Skip to content

Mistari ya Biblia kuhusu Pride

303 mistari · 61 vipengele

Mistari muhimu ya Biblia

Chuja kwa kitabu
  1. Nilingojea mlipokuwa mnaongea, nilizisikiliza hoja zenu; mlipokuwa mkitafuta maneno ya kusema,

  2. niliwasikiliza kwa makini. Lakini hakuna hata mmoja wenu aliyethibitisha kwamba Ayubu amekosa; hakuna hata mmoja wenu aliyeweza kujibu hoja zake.

  3. Msiseme, ‘Tumepata hekima; Mungu na amthibitishe kuwa mwongo, wala si mwanadamu.’

  4. Kwa hiyo, wanadamu mheshimuni, kwa kuwa yeye hamstahi yeyote anayejidhania kuwa ana hekima.”

  5. Ee Bwana, wapige kwa hofu, mataifa na yajue kuwa wao ni watu tu.

  6. Katika kiburi chake, mwovu humtesa maskini, waovu na wanaswe katika hila wanazozitunga.

  7. Hujivunia tamaa za moyo wake; humbariki mlafi na kumtukana Bwana.

  8. Katika kiburi chake, mwovu hamtafuti Mungu, katika mawazo yake yote hakuna nafasi ya Mungu.

  9. Njia zake daima hufanikiwa; hujivuna na amri zako ziko mbali naye, huwacheka kwa dharau adui zake wote.

  10. Anajisemea mwenyewe, “Hakuna kitakachonitikisa, daima nitakuwa na furaha, kamwe sitakuwa na shida.”

  11. Anajisemea mwenyewe, “Mungu amesahau, huficha uso wake na haoni kabisa.”

  12. Bwana na akatilie mbali midomo yote ya hila na kila ulimi uliojaa majivuno,

  13. ule unaosema, “Kwa ndimi zetu tutashinda; midomo ni mali yetu, bwana wetu ni nani?”

  14. Wewe huwaokoa wanyenyekevu, lakini huwashusha wenye kiburi.

  15. Mpendeni Bwana ninyi watakatifu wake wote! Bwana huwahifadhi waaminifu, lakini wenye kiburi huwalipiza kikamilifu.

  16. Heri mtu yule amfanyaye Bwana kuwa tumaini lake, asiyewategemea wenye kiburi, wale wenye kugeukia miungu ya uongo.

  17. Makaburi yao yatabaki kuwa nyumba zao za milele, makao yao vizazi vyote; ingawa walikuwa na mashamba na kuyaita kwa majina yao.

  18. “Huyu ni yule mtu ambaye hakumfanya Mungu kuwa ngome yake, bali alitumainia wingi wa utajiri wake, na akawa hodari kwa kuwaangamiza wengine!”

  19. Kwa hiyo kiburi ni mkufu wao, wamejivika jeuri.

  20. Hudhihaki na kusema kwa ukorofi, katika majivuno yao wanatishia kutesa.

  21. Vinywa vyao huweka madai hata kwa mbingu, nazo ndimi zao humiliki duniani.

  22. Kwa wale wenye majivuno ninasema, ‘Msijisifu tena,’ kwa wale waovu, ‘Msiinue pembe zenu.

  23. Msiinue pembe zenu dhidi ya mbingu; msiseme kwa shingo zilizonyooshwa.’ ”

  24. Hakuna yeyote atokaye mashariki wala magharibi au kutoka jangwani awezaye kumkweza mwanadamu.

  25. Kila amsingiziaye jirani yake kwa siri, huyo nitamnyamazisha; mwenye macho ya dharau na moyo wa kiburi huyo sitamvumilia.