Rukia maudhui

circa 6 BC – AD 30

The Life of Jesus

The eternal Son of God enters history: born in Bethlehem, baptized in the Jordan, crucified at Golgotha, raised on the third day.

3,779 mistari · 4 vitabu vimehusishwa

Mistari ya kipindi hiki

Chuja kwa kitabu
  1. Mathayo 4:11takriban 26 BK

    Ndipo ibilisi akamwacha, nao malaika wakaja na kumhudumia.

  2. Mathayo 4:12takriban 26 BK

    Yesu aliposikia kwamba Yohana Mbatizaji alikuwa ametiwa gerezani, alirudi Galilaya.

  3. Mathayo 4:13takriban 26 BK

    Akaondoka Nazareti akaenda kuishi Kapernaumu, mji ulioko karibu na bahari, katika mipaka ya nchi ya Zabuloni na Naftali,

  4. Mathayo 4:14takriban 26 BK

    ili kutimiza unabii wa nabii Isaya, kama alivyosema:

  5. Mathayo 4:15takriban 26 BK

    “Nchi ya Zabuloni na nchi ya Naftali, kwenye njia ya kuelekea baharini, ngʼambo ya Yordani, Galilaya ya watu wa Mataifa:

  6. Mathayo 4:16takriban 26 BK

    watu wale waliokaa gizani wameona nuru kuu; nao wale walioishi katika nchi ya uvuli wa mauti, nuru imewazukia.”

  7. Mathayo 4:17takriban 26 BK

    Tangu wakati huo, Yesu alianza kuhubiri akisema: “Tubuni, kwa maana Ufalme wa Mbinguni umekaribia.”

  8. Mathayo 4:18takriban 26 BK

    Yesu alipokuwa anatembea kando ya Bahari ya Galilaya, aliwaona ndugu wawili, Simoni aitwaye Petro, na Andrea ndugu yake. Walikuwa wakizitupa nyavu zao baharini kwa kuwa wao walikuwa wavuvi.

  9. Mathayo 4:19takriban 26 BK

    Yesu akawaambia, “Njooni, nifuateni nami nitawafanya mwe wavuvi wa watu.”

  10. Mathayo 4:20takriban 26 BK

    Mara wakaziacha nyavu zao, wakamfuata.

  11. Mathayo 4:21takriban 26 BK

    Alipoendelea mbele kutoka pale, akawaona ndugu wengine wawili, Yakobo mwana wa Zebedayo na Yohana nduguye, wakiwa wamekaa kwenye mashua pamoja na baba yao Zebedayo, wakizitengeneza nyavu zao. Yesu akawaita.

  12. Mathayo 4:22takriban 26 BK

    Nao mara wakaiacha mashua yao, pamoja na baba yao, wakamfuata.

  13. Mathayo 4:23takriban 26 BK

    Yesu akapita katika Galilaya yote, akifundisha katika masinagogi yao, akihubiri habari njema za Ufalme, na akiponya kila ugonjwa na kila aina ya maradhi miongoni mwa watu.

  14. Mathayo 4:24takriban 26 BK

    Kwa hiyo sifa zake zikaenea sehemu zote za Shamu, nao watu wakamletea wote waliokuwa na magonjwa mbalimbali na maumivu, waliopagawa na pepo wachafu, wenye kifafa na waliopooza, naye akawaponya.

  15. Mathayo 4:25takriban 26 BK

    Makutano makubwa ya watu yakawa yanamjia kutoka Galilaya, Dekapoli, Yerusalemu, Uyahudi na kutoka ngʼambo ya Mto Yordani.

  16. Mathayo 5:1takriban 31 BK

    Basi Yesu alipoona makutano, alipanda mlimani akaketi chini, nao wanafunzi wake wakamjia.

  17. Mathayo 5:2takriban 31 BK

    Ndipo akaanza kuwafundisha, akisema:

  18. Mathayo 5:3takriban 31 BK

    “Heri walio maskini wa roho, maana Ufalme wa Mbinguni ni wao.

  19. Mathayo 5:4takriban 31 BK

    Heri wale wanaohuzunika, maana hao watafarijiwa.

  20. Mathayo 5:5takriban 31 BK

    Heri walio wapole, maana hao watairithi nchi.

  21. Mathayo 5:6takriban 31 BK

    Heri wenye njaa na kiu ya haki, maana hao watatoshelezwa.

  22. Mathayo 5:7takriban 31 BK

    Heri wenye huruma, maana hao watapata rehema.

  23. Mathayo 5:8takriban 31 BK

    Heri walio na moyo safi, maana hao watamwona Mungu.

  24. Mathayo 5:9takriban 31 BK

    Heri walio wapatanishi, maana hao wataitwa wana wa Mungu.

  25. Mathayo 5:10takriban 31 BK

    Heri wanaoteswa kwa sababu ya haki, maana Ufalme wa Mbinguni ni wao.