Rukia maudhui

Mistari ya Biblia kuhusu Psalms

896 mistari · 16 vipengele

Mistari muhimu ya Biblia

Chuja kwa kitabu
  1. Kaeni mbali nami, ninyi nyote mtendao mabaya, kwa maana Bwana amesikia kulia kwangu.

  2. Bwana amesikia kilio changu kwa huruma, Bwana amekubali sala yangu.

  3. Adui zangu wote wataaibika na kufadhaika, watarudi nyuma kwa aibu ya ghafula.

  4. Kwa mwimbishaji. Mtindo wa gitithi. Zaburi ya Daudi. Ee Bwana, Bwana wetu, tazama jinsi lilivyo tukufu jina lako duniani mwote! Umeuweka utukufu wako juu ya mbingu.

  5. Midomoni mwa watoto wachanga na wanyonyao umeamuru sifa, kwa sababu ya watesi wako, kumnyamazisha adui na mlipiza kisasi.

  6. Nikiziangalia mbingu zako, kazi ya vidole vyako, mwezi na nyota, ulizoziratibisha,

  7. mwanadamu ni kitu gani hata unamfikiria, binadamu ni nani hata unamjali?

  8. Umemfanya chini kidogo kuliko viumbe wa mbinguni, ukamvika taji ya utukufu na heshima.

  9. Umemfanya mtawala juu ya kazi za mikono yako; umeweka vitu vyote chini ya miguu yake.

  10. Mifugo na makundi yote pia, naam, na wanyama wa kondeni,

  11. ndege wa angani na samaki wa baharini, naam, kila kiogeleacho katika njia za bahari.

  12. Ee Bwana, Bwana wetu, tazama jinsi lilivyo tukufu jina lako duniani mwote!

  13. Kwa mwimbishaji. Zaburi ya Daudi. Kwa Bwana ninakimbilia, unawezaje basi kuniambia: “Ruka kama ndege kwenye mlima wako.

  14. Hebu tazama, waovu wanapinda pinde zao, huweka mishale kwenye uzi wake, wakiwa gizani ili kuwapiga wale wanyofu wa moyo.

  15. Wakati misingi imeharibiwa, mwenye haki anaweza kufanya nini?”

  16. Bwana yuko ndani ya Hekalu lake takatifu; Bwana yuko kwenye kiti chake cha enzi mbinguni. Huwaangalia wana wa watu, macho yake yanawajaribu.

  17. Bwana huwajaribu wenye haki, lakini waovu na wanaopenda jeuri, nafsi yake huwachukia.

  18. Atawanyeshea waovu makaa ya moto mkali na kiberiti kinachowaka, upepo wenye joto kali ndio fungu lao.

  19. Kwa kuwa Bwana ni mwenye haki, yeye hupenda haki. Wanyofu watauona uso wake.

  20. Kwa mwimbishaji. Mtindo wa sheminithi. Zaburi ya Daudi. Bwana tusaidie, kwa kuwa wacha Mungu wametoweka; waaminifu wametoweka miongoni mwa wanadamu.

  21. Kila mmoja humwambia jirani yake uongo; midomo yao ya hila huzungumza kwa udanganyifu.

  22. Bwana na akatilie mbali midomo yote ya hila na kila ulimi uliojaa majivuno,

  23. ule unaosema, “Kwa ndimi zetu tutashinda; midomo ni mali yetu, bwana wetu ni nani?”

  24. “Kwa sababu ya uonevu wa wanyonge na kulia kwa uchungu kwa wahitaji, nitainuka sasa,” asema Bwana. “Nitawalinda kutokana na wale wenye nia mbaya juu yao.”

  25. Maneno ya Bwana ni safi, kama fedha iliyosafishwa katika tanuru, iliyosafishwa mara saba.