Rukia maudhui

circa AD 48–96

Letters to the Churches

Paul and other apostles write to strengthen, correct, and encourage the scattered churches across the Roman world.

2,767 mistari · 21 vitabu vimehusishwa

Mistari ya kipindi hiki

Chuja kwa kitabu
  1. Warumi 16:20takriban 60 BK

    Mungu wa amani atamponda Shetani chini ya miguu yenu upesi. Neema ya Bwana wetu Yesu iwe nanyi. Amen.

  2. Warumi 16:21takriban 60 BK

    Timotheo, mtendakazi mwenzangu anawasalimu. Vivyo hivyo Lukio, Yasoni, na Sosipatro, ndugu zangu.

  3. Warumi 16:22takriban 60 BK

    Mimi, Tertio, niliye mwandishi wa waraka huu, nawasalimu katika Bwana.

  4. Warumi 16:23takriban 60 BK

    Gayo, ambaye ni mwenyeji wangu na wa kanisa lote, anawasalimu. Erasto, mweka hazina wa mji huu, pamoja na Kwarto ndugu yetu pia wanawasalimu. [

  5. Warumi 16:24takriban 60 BK

    Neema ya Bwana wetu Yesu Kristo iwe pamoja nanyi nyote. Amen.]

  6. Warumi 16:25takriban 60 BK

    Sasa atukuzwe yeye awezaye kuwafanya ninyi imara kwa Injili yangu na kuhubiriwa kwa Yesu Kristo, kutokana na kufunuliwa siri zilizofichika tangu zamani za kale.

  7. Warumi 16:26takriban 60 BK

    Lakini sasa siri hiyo imefunuliwa na kujulikana kupitia maandiko ya kinabii kutokana na amri ya Mungu wa milele, ili mataifa yote yaweze kumwamini na kumtii

  8. Warumi 16:27takriban 60 BK

    Mungu aliye pekee, mwenye hekima, ambaye kwa njia ya Yesu Kristo utukufu ni wake milele na milele! Amen.

  9. 1 Wakorintho 1:1takriban 59 BK

    Paulo, niliyeitwa kwa mapenzi ya Mungu kuwa mtume wa Kristo Yesu, na Sosthene ndugu yetu.

  10. 1 Wakorintho 1:2takriban 59 BK

    Kwa kanisa la Mungu lililoko Korintho, kwa wale waliotakaswa katika Kristo Yesu na walioitwa kuwa watakatifu, pamoja na wale wote ambao kila mahali wanaliitia Jina la Kristo Yesu Bwana wetu, aliye Bwana wao na wetu pia:

  11. 1 Wakorintho 1:3takriban 59 BK

    Neema na amani itokayo kwa Mungu Baba yetu na kwa Bwana Yesu Kristo iwe nanyi.

  12. 1 Wakorintho 1:4takriban 59 BK

    Ninamshukuru Mungu siku zote kwa ajili yenu kwa sababu ya neema yake mliyopewa katika Kristo Yesu.

  13. 1 Wakorintho 1:5takriban 59 BK

    Kwa kuwa katika Kristo mmetajirishwa kwa kila hali, katika kusema kwenu na katika maarifa yenu yote,

  14. 1 Wakorintho 1:6takriban 59 BK

    kwa sababu ushuhuda wetu kumhusu Kristo ulithibitishwa ndani yenu.

  15. 1 Wakorintho 1:7takriban 59 BK

    Kwa hiyo hamkupungukiwa na karama yoyote ya kiroho wakati mnangoja kwa shauku kudhihirishwa kwa Bwana wetu Yesu Kristo.

  16. 1 Wakorintho 1:8takriban 59 BK

    Atawafanya imara mpaka mwisho, ili msiwe na hatia siku ile ya Bwana wetu Yesu Kristo.

  17. 1 Wakorintho 1:9takriban 59 BK

    Mungu ambaye mmeitwa naye ili mwe na ushirika na Mwanawe Yesu Kristo, Bwana wetu ni mwaminifu.

  18. 1 Wakorintho 1:10takriban 59 BK

    Nawasihi ndugu zangu, katika Jina la Bwana wetu Yesu Kristo, kwamba mpatane nia zenu ninyi kwa ninyi, ili pasiwepo na matengano katikati yenu na kwamba mwe na umoja kikamilifu katika nia na katika kusudi.

  19. 1 Wakorintho 1:11takriban 59 BK

    Ndugu zangu, nimepata habari kutoka kwa baadhi ya watu wa nyumbani mwa Kloe kwamba kuna magomvi katikati yenu.

  20. 1 Wakorintho 1:12takriban 59 BK

    Maana yangu ni kwamba: Mmoja wenu husema, “Mimi ni wa Paulo”; mwingine, “Mimi ni wa Apolo”; mwingine, “Mimi ni wa Kefa,” na mwingine, “Mimi ni wa Kristo.”

  21. 1 Wakorintho 1:13takriban 59 BK

    Je, Kristo amegawanyika? Je, Paulo ndiye alisulubishwa kwa ajili yenu? Je, mlibatizwa kwa jina la Paulo?

  22. 1 Wakorintho 1:14takriban 59 BK

    Nashukuru kwamba sikumbatiza mtu yeyote isipokuwa Krispo na Gayo.

  23. 1 Wakorintho 1:15takriban 59 BK

    Kwa hiyo hakuna mtu yeyote anayeweza kusema kwamba alibatizwa kwa jina langu.

  24. 1 Wakorintho 1:16takriban 59 BK

    (Naam, niliwabatiza pia watu wa nyumbani mwa Stefana. Lakini zaidi ya hao sijui kama nilimbatiza mtu mwingine yeyote.)

  25. 1 Wakorintho 1:17takriban 59 BK

    Kwa maana Kristo hakunituma ili kubatiza bali kuhubiri Injili; sio kwa maneno ya hekima ya kibinadamu, ili msalaba wa Kristo usije ukakosa nguvu yake.