Rukia maudhui

circa AD 48–96

Letters to the Churches

Paul and other apostles write to strengthen, correct, and encourage the scattered churches across the Roman world.

2,767 mistari · 21 vitabu vimehusishwa

Mistari ya kipindi hiki

Chuja kwa kitabu
  1. 1 Wakorintho 1:18takriban 59 BK

    Kwa maana ujumbe wa msalaba kwa wale wanaopotea ni upuzi, lakini kwetu sisi tunaookolewa ni nguvu ya Mungu.

  2. 1 Wakorintho 1:19takriban 59 BK

    Kwa maana imeandikwa: “Nitaiharibu hekima ya wenye hekima, na kubatilisha akili ya wenye akili.”

  3. 1 Wakorintho 1:20takriban 59 BK

    Yuko wapi mwenye hekima? Yuko wapi msomi? Yuko wapi mwanafalsafa wa nyakati hizi? Je, Mungu hakufanya hekima ya ulimwengu huu kuwa upumbavu?

  4. 1 Wakorintho 1:21takriban 59 BK

    Kwa kuwa katika hekima ya Mungu, ulimwengu kwa hekima yake haukumjua yeye, ilimpendeza Mungu kuwaokoa wale walioamini kwa upuzi wa lile neno lililohubiriwa.

  5. 1 Wakorintho 1:22takriban 59 BK

    Wayahudi wanadai ishara za miujiza na Wayunani wanatafuta hekima.

  6. 1 Wakorintho 1:23takriban 59 BK

    Lakini sisi tunamhubiri Kristo aliyesulubiwa: yeye kwa Wayahudi ni kikwazo na kwa Wayunani ni upuzi.

  7. 1 Wakorintho 1:24takriban 59 BK

    Lakini kwa wale ambao Mungu amewaita, Wayahudi na pia Wayunani, Kristo ndiye nguvu ya Mungu na pia hekima ya Mungu.

  8. 1 Wakorintho 1:25takriban 59 BK

    Kwa maana upumbavu wa Mungu una hekima zaidi kuliko hekima ya wanadamu, nao udhaifu wa Mungu una nguvu kuliko nguvu ya wanadamu.

  9. 1 Wakorintho 1:26takriban 59 BK

    Ndugu zangu, kumbukeni mlivyokuwa mlipoitwa. Kwa kipimo cha kibinadamu, si wengi wenu mliokuwa na hekima. Si wengi mliokuwa na ushawishi, si wengi mliozaliwa katika jamaa zenye vyeo.

  10. 1 Wakorintho 1:27takriban 59 BK

    Lakini Mungu alivichagua vitu vipumbavu vya ulimwengu ili awaaibishe wenye hekima, Mungu alivichagua vitu dhaifu vya ulimwengu ili awaaibishe wenye nguvu.

  11. 1 Wakorintho 1:28takriban 59 BK

    Alivichagua vitu vya chini na vinavyodharauliwa vya dunia hii, vitu ambavyo haviko, ili avibatilishe vile vilivyoko,

  12. 1 Wakorintho 1:29takriban 59 BK

    ili mtu yeyote asijisifu mbele zake.

  13. 1 Wakorintho 1:30takriban 59 BK

    Bali kwa yeye ninyi mmepata kuwa katika Kristo Yesu, aliyefanyika kwetu hekima itokayo kwa Mungu, yaani haki, na utakatifu na ukombozi.

  14. 1 Wakorintho 1:31takriban 59 BK

    Hivyo, kama ilivyoandikwa: “Yeye ajisifuye na ajisifu katika Bwana.”

  15. 1 Wakorintho 2:1takriban 59 BK

    Ndugu zangu nilipokuja kwenu, sikuja na maneno ya ushawishi wala hekima ya hali ya juu nilipowahubiria siri ya Mungu.

  16. 1 Wakorintho 2:2takriban 59 BK

    Kwa kuwa niliamua kutokujua kitu chochote wakati nikiwa nanyi isipokuwa Yesu Kristo aliyesulubiwa.

  17. 1 Wakorintho 2:3takriban 59 BK

    Mimi nilikuja kwenu nikiwa dhaifu na mwenye hofu na kwa kutetemeka sana.

  18. 1 Wakorintho 2:4takriban 59 BK

    Kuhubiri kwangu na ujumbe wangu haukuwa kwa hekima na maneno ya ushawishi bali kwa madhihirisho ya nguvu za Roho

  19. 1 Wakorintho 2:5takriban 59 BK

    ili imani yenu isiwe imejengwa katika hekima ya wanadamu bali katika nguvu za Mungu.

  20. 1 Wakorintho 2:6takriban 59 BK

    Lakini miongoni mwa watu waliokomaa twanena hekima, wala si hekima ya ulimwengu huu au ya watawala wa dunia hii wanaobatilika.

  21. 1 Wakorintho 2:7takriban 59 BK

    Sisi tunanena hekima ya Mungu ambayo ni siri, tena iliyofichika, ambayo Mungu aliikusudia kabla ya ulimwengu kuwepo, kwa ajili ya utukufu wetu.

  22. 1 Wakorintho 2:8takriban 59 BK

    Hakuna hata mtawala mmoja wa nyakati hizi aliyeelewa jambo hili. Kwa maana kama wangelielewa, wasingemsulubisha Bwana wa utukufu.

  23. 1 Wakorintho 2:9takriban 59 BK

    Lakini ni kama ilivyoandikwa: “Hakuna jicho limepata kuona, wala sikio limepata kusikia, wala hayakuingia moyoni wowote, yale Mungu amewaandalia wale wampendao”:

  24. 1 Wakorintho 2:10takriban 59 BK

    Lakini mambo haya Mungu ametufunulia kwa Roho wake. Roho huchunguza kila kitu, hata mambo ya ndani sana ya Mungu.

  25. 1 Wakorintho 2:11takriban 59 BK

    Kwa maana ni nani anayejua mawazo ya mtu isipokuwa roho iliyo ndani ya huyo mtu? Vivyo hivyo hakuna mtu ajuaye mawazo ya Mungu isipokuwa Roho wa Mungu.