.

  10. Usinifiche uso wako ninapokuwa katika shida. Unitegee sikio lako, ninapoita, unijibu kwa upesi.

  11. Ataitikia maombi ya mtu mkiwa, wala hatadharau hoja yao.

  12. Hili na liandikwe kwa ajili ya kizazi kijacho, ili taifa litakaloumbwa baadaye waweze kumsifu Bwana:

  13. “Bwana alitazama chini kutoka patakatifu pake palipo juu, kutoka mbinguni alitazama dunia,

  14. kusikiliza vilio vya uchungu vya wafungwa na kuwaweka huru wale waliohukumiwa kufa.”

  15. Lishangilieni jina lake takatifu, mioyo ya wale wamtafutao Bwana na ifurahi.

  16. Mtafuteni Bwana na nguvu zake, utafuteni uso wake siku zote.

  17. Tumetenda dhambi, kama vile baba zetu walivyotenda, tumekosa na tumetenda uovu.

  18. Wakati baba zetu walipokuwa Misri, hawakuzingatia maajabu yako, wala hawakukumbuka wingi wa fadhili zako, bali waliasi kando ya bahari, Bahari ya Shamu.

  19. Lakini akaangalia mateso yao wakati aliposikia kilio chao;

  20. Ee Bwana Mungu wetu, tuokoe. Tukusanye tena kutoka kwa mataifa, ili tuweze kulishukuru jina lako takatifu, na kushangilia katika sifa zako.

  21. Ndipo walipomlilia Bwana katika shida yao, naye akawaokoa kutoka taabu yao.

  22. Akawaongoza kwa njia iliyo sawa hadi mji ambao wangeweza kuishi.

  23. Ndipo walipomlilia Bwana katika shida yao, naye akawaokoa kutoka taabu yao.

  24. Akawatoa katika giza na huzuni kuu na akavunja minyororo yao.

  25. Basi na wamshukuru Bwana kwa upendo wake usiokoma, na kwa matendo yake ya ajabu kwa wanadamu,