Rukia maudhui

Mistari ya Biblia kuhusu Psalms

896 mistari · 16 vipengele

Mistari muhimu ya Biblia

Chuja kwa kitabu
  1. Alama za mipaka zimeniangukia mahali pazuri, hakika nimepata urithi mzuri.

  2. Nitamsifu Bwana ambaye hunishauri, hata wakati wa usiku moyo wangu hunifundisha.

  3. Nimemweka Bwana mbele yangu daima. Kwa sababu yuko mkono wangu wa kuume, sitatikisika.

  4. Kwa hiyo moyo wangu unafurahia, na ulimi wangu unashangilia; mwili wangu nao utapumzika salama,

  5. kwa maana hutaniacha kaburini, wala hutamwacha Mtakatifu Wako kuona uharibifu.

  6. Umenijulisha njia ya uzima; utanijaza na furaha mbele zako, pamoja na furaha za milele katika mkono wako wa kuume.

  7. Sala ya Daudi. Sikia, Ee Bwana, kusihi kwangu kwa haki, sikiliza kilio changu. Tega sikio kwa ombi langu, halitoki kwenye midomo ya udanganyifu.

  8. Hukumu yangu na itoke kwako, macho yako na yaone yale yaliyo haki.

  9. Ingawa unauchunguza moyo wangu na kunikagua usiku, ingawa umenijaribu, hutaona chochote. Nimeamua kwamba kinywa changu hakitatenda dhambi.

  10. Kuhusu matendo ya wanadamu: kwa neno la midomo yako, nimejiepusha na njia za wenye jeuri.

  11. Hatua zangu zimeshikamana na njia zako; nyayo zangu hazikuteleza.

  12. Ee Mungu, ninakuita, kwa kuwa utanijibu, nitegee sikio lako na usikie ombi langu.

  13. Uonyeshe ajabu ya upendo wako mkuu, wewe uokoaye kwa mkono wako wa kuume wale wanaokukimbilia kutokana na adui zao.

  14. Nilinde kama mboni ya jicho lako, unifiche chini ya kivuli cha mbawa zako

  15. kutokana na waovu wanaonishambulia, kutokana na adui wauaji wanaonizunguka.

  16. Huifunga mioyo yao iliyo migumu, vinywa vyao hunena kwa majivuno.

  17. Wamenifuatia nyayo zangu, sasa wamenizingira, wakiwa macho, waniangushe chini.

  18. Wamefanana na simba mwenye njaa awindaye, kama simba mkubwa anyemeleaye mafichoni.

  19. Inuka, Ee Bwana, pambana nao, uwaangushe, niokoe kutokana na waovu kwa upanga wako.

  20. Ee Bwana, mkono wako uniokoe na watu wa jinsi hii, kutokana na watu wa ulimwengu huu ambao fungu lao liko katika maisha haya. Na wapate adhabu ya kuwatosha. Watoto wao na wapate zaidi ya hayo, hukumu na iendelee kwa watoto wa watoto wao.

  21. Na mimi katika haki nitauona uso wako, niamkapo, nitaridhika kwa kuona sura yako.

  22. Kwa mwimbishaji. Zaburi ya Daudi. Mbingu zinatangaza utukufu wa Mungu, anga zahubiri kazi ya mikono yake.

  23. Siku baada ya siku zinatoa habari, usiku baada ya usiku zinatangaza maarifa.

  24. Hakuna msemo wala lugha, ambapo sauti zao hazisikiki.

  25. Sauti yao imeenea duniani pote, nayo maneno yao yameenea hadi miisho ya ulimwengu. Katika mbingu amepiga hema kwa ajili ya jua,