Rukia maudhui

circa AD 48–96

Letters to the Churches

Paul and other apostles write to strengthen, correct, and encourage the scattered churches across the Roman world.

2,767 mistari · 21 vitabu vimehusishwa

Mistari ya kipindi hiki

Chuja kwa kitabu
  1. Waebrania 13:15takriban 64 BK

    Basi kwa njia ya Yesu, tuzidi kumtolea Mungu dhabihu ya sifa, yaani matunda ya midomo inayolikiri Jina lake.

  2. Waebrania 13:16takriban 64 BK

    Na msiache kutenda mema na kushirikiana vile vitu mlivyo navyo, kwa kuwa dhabihu kama hizo ndizo zinazompendeza Mungu.

  3. Waebrania 13:17takriban 64 BK

    Watiini viongozi wenu na kujinyenyekeza chini ya mamlaka yao. Kwa maana wao wanakesha kwa ajili yenu kama watu watakaopaswa kutoa hesabu. Watiini ili wafanye kazi yao kwa furaha, wala si kama mzigo, maana hiyo haitakuwa na faida kwenu.

  4. Waebrania 13:18takriban 64 BK

    Tuombeeni. Tuna hakika kuwa tunayo dhamiri safi na shauku ya kuishi kwa uadilifu kwa kila njia.

  5. Waebrania 13:19takriban 64 BK

    Ninawasihi zaidi mniombee ili nipate kurudishwa kwenu upesi.

  6. Waebrania 13:20takriban 64 BK

    Basi Mungu wa amani, ambaye kwa damu ya Agano la milele alimleta tena kutoka kwa wafu Bwana wetu Yesu, yule Mchungaji Mkuu wa kondoo,

  7. Waebrania 13:21takriban 64 BK

    awafanye ninyi wakamilifu mkiwa mmekamilishwa katika kila jambo jema ili mpate kutenda mapenzi yake, naye atende ndani yetu kile kinachompendeza machoni Pake, kwa njia ya Yesu Kristo, ambaye utukufu una yeye milele na milele. Amen.

  8. Waebrania 13:22takriban 64 BK

    Ndugu zangu, nawasihi mchukuliane na maneno yangu ya maonyo, kwa kuwa nimewaandikia waraka mfupi tu.

  9. Waebrania 13:23takriban 64 BK

    Nataka ninyi mjue kwamba ndugu yetu Timotheo amefunguliwa kutoka gerezani. Akifika mapema, nitakuja pamoja naye kuwaona.

  10. Waebrania 13:24takriban 64 BK

    Wasalimuni viongozi wenu wote na watakatifu wote. Wale wa kutoka Italia wanawasalimu.

  11. Waebrania 13:25takriban 64 BK

    Neema iwe nanyi nyote. Amen.

  12. Yakobo 1:1takriban 60 BK

    Yakobo, mtumwa wa Mungu na wa Bwana Yesu Kristo: Kwa makabila kumi na mawili yaliyotawanyika ulimwenguni: Salamu.

  13. Yakobo 1:2takriban 60 BK

    Ndugu zangu, hesabuni kuwa ni furaha tupu mnapopatwa na majaribu mbalimbali,

  14. Yakobo 1:3takriban 60 BK

    kwa sababu mnajua ya kuwa kujaribiwa kwa imani yenu huleta saburi.

  15. Yakobo 1:4takriban 60 BK

    Saburi na iwe na kazi timilifu, ili mpate kuwa wakamilifu, mmekamilishwa, bila kupungukiwa na kitu chochote.

  16. Yakobo 1:5takriban 60 BK

    Kama mtu yeyote miongoni mwenu amepungukiwa na hekima na amwombe Mungu, yeye awapaye watu wote kwa ukarimu wala hana kinyongo, naye atapewa.

  17. Yakobo 1:6takriban 60 BK

    Lakini anapoomba, lazima aamini wala asiwe na shaka, kwa sababu mtu aliye na shaka ni kama wimbi la bahari, lililochukuliwa na upepo na kutupwa huku na huku.

  18. Yakobo 1:7takriban 60 BK

    Mtu kama huyo asidhani ya kuwa atapata kitu chochote kutoka kwa Bwana.

  19. Yakobo 1:8takriban 60 BK

    Yeye ni mtu mwenye nia mbili, mwenye kusitasita katika njia zake zote.

  20. Yakobo 1:9takriban 60 BK

    Ndugu asiye na cheo kikubwa yampasa ajivunie hali hiyo maana ametukuzwa.

  21. Yakobo 1:10takriban 60 BK

    Lakini yeye aliye tajiri afurahi kwa kuwa ameshushwa, kwa sababu atatoweka kama ua la shambani.

  22. Yakobo 1:11takriban 60 BK

    Kwa maana jua kali lenye kuchoma huchomoza na kuliunguza, likayakausha majani, na ua lake likapukutika, nao uzuri wake huharibika. Vivyo hivyo tajiri naye atanyauka akiwa anaendelea na shughuli zake.

  23. Yakobo 1:12takriban 60 BK

    Heri mtu anayevumilia wakati wa majaribu, kwa sababu akiisha kushinda hilo jaribio atapewa taji la uzima Mungu alilowaahidia wale wampendao.

  24. Yakobo 1:13takriban 60 BK

    Mtu anapojaribiwa asiseme, “Ninajaribiwa na Mungu.” Kwa maana Mungu hawezi kujaribiwa na maovu wala yeye hamjaribu mtu yeyote.

  25. Yakobo 1:14takriban 60 BK

    Lakini kila mtu hujaribiwa wakati anapovutwa na kudanganywa na tamaa zake mwenyewe zilizo mbaya.