Rukia maudhui

Mistari ya Biblia kuhusu Psalms

896 mistari · 16 vipengele

Mistari muhimu ya Biblia

Chuja kwa kitabu
  1. Fahamuni hakika kwamba Bwana amewatenga wale wamchao kwa ajili yake; Bwana atanisikia nimwitapo.

  2. Katika hasira yako, usitende dhambi. Mkiwa vitandani mwenu, mtulie kimya mkiichunguza mioyo yenu.

  3. Toeni dhabihu zilizo haki; mtegemeeni Bwana.

  4. Wengi wanauliza, “Ni nani awezaye kutuonyesha jema lolote?” Ee Bwana, tuangazie nuru ya uso wako.

  5. Wewe umejaza moyo wangu kwa furaha kubwa kuliko watu waliopata nafaka na divai kwa wingi.

  6. Nitajilaza chini na kulala kwa amani, kwa kuwa wewe peke yako, Ee Bwana, waniwezesha kukaa kwa salama.

  7. Kwa mwimbishaji. Kwa filimbi. Zaburi ya Daudi. Ee Bwana, tegea sikio maneno yangu, uangalie kupiga kite kwangu.

  8. Sikiliza kilio changu ili unisaidie, Mfalme wangu na Mungu wangu, kwa maana kwako ninaomba.

  9. Asubuhi, unasikia sauti yangu, Ee Bwana; asubuhi naleta haja zangu mbele zako, na kusubiri kwa matumaini.

  10. Wewe si Mungu unayefurahia uovu, kwako mtu mwovu hataishi.

  11. Wenye kiburi hawawezi kusimama mbele yako, unawachukia wote watendao mabaya.

  12. Unawaangamiza wasemao uongo. Bwana huwachukia wamwagao damu na wadanganyifu.

  13. Lakini mimi, kwa rehema zako kuu, nitakuja katika nyumba yako, kwa unyenyekevu, nitasujudu kuelekea Hekalu lako takatifu.

  14. Niongoze katika haki yako, Ee Bwana, kwa sababu ya adui zangu, nyoosha njia yako mbele yangu.

  15. Hakuna neno kinywani mwao linaloweza kuaminika, mioyo yao imejaa maangamizi. Koo lao ni kaburi lililo wazi, kwa ndimi zao, wao hunena udanganyifu.

  16. Uwatangaze kuwa wenye hatia, Ee Mungu! Hila zao ziwe anguko lao wenyewe. Wafukuzie mbali kwa sababu ya dhambi zao nyingi, kwa kuwa wamekuasi wewe.

  17. Lakini wote wakimbiliao kwako na wafurahi, waimbe kwa shangwe daima. Ueneze ulinzi wako juu yao, ili wale wapendao jina lako wapate kukushangilia.

  18. Kwa hakika, Ee Bwana, unawabariki wenye haki, unawazunguka kwa wema wako kama ngao.

  19. Kwa mwimbishaji. Kwa ala za nyuzi za muziki. Mtindo wa sheminithi. Zaburi ya Daudi. Ee Bwana, usinikemee katika hasira yako, wala usiniadhibu katika ghadhabu yako.

  20. Unirehemu Bwana, kwa maana nimedhoofika; Ee Bwana, uniponye, kwa maana mifupa yangu ina maumivu makali.

  21. Nafsi yangu ina uchungu mwingi. Mpaka lini, Ee Bwana, mpaka lini?

  22. Geuka Ee Bwana, unikomboe, uniokoe kwa sababu ya fadhili zako.

  23. Hakuna mtu anayekukumbuka akiwa amekufa. Ni nani awezaye kukusifu akiwa kuzimu?

  24. Nimechakaa kwa kulia kwa huzuni; usiku kucha nafurikisha kitanda changu kwa machozi; nimelowesha viti vyangu vya fahari kwa machozi.

  25. Macho yangu yamedhoofika kwa kuhuzunika, yamedhoofika kwa sababu ya adui zangu wote.