Rukia maudhui

Mistari ya Biblia kuhusu Psalms: Didactic Psalms

225 mistari · 16 vipengele

Mistari kuhusu Didactic Psalms

  1. Heri mtu yule ambaye haendi katika shauri la watu waovu, wala hasimami katika njia ya wenye dhambi, au kuketi katika baraza la wenye mizaha.

  2. Bali huifurahia sheria ya Bwana, naye huitafakari hiyo sheria usiku na mchana.

  3. Mtu huyo ni kama mti uliopandwa kando ya vijito vya maji, ambao huzaa matunda kwa majira yake na majani yake hayanyauki. Lolote afanyalo hufanikiwa.

  4. Sivyo walivyo waovu! Wao ni kama makapi yapeperushwayo na upepo.

  5. Kwa hiyo waovu hawatastahimili hukumu, wala wenye dhambi katika kusanyiko la wenye haki.

  6. Kwa maana Bwana huziangalia njia za mwenye haki, bali njia ya waovu itaangamia.

  7. Kwa mwimbishaji. Kwa filimbi. Zaburi ya Daudi. Ee Bwana, tegea sikio maneno yangu, uangalie kupiga kite kwangu.

  8. Sikiliza kilio changu ili unisaidie, Mfalme wangu na Mungu wangu, kwa maana kwako ninaomba.

  9. Asubuhi, unasikia sauti yangu, Ee Bwana; asubuhi naleta haja zangu mbele zako, na kusubiri kwa matumaini.

  10. Wewe si Mungu unayefurahia uovu, kwako mtu mwovu hataishi.

  11. Wenye kiburi hawawezi kusimama mbele yako, unawachukia wote watendao mabaya.

  12. Unawaangamiza wasemao uongo. Bwana huwachukia wamwagao damu na wadanganyifu.

  13. Lakini mimi, kwa rehema zako kuu, nitakuja katika nyumba yako, kwa unyenyekevu, nitasujudu kuelekea Hekalu lako takatifu.

  14. Niongoze katika haki yako, Ee Bwana, kwa sababu ya adui zangu, nyoosha njia yako mbele yangu.

  15. Hakuna neno kinywani mwao linaloweza kuaminika, mioyo yao imejaa maangamizi. Koo lao ni kaburi lililo wazi, kwa ndimi zao, wao hunena udanganyifu.

  16. Uwatangaze kuwa wenye hatia, Ee Mungu! Hila zao ziwe anguko lao wenyewe. Wafukuzie mbali kwa sababu ya dhambi zao nyingi, kwa kuwa wamekuasi wewe.

  17. Lakini wote wakimbiliao kwako na wafurahi, waimbe kwa shangwe daima. Ueneze ulinzi wako juu yao, ili wale wapendao jina lako wapate kukushangilia.

  18. Kwa hakika, Ee Bwana, unawabariki wenye haki, unawazunguka kwa wema wako kama ngao.

  19. Kwa mwimbishaji. Zaburi ya Daudi. Kwa Bwana ninakimbilia, unawezaje basi kuniambia: “Ruka kama ndege kwenye mlima wako.

  20. Hebu tazama, waovu wanapinda pinde zao, huweka mishale kwenye uzi wake, wakiwa gizani ili kuwapiga wale wanyofu wa moyo.

  21. Wakati misingi imeharibiwa, mwenye haki anaweza kufanya nini?”

  22. Bwana yuko ndani ya Hekalu lake takatifu; Bwana yuko kwenye kiti chake cha enzi mbinguni. Huwaangalia wana wa watu, macho yake yanawajaribu.

  23. Bwana huwajaribu wenye haki, lakini waovu na wanaopenda jeuri, nafsi yake huwachukia.

  24. Atawanyeshea waovu makaa ya moto mkali na kiberiti kinachowaka, upepo wenye joto kali ndio fungu lao.

  25. Kwa kuwa Bwana ni mwenye haki, yeye hupenda haki. Wanyofu watauona uso wake.