Rukia maudhui

circa 1010–970 BC

The Reign of David

David unites the tribes, conquers Jerusalem, and establishes Israel's golden age—even through deep personal failure.

1,230 mistari · 2 vitabu vimehusishwa

Mistari ya kipindi hiki

Chuja kwa kitabu
  1. 1 Nyakati 14:16takriban 1047 KK

    Kwa hiyo Daudi akafanya kama alivyoagizwa na Mungu, wakalipiga jeshi la Wafilisti kuanzia Gibeoni hadi Gezeri.

  2. 1 Nyakati 14:17takriban 1047 KK

    Hivyo umaarufu wa Daudi ukaenea katika kila nchi, naye Bwana akayafanya mataifa yote kumwogopa Daudi.

  3. 1 Nyakati 15:1takriban 1042 KK

    Baada ya Daudi kujijengea nyumba zake katika Mji wa Daudi, akatengeneza sehemu kwa ajili ya Sanduku la Mungu, kisha akasimamisha hema kwa ajili yake.

  4. 1 Nyakati 15:2takriban 1042 KK

    Kisha Daudi akasema, “Hakuna mtu yeyote anayeruhusiwa kulibeba Sanduku la Mungu isipokuwa Walawi peke yao, kwa sababu Bwana aliwachagua kulibeba Sanduku la Bwana na kuhudumu mbele zake milele.”

  5. 1 Nyakati 15:3takriban 1042 KK

    Daudi akawakusanya Israeli wote huko Yerusalemu ili kulipandisha Sanduku la Bwana na kulileta hadi kwenye sehemu aliyokuwa ametengeneza kwa ajili yake.

  6. 1 Nyakati 15:4takriban 1042 KK

    Kisha Daudi akawakusanya pamoja wazao wa Aroni na Walawi:

  7. 1 Nyakati 15:5takriban 1042 KK

    Kutoka wazao wa Kohathi, Urieli kiongozi na ndugu zake 120,

  8. 1 Nyakati 15:6takriban 1042 KK

    Kutoka wazao wa Merari, Asaya kiongozi na ndugu zake 220.

  9. 1 Nyakati 15:7takriban 1042 KK

    Kutoka wazao wa Gershoni, Yoeli kiongozi na ndugu zake 130.

  10. 1 Nyakati 15:8takriban 1042 KK

    Kutoka wazao wa Elisafani, Shemaya kiongozi na ndugu zake 200.

  11. 1 Nyakati 15:9takriban 1042 KK

    Kutoka wazao wa Hebroni, Elieli kiongozi na ndugu zake 80.

  12. 1 Nyakati 15:10takriban 1042 KK

    Kutoka wazao wa Uzieli, Aminadabu kiongozi na ndugu zake 112.

  13. 1 Nyakati 15:11takriban 1042 KK

    Kisha Daudi akawaita makuhani Sadoki na Abiathari, pamoja na Walawi Urieli, Asaya, Yoeli, Shemaya, Elieli na Aminadabu.

  14. 1 Nyakati 15:12takriban 1042 KK

    Akawaambia, “Ninyi ndio viongozi wa jamaa za Walawi. Ninyi pamoja na Walawi wenzenu inawapasa mjitakase na kulipandisha Sanduku la Bwana, Mungu wa Israeli hadi mahali ambapo nimetengeneza kwa ajili yake.

  15. 1 Nyakati 15:13takriban 1042 KK

    Ilikuwa ni kwa sababu hii, ninyi Walawi, hamkulipandisha Sanduku la Bwana mara ya kwanza, hata ikasababisha Bwana Mungu wetu kuwaka hasira dhidi yetu. Hatukumuuliza jinsi ya kufanya ili tupate kulileta jinsi alivyoagiza.”

  16. 1 Nyakati 15:14takriban 1042 KK

    Kwa hiyo makuhani pamoja na Walawi wakajitakasa ili kulipandisha Sanduku la Bwana, Mungu wa Israeli.

  17. 1 Nyakati 15:15takriban 1042 KK

    Nao Walawi wakalichukua Sanduku la Mungu mabegani mwao wakitumia mipiko, kama vile Mose alivyoamuru sawasawa na neno la Bwana.

  18. 1 Nyakati 15:16takriban 1042 KK

    Daudi akawaambia viongozi wa Walawi kuwaweka ndugu zao waimbaji ili waimbe nyimbo za shangwe, wakiwa na vyombo vya uimbaji: zeze, vinubi na matoazi.

  19. 1 Nyakati 15:17takriban 1042 KK

    Basi Walawi wakawaweka Hemani mwana wa Yoeli; kutoka miongoni mwa ndugu zake, Asafu mwana wa Berekia; kutoka miongoni mwa ndugu zao Wamerari, Ethani mwana wa Kushaiya;

  20. 1 Nyakati 15:18takriban 1042 KK

    hawa ndio waliochaguliwa kuwa wasaidizi wao: Zekaria, Yaazieli, Shemiramothi, Yehieli, Uni, Eliabu, Benaya, Maaseya, Matithia, Elifelehu, Mikneya, pamoja na mabawabu Obed-Edomu na Yehieli.

  21. 1 Nyakati 15:19takriban 1042 KK

    Waimbaji Hemani, Asafu na Ethani walichaguliwa kupiga matoazi ya shaba;

  22. 1 Nyakati 15:20takriban 1042 KK

    Zekaria, Azieli, Shemiramothi, Yehieli, Uni, Eliabu, Maaseya na Benaya walikuwa wapiga zeze kufuatana na sauti ya alamothi,

  23. 1 Nyakati 15:21takriban 1042 KK

    na Matithia, Elifelehu, Mikneya, Obed-Edomu, Yehieli na Azazia walikuwa wapiga vinubi, wakiongozwa kwa kufuata sauti ya sheminithi.

  24. 1 Nyakati 15:22takriban 1042 KK

    Kenania kiongozi wa Walawi alikuwa msimamizi wa uimbaji; huu ndio uliokuwa wajibu wake kwa sababu alikuwa stadi katika hilo.

  25. 1 Nyakati 15:23takriban 1042 KK

    Berekia na Elikana walikuwa mabawabu kwa ajili ya Sanduku.