Skip to content

Mistari ya Biblia kuhusu The Scriptures

159 mistari · 108 vipengele

Mistari muhimu ya Biblia

Chuja kwa kitabu
  1. Maneno ya Bwana ni safi, kama fedha iliyosafishwa katika tanuru, iliyosafishwa mara saba.

  2. Kuhusu matendo ya wanadamu: kwa neno la midomo yako, nimejiepusha na njia za wenye jeuri.

  3. Sheria ya Bwana ni kamilifu, ikihuisha nafsi. Shuhuda za Bwana ni za kuaminika, zikimpa mjinga hekima.

  4. Maagizo ya Bwana ni kamili, nayo hufurahisha moyo. Amri za Bwana huangaza, zatia nuru machoni.

  5. Ni za thamani kuliko dhahabu, kuliko dhahabu iliyo safi sana, ni tamu kuliko asali, kuliko asali kutoka kwenye sega.

  6. Kwa hizo mtumishi wako anaonywa, katika kuzishika kuna thawabu kubwa.

  7. Ndipo niliposema, “Mimi hapa, nimekuja: imeandikwa kunihusu katika kitabu.

  8. Kijana aifanye njia yake kuwa safi jinsi gani? Ni kwa kutii, akilifuata neno lako.

  9. Nimelificha neno lako moyoni mwangu ili nisikutende dhambi.

  10. Sifa ni zako, Ee Bwana, nifundishe maagizo yako.

  11. Kwa midomo yangu nitasimulia sheria zote zinazotoka katika kinywa chako.

  12. Ninafurahia maagizo yako, wala sitalipuuza neno lako.

  13. Nimelazwa chini mavumbini, yahifadhi maisha yangu sawasawa na neno lako.

  14. Nafsi yangu imechakazwa kwa huzuni, uniimarishe sawasawa na neno lako.

  15. Ee Bwana, nifundishe kuyafuata maagizo yako, nami nitayashika mpaka mwisho.

  16. Ee Bwana, upendo wako usiokoma unijie, wokovu wako sawasawa na ahadi yako,

  17. ndipo nitakapomjibu anayenidhihaki, kwa kuwa ninalitumainia neno lako.

  18. Kumbuka neno lako kwa mtumishi wako, kwa sababu umenipa tumaini.

  19. Faraja yangu katika mateso yangu ni hii: Ahadi yako inahifadhi maisha yangu.

  20. Nifundishe maarifa na uamuzi mzuri, kwa kuwa ninaamini amri zako.

  21. Kabla sijapata shida nilipotea njia, lakini sasa ninalitii neno lako.

  22. Wakuchao wafurahie wanaponiona, kwa kuwa nimeweka tumaini langu katika neno lako.

  23. Upendo wako usiokoma uwe faraja yangu, sawasawa na ahadi yako kwa mtumishi wako.

  24. Nafsi yangu inazimia kwa kutamani wokovu wako, lakini nimeweka tumaini langu katika neno lako.

  25. Macho yangu yamefifia, nikingoja ahadi yako; ninasema, “Utanifajiri lini?”