Skip to content

Mistari ya Biblia kuhusu Pride

303 mistari · 61 vipengele

Mistari muhimu ya Biblia

Chuja kwa kitabu
  1. Ni afadhali kuwa mnyenyekevu katika roho miongoni mwa walioonewa kuliko kugawana nyara pamoja na wenye kiburi.

  2. Yeye apendaye ugomvi apenda dhambi; naye ainuaye sana lango lake hutafuta uharibifu.

  3. Mali ya tajiri ni mji wake wenye ngome, wanaudhania kuwa ukuta usioweza kurukwa.

  4. Kabla ya anguko moyo wa mtu hujaa kiburi, bali unyenyekevu hutangulia heshima.

  5. Watu wengi hujidai kuwa na upendo usiokoma, bali mtu mwaminifu ni nani awezaye kumpata?

  6. Macho ya kudharau na moyo wa kiburi, ambavyo ni taa ya waovu, vyote ni dhambi!

  7. Mtu mwenye kiburi na majivuno, “Mdhihaki” ndilo jina lake; hutenda mambo kwa kiburi kilichozidi.

  8. Kama vile mawingu na upepo pasipo mvua ndivyo alivyo mtu ajisifuye kwa zawadi ambazo hatoi.

  9. Si vyema kula asali nyingi sana, wala si heshima kujitafutia heshima yako mwenyewe.

  10. Mjibu mpumbavu sawasawa na upumbavu wake, ama atakuwa mwenye hekima machoni pake mwenyewe.

  11. Je, unamwona mtu ajionaye mwenye hekima machoni pake mwenyewe? Liko tumaini zaidi kwa mpumbavu kuliko kwake.

  12. Mtu mvivu ni mwenye hekima machoni pake mwenyewe, kuliko watu saba wawezao kujibu kwa busara.

  13. Mwache mwingine akusifu, wala si kinywa chako mwenyewe; mtu mwingine afanye hivyo na si midomo yako mwenyewe.

  14. Mtu tajiri anaweza kuwa na hekima machoni pake mwenyewe, bali mtu maskini mwenye ufahamu atamfichua.

  15. Mtu mwenye tamaa huchochea fitina, bali yule amtegemeaye Bwana atafanikiwa.

  16. Wenye mzaha huuchochea mji, bali watu wenye hekima hugeuzia mbali hasira.

  17. Kiburi cha mtu humshusha, bali mtu mwenye roho ya unyenyekevu hupata heshima.

  18. wale ambao ni safi machoni pao wenyewe kumbe hawakuoshwa uchafu wao;

  19. wale ambao daima macho yao ni ya kiburi, ambao kutazama kwao ni kwa dharau;

  20. Macho ya mtu mwenye majivuno yatanyenyekezwa na kiburi cha wanadamu kitashushwa, Bwana peke yake ndiye atakayetukuzwa siku hiyo.

  21. Bwana Mwenye Nguvu Zote anayo siku aliyoiweka akiba kwa wote wenye kujivuna na wenye kiburi, kwa wote wanaojikweza (nao watanyenyekezwa),

  22. kwa mierezi yote ya Lebanoni iliyo mirefu sana, na mialoni yote ya Bashani,

  23. kwa milima yote mirefu na vilima vyote vilivyoinuka,

  24. kwa kila mnara ulio mrefu sana na kila ukuta wenye ngome,

  25. kwa kila meli ya biashara, na kila chombo cha baharini cha fahari.