Rukia maudhui

Mistari ya Biblia kuhusu Psalms: For God's mercies to individuals

58 mistari · 16 vipengele

Mistari kuhusu For God's mercies to individuals

  1. Utenzi wa kuweka wakfu hekalu. Zaburi ya Daudi. Nitakutukuza wewe, Ee Bwana, kwa kuwa umeniinua kutoka vilindi, na hukuacha adui zangu washangilie juu yangu.

  2. Ee Bwana, Mungu wangu, nilikuita unisaidie na wewe umeniponya.

  3. Ee Bwana, umenitoa Kuzimu, umeniokoa nisishuke kwenye shimo la mauti.

  4. Mwimbieni Bwana, enyi watakatifu wake; lisifuni jina lake takatifu.

  5. Kwa maana hasira yake ni ya muda mfupi, bali upendo wake hudumu siku zote. Inawezekana kilio kiwepo usiku kucha, lakini asubuhi kukawa na furaha.

  6. Nilipofanikiwa nilisema, “Sitatikiswa kamwe.”

  7. Ee Bwana, uliponijalia, uliuimarisha mlima wangu, lakini ulipouficha uso wako nilifadhaika.

  8. Kwako wewe, Ee Bwana, niliita, kwa Bwana niliomba rehema:

  9. “Kuna faida gani katika kuangamia kwangu? Katika kushuka kwangu shimoni? Je, mavumbi yatakusifu? Je, yatatangaza uaminifu wako?

  10. Ee Bwana, unisikie na kunihurumia, Ee Bwana, uwe msaada wangu.”

  11. Uligeuza maombolezo yangu kuwa kucheza, ulinivua nguo za gunia ukanivika shangwe,

  12. ili moyo wangu uweze kukusifu na usikae kimya. Ee Bwana Mungu wangu, nitakushukuru milele.

  13. Kwa mwimbishaji. Mtindo wa “Usiharibu!” Zaburi ya Asafu. Wimbo. Ee Mungu, tunakushukuru, tunakushukuru wewe, kwa kuwa jina lako li karibu; watu husimulia matendo yako ya ajabu.

  14. Unasema, “Ninachagua wakati maalum; ni mimi nihukumuye kwa haki.

  15. Wakati dunia na watu wake wote inapotetemeka, ni mimi ninayezishikilia nguzo zake imara.

  16. Kwa wale wenye majivuno ninasema, ‘Msijisifu tena,’ kwa wale waovu, ‘Msiinue pembe zenu.

  17. Msiinue pembe zenu dhidi ya mbingu; msiseme kwa shingo zilizonyooshwa.’ ”

  18. Hakuna yeyote atokaye mashariki wala magharibi au kutoka jangwani awezaye kumkweza mwanadamu.

  19. Bali Mungu ndiye ahukumuye: Humshusha huyu na kumkweza mwingine.

  20. Mkononi mwa Bwana kuna kikombe kilichojaa mvinyo unaotoka povu uliochanganywa na vikolezo; huumimina, nao waovu wote wa dunia hunywa mpaka tone la mwisho.

  21. Bali mimi, nitatangaza hili milele; nitaimba sifa kwa Mungu wa Yakobo.

  22. Nitazikatilia mbali pembe za waovu wote, bali pembe za wenye haki zitainuliwa juu.

  23. Wimbo. Zaburi ya Daudi. Ee Mungu, moyo wangu ni thabiti; nitaimba na kusifu kwa moyo wangu wote.

  24. Amka, kinubi na zeze! Nitayaamsha mapambazuko.

  25. Nitakusifu wewe, Ee Bwana, katikati ya mataifa; nitaimba habari zako, katikati ya jamaa za watu.