Rukia maudhui

Mistari ya Biblia kuhusu Woman

193 mistari · 73 vipengele

Mistari muhimu ya Biblia

Chuja kwa kitabu
  1. Mke mwenye sifa nzuri, ni nani awezaye kumpata? Yeye ni wa thamani sana kuliko marijani.

  2. Mume wake anamwamini kikamilifu wala hakosi kitu chochote cha thamani.

  3. Humtendea mumewe mema, wala si mabaya, siku zote za maisha yake.

  4. Huchagua sufu na kitani naye hufanya kazi kwa mikono yenye bidii.

  5. Yeye ni kama meli za biashara akileta chakula chake kutoka mbali.

  6. Yeye huamka kungali bado giza huwapa jamaa yake chakula na mafungu kwa watumishi wake wa kike.

  7. Huangalia shamba na kulinunua, kutokana na mapato yake hupanda shamba la mizabibu.

  8. Hufanya kazi zake kwa nguvu, mikono yake ina nguvu kwa ajili ya kazi zake.

  9. Huona kwamba biashara yake ina faida, wala taa yake haizimiki usiku.

  10. Huweka mikono yake kwenye pia, navyo vidole vyake hushikilia kijiti chenye uzi.

  11. Huwanyooshea maskini mikono yake na kuwakunjulia wahitaji vitanga vyake.

  12. Theluji ishukapo, hana hofu kwa ajili ya watu wa nyumbani mwake, kwa maana wote wamevikwa nguo za kutia joto.

  13. Hutengeneza mazulia ya urembo ya kufunika kitanda chake, yeye huvaa kitani safi na urujuani.

  14. Mume wake anaheshimiwa kwenye lango la mji, aketipo miongoni mwa wazee wa nchi.

  15. Hutengeneza mavazi ya kitani na kuyauza, naye huwauzia wafanyabiashara mishipi.

  16. Amevikwa nguvu na heshima, anaweza kucheka bila kuwa na hofu kwa siku zijazo.

  17. Huzungumza kwa hekima na mafundisho ya kuaminika yapo ulimini mwake.

  18. Huangalia mambo ya nyumbani mwake wala hali chakula cha uvivu.

  19. Watoto wake huamka na kumwita aliyebarikiwa, mumewe pia humsifu, akisema:

  20. Kujipamba ili kuvutia ni udanganyifu na uzuri unapita upesi, bali mwanamke anayemcha Bwana atasifiwa.

  21. Nimeona jambo lililo chungu kuliko mauti, mwanamke ambaye ni mtego, ambaye moyo wake ni wavu wa kutegea na mikono yake ni minyororo. Mtu ampendezaye Mungu atamkwepa, bali mwenye dhambi atanaswa naye.

  22. Manukato yako yananukia vizuri, jina lako ni kama manukato yaliyomiminwa. Ndiyo sababu wanawali wanakupenda!

  23. Mimi ni mweusi, lakini napendeza, enyi binti za Yerusalemu, mweusi kama mahema ya Kedari, kama mapazia ya hema la Solomoni.

  24. Usinikazie macho kwa sababu mimi ni mweusi, kwa sababu nimefanywa mweusi na jua. Wana wa mama yangu walinikasirikia na kunifanya niwe mtunza mashamba ya mizabibu. Shamba langu mwenyewe la mizabibu nimeliacha.

  25. Kama hujui, ewe mwanamke mzuri kuliko wote, fuata nyayo za kondoo, na kulisha wana-mbuzi wako karibu na hema za wachungaji.