Rukia maudhui

Mistari ya Biblia kuhusu Psalms: Intercessional Psalms

40 mistari · 16 vipengele

Mistari kuhusu Intercessional Psalms

  1. Kwa mwimbishaji. Zaburi ya Daudi. Bwana na akujibu unapokuwa katika dhiki, jina la Mungu wa Yakobo na liwe kinga yako.

  2. Na akutumie msaada kutoka patakatifu na akupatie msaada kutoka Sayuni.

  3. Na azikumbuke dhabihu zako zote, na azikubali sadaka zako za kuteketezwa.

  4. Na akujalie haja ya moyo wako, na aifanikishe mipango yako yote.

  5. Tutashangilia kwa furaha utakaposhinda, tutainua bendera zetu kwa jina la Mungu wetu. Bwana na akupe haja zako zote.

  6. Sasa nafahamu kuwa Bwana humwokoa mpakwa mafuta wake, humjibu kutoka mbingu yake takatifu kwa nguvu za wokovu wa mkono wake wa kuume.

  7. Wengine wanatumaini magari ya vita, na wengine farasi, bali sisi tutalitumainia jina la Bwana, Mungu wetu.

  8. Wao wameshushwa chini na kuanguka, bali sisi tunainuka na kusimama imara.

  9. Ee Bwana, mwokoe mfalme! Tujibu tunapokuita!

  10. Kwa mwimbishaji. Na ala za nyuzi za muziki. Zaburi. Wimbo. Mungu aturehemu na kutubariki, na kutuangazia nuru za uso wake,

  11. ili njia zako zijulikane duniani, wokovu wako katikati ya mataifa yote.

  12. Ee Mungu, mataifa na wakusifu, mataifa yote na wakusifu.

  13. Mataifa yote wafurahi na kuimba kwa shangwe, kwa kuwa unatawala watu kwa haki na kuongoza mataifa ya dunia.

  14. Ee Mungu, mataifa na wakusifu, mataifa yote na wakusifu.

  15. Ndipo nchi itatoa mazao yake, naye Mungu, Mungu wetu, atatubariki.

  16. Mungu atatubariki na miisho yote ya dunia itamcha yeye.

  17. Wimbo wa kwenda juu. Wa Daudi. Nilishangilia pamoja na wale walioniambia, “Twende nyumbani ya Bwana.”

  18. Ee Yerusalemu, miguu yetu imesimama malangoni mwako.

  19. Yerusalemu imejengwa vyema kama mji ambao umeshikamanishwa pamoja.

  20. Huko ndiko makabila hukwea, makabila ya Bwana, kulisifu jina la Bwana kulingana na maagizo waliopewa Israeli.

  21. Huko viti vya enzi vya hukumu hukaa, viti vya enzi vya nyumba ya Daudi.

  22. Omba kwa ajili ya amani ya Yerusalemu: “Wote wakupendao na wawe salama.

  23. Amani na iwepo ndani ya kuta zako na usalama ndani ya ngome zako.”

  24. Kwa ajili ya ndugu zangu na marafiki, nitasema, “Amani iwe ndani yako.”

  25. Kwa ajili ya nyumba ya Bwana Mungu wetu, nitatafuta mafanikio yako.