Rukia maudhui

circa 6 BC – AD 30

The Life of Jesus

The eternal Son of God enters history: born in Bethlehem, baptized in the Jordan, crucified at Golgotha, raised on the third day.

3,779 mistari · 4 vitabu vimehusishwa

Mistari ya kipindi hiki

Chuja kwa kitabu
  1. Mathayo 3:3takriban 26 BK

    Huyu ndiye yule aliyenenwa habari zake na nabii Isaya aliposema: “Sauti ya mtu aliaye huko nyikani, ‘Tayarisheni njia kwa ajili ya Bwana, yanyoosheni mapito yake.’ ”

  2. Mathayo 3:4takriban 26 BK

    Basi Yohana alivaa mavazi yaliyotengenezwa kwa singa za ngamia, akiwa na mkanda wa ngozi kiunoni mwake. Chakula chake kilikuwa nzige na asali ya mwitu.

  3. Mathayo 3:5takriban 26 BK

    Watu walikuwa wakimwendea kutoka Yerusalemu, Uyahudi yote na nchi zote za kandokando ya Mto Yordani.

  4. Mathayo 3:6takriban 26 BK

    Nao wakaziungama dhambi zao, akawabatiza katika Mto Yordani.

  5. Mathayo 3:7takriban 26 BK

    Lakini alipowaona Mafarisayo na Masadukayo wengi wakija ili kubatizwa, aliwaambia: “Ninyi watoto wa nyoka! Ni nani aliyewaonya kuikimbia ghadhabu inayokuja?

  6. Mathayo 3:8takriban 26 BK

    Basi zaeni matunda yastahiliyo toba.

  7. Mathayo 3:9takriban 26 BK

    Wala msidhani mnaweza kusema mioyoni mwenu kuwa, ‘Sisi tunaye Abrahamu, baba yetu.’ Nawaambia kuwa Mungu anaweza kumwinulia Abrahamu watoto kutoka kwa mawe haya.

  8. Mathayo 3:10takriban 26 BK

    Hata sasa shoka limeshawekwa tayari kwenye shina la kila mti, basi kila mti usiozaa matunda mazuri, hukatwa na kutupwa motoni.

  9. Mathayo 3:11takriban 26 BK

    “Mimi nawabatiza kwa maji kwa ajili ya toba. Lakini nyuma yangu anakuja yeye aliye na uwezo kuliko mimi, ambaye sistahili hata kuvichukua viatu vyake. Yeye atawabatiza kwa Roho Mtakatifu na kwa moto.

  10. Mathayo 3:12takriban 26 BK

    Pepeto lake liko mkononi mwake, naye atasafisha sakafu yake ya kupuria, na kuikusanya ngano ghalani na kuyateketeza makapi kwa moto usiozimika.”

  11. Mathayo 3:13takriban 26 BK

    Kisha Yesu akaja kutoka Galilaya mpaka Mto Yordani ili Yohana ambatize.

  12. Mathayo 3:14takriban 26 BK

    Lakini Yohana akajitahidi kumzuia, akimwambia, “Mimi ninahitaji kubatizwa na wewe, nawe waja kwangu nikubatize?”

  13. Mathayo 3:15takriban 26 BK

    Lakini Yesu akamjibu, “Kubali hivi sasa, kwa maana ndivyo itupasavyo kwa njia hii kuitimiza haki yote.” Hivyo Yohana akakubali.

  14. Mathayo 3:16takriban 26 BK

    Naye Yesu alipokwisha kubatizwa, mara alipotoka ndani ya maji, ghafula mbingu zikafunguka, akamwona Roho wa Mungu akishuka kama hua na kutulia juu yake.

  15. Mathayo 3:17takriban 26 BK

    Nayo sauti kutoka mbinguni ikasema, “Huyu ni Mwanangu mpendwa, ambaye ninapendezwa sana naye.”

  16. Mathayo 4:1takriban 26 BK

    Kisha Yesu akaongozwa na Roho Mtakatifu kwenda nyikani ili akajaribiwe na ibilisi.

  17. Mathayo 4:2takriban 26 BK

    Baada ya kufunga siku arobaini usiku na mchana, hatimaye akaona njaa.

  18. Mathayo 4:3takriban 26 BK

    Mjaribu akamjia na kumwambia, “Ikiwa wewe ndiye Mwana wa Mungu, amuru mawe haya yawe mikate.”

  19. Mathayo 4:4takriban 26 BK

    Lakini Yesu akajibu, “Imeandikwa: ‘Mtu haishi kwa mkate tu, ila kwa kila neno litokalo katika kinywa cha Mungu.’ ”

  20. Mathayo 4:5takriban 26 BK

    Ndipo ibilisi akamchukua Yesu mpaka mji mtakatifu na kumweka juu ya mnara mrefu wa Hekalu,

  21. Mathayo 4:6takriban 26 BK

    akamwambia, “Kama wewe ndiwe Mwana wa Mungu jitupe chini. Kwa kuwa imeandikwa: “ ‘Atakuagizia malaika zake, nao watakuchukua mikononi mwao ili usije ukajikwaa mguu wako katika jiwe.’ ”

  22. Mathayo 4:7takriban 26 BK

    Yesu akamjibu, “Pia imeandikwa: ‘Usimjaribu Bwana Mungu wako.’ ”

  23. Mathayo 4:8takriban 26 BK

    Kwa mara nyingine, ibilisi akamchukua Yesu mpaka kwenye kilele cha mlima mrefu na kumwonyesha falme zote za dunia na fahari zake,

  24. Mathayo 4:9takriban 26 BK

    kisha akamwambia, “Nitakupa hivi vyote kama ukinisujudia na kuniabudu.”

  25. Mathayo 4:10takriban 26 BK

    Yesu akamwambia, “Ondoka mbele yangu, Shetani! Kwa maana imeandikwa, ‘Mwabudu Bwana Mungu wako, na umtumikie yeye peke yake.’ ”