Skip to content

Mistari ya Biblia kuhusu The Scriptures

159 mistari · 108 vipengele

Mistari muhimu ya Biblia

Chuja kwa kitabu
  1. Sitasahau mausia yako kamwe, kwa maana kwayo umehifadhi maisha yangu.

  2. Aha! Tazama, sheria yako naipenda mno ajabu. Ninaitafakari mchana kutwa.

  3. Nina akili zaidi kuliko walimu wangu wote, kwa kuwa ninatafakari juu ya sheria zako.

  4. Tazama jinsi maneno yako yalivyo matamu kwangu, matamu kuliko asali katika kinywa changu!

  5. Neno lako ni taa ya miguu yangu na mwanga katika njia yangu.

  6. Sheria zako ni urithi wangu milele, naam ni furaha ya moyo wangu.

  7. Ninachukia watu wa nia mbili, lakini ninapenda sheria yako.

  8. Kuingia kwa maneno yako kunaleta nuru, kunampa mjinga ufahamu.

  9. Ongoza hatua zangu kulingana na neno lako, usiache dhambi yoyote initawale.

  10. Ahadi zako zimejaribiwa kikamilifu, mtumishi wako anazipenda.

  11. Ninaamka asubuhi na mapema na kukuomba msaada; nimeweka tumaini langu katika neno lako.

  12. Sikufumba macho yangu usiku kucha, ili niweze kutafakari juu ya ahadi zako.

  13. Ninawatazama wasioamini kwa chuki, kwa kuwa hawalitii neno lako.

  14. Tazama jinsi ninavyopenda mausia yako; Ee Bwana, uyahifadhi maisha yangu, sawasawa na upendo wako.

  15. Maneno yako yote ni kweli, sheria zako zote za haki ni za milele.

  16. Watawala wamenitesa bila sababu, lakini moyo wangu unatetemeka kwa neno lako.

  17. Nafurahia ahadi zako kama mtu aliyepata mateka mengi.

  18. Ninazitii sheria zako, kwa sababu ninazipenda mno.

  19. Ee Bwana, kilio changu na kifike mbele zako, nipe ufahamu sawasawa na neno lako.

  20. Ulimi wangu na uimbe kuhusu neno lako, kwa kuwa amri zako zote ni za haki.

  21. Kwa maana amri hizi ni taa, mafundisho haya ni mwanga na maonyo ya maadili ni njia ya uzima,

  22. “Kila neno la Mungu ni kamilifu; yeye ni ngao kwa wale wanaomkimbilia.

  23. Kwa sheria na kwa ushuhuda! Kama hawatasema sawasawa na neno hili, hawana mwanga wa mapambazuko.

  24. Hawa ni watu waasi, watoto wadanganyifu, watoto ambao hawataki kusikiliza mafundisho ya Bwana.

  25. Angalieni katika gombo la Bwana na msome: Hakuna hata mmoja katika hawa atakayekosekana, hakuna hata mmoja atakayemkosa mwenzi wake. Kwa kuwa ni kinywa chake Mungu kimeagiza, na Roho wake atawakusanya pamoja.