Rukia maudhui

circa 1010–970 BC

The Reign of David

David unites the tribes, conquers Jerusalem, and establishes Israel's golden age—even through deep personal failure.

1,230 mistari · 2 vitabu vimehusishwa

Mistari ya kipindi hiki

Chuja kwa kitabu
  1. 1 Nyakati 15:24takriban 1042 KK

    Shebania, Yoshafati, Nethaneli, Amasai, Zekaria, Benaya na Eliezeri, makuhani, walikuwa wapiga tarumbeta mbele ya Sanduku la Mungu. Obed-Edomu na Yehiya waliwekwa pia kuwa mabawabu wa Sanduku.

  2. 1 Nyakati 15:25takriban 1042 KK

    Basi Daudi pamoja na wazee wa Israeli na majemadari wa vikosi vya elfu wakaenda ili kulipandisha Sanduku la Agano la Bwana kutoka nyumba ya Obed-Edomu kwa shangwe.

  3. 1 Nyakati 15:26takriban 1042 KK

    Kwa sababu Mungu alikuwa amewasaidia Walawi waliokuwa wanalichukua Sanduku la Agano la Bwana, mafahali saba na kondoo dume saba walitolewa dhabihu.

  4. 1 Nyakati 15:27takriban 1042 KK

    Basi Daudi alikuwa amevaa joho la kitani safi, kama walivyokuwa wamevaa Walawi wote waliokuwa wanalichukua lile Sanduku, waimbaji nao walivaa vivyo hivyo, pamoja na Kenania aliyekuwa anaongoza nyimbo za waimbaji. Daudi alivaa pia kisibau cha kitani safi.

  5. 1 Nyakati 15:28takriban 1042 KK

    Hivyo Israeli wote wakalipandisha Sanduku la Agano la Bwana kwa shangwe, wakipiga pembe za kondoo dume, tarumbeta, matoazi, wakipiga zeze na vinubi.

  6. 1 Nyakati 15:29takriban 1042 KK

    Sanduku la Agano la Bwana lilipokuwa linaingia katika Mji wa Daudi, Mikali binti Sauli akachungulia dirishani. Naye alipomwona Mfalme Daudi akicheza na kusherehekea, akamdharau moyoni mwake.

  7. 1 Nyakati 16:1takriban 1042 KK

    Wakaleta Sanduku la Mungu na kuliweka ndani ya hema ambalo Daudi alikuwa amelisimamisha kwa ajili yake, na wakatoa sadaka za kuteketezwa na sadaka za amani mbele za Mungu.

  8. 1 Nyakati 16:2takriban 1042 KK

    Baada ya Daudi kumaliza kutoa hizo sadaka za kuteketezwa na hizo sadaka za amani, akawabariki watu katika jina la Bwana.

  9. 1 Nyakati 16:3takriban 1042 KK

    Kisha akamgawia kila Mwisraeli mwanaume na mwanamke mkate, andazi la tende na andazi la zabibu kavu.

  10. 1 Nyakati 16:4takriban 1042 KK

    Akawaweka pia baadhi ya Walawi ili wahudumu mbele ya Sanduku la Bwana kufanya maombi, kumshukuru na kumsifu Bwana, Mungu wa Israeli:

  11. 1 Nyakati 16:5takriban 1042 KK

    Asafu ndiye alikuwa mkuu wao, akisaidiwa na Zekaria, Yeieli, Shemiramothi, Yehieli, Matithia, Eliabu, Benaya, Obed-Edomu na Yeieli. Hawa ndio wangepiga zeze na vinubi, Asafu angepiga matoazi,

  12. 1 Nyakati 16:6takriban 1042 KK

    nao Benaya na Yahazieli makuhani, ndio wangepiga tarumbeta mara kwa mara mbele ya Sanduku la Agano la Mungu.

  13. 1 Nyakati 16:7takriban 1042 KK

    Siku ile, kitu cha kwanza Daudi alichofanya ni kumkabidhi Asafu na wenzake zaburi hii ya shukrani kwa Bwana:

  14. 1 Nyakati 16:8takriban 1042 KK

    Mshukuruni Bwana, liitieni jina lake; wajulisheni mataifa yale aliyoyatenda.

  15. 1 Nyakati 16:9takriban 1042 KK

    Mwimbieni yeye, mwimbieni yeye sifa; waambieni matendo yake yote ya ajabu.

  16. 1 Nyakati 16:10takriban 1042 KK

    Lishangilieni jina lake takatifu; mioyo ya wale wamtafutao Bwana na ifurahi.

  17. 1 Nyakati 16:11takriban 1042 KK

    Mtafuteni Bwana na nguvu zake; utafuteni uso wake siku zote.

  18. 1 Nyakati 16:12takriban 1042 KK

    Kumbuka matendo ya ajabu aliyoyafanya, miujiza yake na hukumu alizozitamka,

  19. 1 Nyakati 16:13takriban 1042 KK

    enyi wazao wa Israeli mtumishi wake, enyi wana wa Yakobo, wateule wake.

  20. 1 Nyakati 16:14takriban 1042 KK

    Yeye ndiye Bwana Mungu wetu; hukumu zake zimo duniani pote.

  21. 1 Nyakati 16:15takriban 1042 KK

    Hulikumbuka agano lake milele, neno ambalo aliamuru, kwa vizazi elfu,

  22. 1 Nyakati 16:16takriban 1042 KK

    agano alilolifanya na Abrahamu, kiapo alichomwapia Isaki.

  23. 1 Nyakati 16:17takriban 1042 KK

    Alilithibitisha kwa Yakobo kuwa amri, kwa Israeli liwe agano la milele:

  24. 1 Nyakati 16:18takriban 1042 KK

    “Nitakupa wewe nchi ya Kanaani kuwa sehemu utakayoirithi.”

  25. 1 Nyakati 16:19takriban 1042 KK

    Walipokuwa wachache kwa idadi, wachache sana na wageni ndani yake,