Skip to content

Mistari ya Biblia kuhusu Pride

303 mistari · 61 vipengele

Mistari muhimu ya Biblia

Chuja kwa kitabu
  1. Wakati Hamani alipoona kuwa Mordekai hampigii magoti wala kumpa heshima alighadhibika.

  2. Mpumbavu aweza kuwa mwenye hekima, endapo mtoto wa punda-mwitu atazaliwa mwanadamu.

  3. “Bila shaka ninyi ndio watu, nayo hekima itakoma mtakapokufa!

  4. Lakini mimi ninao ufahamu kama ninyi; mimi si duni kwenu. Ni nani asiyejua mambo haya yote?

  5. Hayo mnayoyajua mimi pia ninayajua; mimi si mtu duni kuliko ninyi.

  6. Laiti wote mngenyamaza kimya! Kwa kuwa kwenu hilo lingekuwa hekima.

  7. Kisha Elifazi Mtemani akajibu:

  8. “Je, mtu mwenye hekima hujibu kwa mawazo matupu, au kujaza tumbo lake kwa upepo wenye joto wa mashariki?

  9. Je, aweza kubishana juu ya maneno yasiyofaa, kwa hotuba zisizo na maana?

  10. Lakini unadhoofisha hata uchaji wa Mungu na kuzuia ibada mbele za Mungu.

  11. Dhambi yako inasukuma kinywa chako, nawe umechagua ulimi wa hila.

  12. Kinywa chako mwenyewe kinakuhukumu, wala si changu; midomo yako mwenyewe inashuhudia dhidi yako.

  13. “Je, wewe ni mtu wa kwanza kuzaliwa? Ulizaliwa kabla ya vilima?

  14. Je, wewe husikiliza mashauri ya siri ya Mungu? Je, wewe unaizuia hekima iwe yako mwenyewe?

  15. Wewe unajua kitu gani tusichokijua sisi? Unafahamu kitu gani tusichokifahamu sisi?

  16. Wale wenye mvi na wazee wako upande wetu, watu ambao ni wazee hata kuliko baba yako.

  17. Je, faraja za Mungu hazikutoshi, au maneno yaliyosemwa kwako kwa upole si kitu?

  18. Kwa nini moyo wako unakudanganya, na kwa nini macho yako yanangʼaa,

  19. ili kwamba upate kutoa hasira yako dhidi ya Mungu, na kumwaga maneno kama hayo kutoka kinywani mwako?

  20. Kwa nini sisi tunafikiriwa kama wanyama, na kuonekana wajinga machoni pako?

  21. Wewe unayejirarua mwenyewe vipande vipande katika hasira yako, je, dunia iachwe kwa ajili yako wewe? Au ni lazima miamba iondolewe mahali pake?

  22. Ni nani hulaumu matendo yake mbele ya uso wake? Ni nani ampatilizaye kwa yale aliyoyatenda?

  23. Hupelekwa kaburini, nao ulinzi ukawekwa kwenye kaburi lake.

  24. Sio wazee peke yao walio na hekima, sio wenye umri mkubwa peke yao wanaofahamu lililo sawa.

  25. “Kwa hiyo nasema: Nisikilizeni mimi; mimi nami nitawaambia lile ninalojua.