Rukia maudhui

Mistari ya Biblia kuhusu Psalms: Of Zacharias

12 mistari · 16 vipengele

Mistari kuhusu Of Zacharias

  1. “Ahimidiwe Bwana, Mungu wa Israeli, kwa kuwa amewajilia watu wake na kuwakomboa.

  2. Naye ametusimamishia pembe ya wokovu katika nyumba ya Daudi mtumishi wake,

  3. kama alivyonena kwa vinywa vya manabii wake watakatifu tangu zamani,

  4. kwamba atatuokoa kutoka kwa adui zetu, na kutoka mikononi mwao wote watuchukiao:

  5. ili kuonyesha rehema kwa baba zetu na kukumbuka Agano lake takatifu,

  6. kiapo alichomwapia baba yetu Abrahamu:

  7. kutuokoa kutoka mikononi mwa adui zetu, tupate kumtumikia yeye pasipo hofu

  8. katika utakatifu na haki mbele zake, siku zetu zote.

  9. “Nawe mtoto wangu, utaitwa nabii wa Aliye Juu Sana; kwa kuwa utamtangulia Bwana na kuandaa njia kwa ajili yake,

  10. kuwajulisha watu wake juu ya wokovu utakaopatikana kwa kusamehewa dhambi zao,

  11. kwa ajili ya wingi wa rehema za Mungu wetu, nuru itokayo juu itatuzukia

  12. ili kuwaangazia wale waishio gizani na katika uvuli wa mauti, kuiongoza miguu yetu katika njia ya amani.”