Rukia maudhui

circa AD 48–96

Letters to the Churches

Paul and other apostles write to strengthen, correct, and encourage the scattered churches across the Roman world.

2,767 mistari · 21 vitabu vimehusishwa

Mistari ya kipindi hiki

Chuja kwa kitabu
  1. Yakobo 2:13takriban 60 BK

    Kwa kuwa hukumu bila huruma itatolewa kwa mtu yeyote asiyekuwa na huruma. Huruma huishinda hukumu.

  2. Yakobo 2:14takriban 60 BK

    Ndugu zangu, yafaa nini ikiwa mtu atadai kuwa anayo imani lakini hana matendo? Je, imani kama hiyo yaweza kumwokoa?

  3. Yakobo 2:15takriban 60 BK

    Ikiwa ndugu yako au dada hana mavazi wala chakula,

  4. Yakobo 2:16takriban 60 BK

    mmoja wenu akamwambia, “Enenda zako kwa amani, ukaote moto na kushiba,” pasipo kumpatia yale mahitaji ya mwili aliyopungukiwa, yafaa nini?

  5. Yakobo 2:17takriban 60 BK

    Vivyo hivyo, imani peke yake kama haikuambatana na matendo, imekufa.

  6. Yakobo 2:18takriban 60 BK

    Lakini mtu mwingine atasema, “Wewe unayo imani; mimi ninayo matendo.” Nionyeshe imani yako pasipo matendo nami nitakuonyesha imani yangu kwa matendo.

  7. Yakobo 2:19takriban 60 BK

    Unaamini kwamba kuna Mungu mmoja. Vyema! Hata mashetani yanaamini hivyo na kutetemeka.

  8. Yakobo 2:20takriban 60 BK

    Ewe mpumbavu! Je, wataka kujua kwamba imani bila matendo haifai kitu?

  9. Yakobo 2:21takriban 60 BK

    Je, Abrahamu baba yetu hakuhesabiwa haki kwa kile alichotenda, alipomtoa mwanawe Isaki madhabahuni?

  10. Yakobo 2:22takriban 60 BK

    Unaona jinsi ambavyo imani yake na matendo yake vilikuwa vinatenda kazi pamoja, nayo imani yake ikakamilishwa na kile alichotenda.

  11. Yakobo 2:23takriban 60 BK

    Kwa njia hiyo yakatimizwa yale Maandiko yasemayo, “Abrahamu alimwamini Mungu na ikahesabiwa kwake kuwa haki,” naye akaitwa rafiki wa Mungu.

  12. Yakobo 2:24takriban 60 BK

    Mnaona ya kwamba mtu huhesabiwa haki kwa yale anayotenda wala si kwa imani peke yake.

  13. Yakobo 2:25takriban 60 BK

    Vivyo hivyo, hata Rahabu, yule kahaba, hakuhesabiwa haki kwa yale aliyotenda alipowapokea wale wapelelezi na kuwaambia waende njia nyingine?

  14. Yakobo 2:26takriban 60 BK

    Kama vile ambavyo mwili pasipo roho umekufa, kadhalika nayo imani pasipo matendo imekufa.

  15. Yakobo 3:1takriban 60 BK

    Ndugu zangu, msiwe walimu wengi, kwa maana mnafahamu kwamba sisi tufundishao tutahukumiwa vikali zaidi.

  16. Yakobo 3:2takriban 60 BK

    Sisi sote tunajikwaa katika mambo mengi. Ikiwa mtu yeyote hakosei kamwe katika yale anayosema, yeye ni mkamilifu, naye anaweza kuuzuia pia na mwili wake wote.

  17. Yakobo 3:3takriban 60 BK

    Tunapotia lijamu kwenye vinywa vya farasi ili kuwafanya watutii, tunaweza kuigeuza miili yao yote.

  18. Yakobo 3:4takriban 60 BK

    Au angalia pia meli, ingawa ni kubwa sana, nazo huchukuliwa na upepo mkali, lakini hugeuzwa kwa usukani mdogo sana, kokote anakotaka nahodha.

  19. Yakobo 3:5takriban 60 BK

    Vivyo hivyo ulimi ni kiungo kidogo sana katika mwili, lakini hujivuna majivuno makuu. Fikirini jinsi moto mdogo unavyoweza kuteketeza msitu mkubwa!

  20. Yakobo 3:6takriban 60 BK

    Ulimi pia ni moto, ndio ulimwengu wa uovu kati ya viungo vya mwili. Ulimi huutia mwili wote wa mtu unajisi na kuuwasha moto mfumo mzima wa maisha yake, nao wenyewe huchomwa moto wa jehanamu.

  21. Yakobo 3:7takriban 60 BK

    Kwa maana kila aina ya wanyama, ndege, wanyama watambaao na viumbe vya baharini vinafugika na vimefugwa na binadamu,

  22. Yakobo 3:8takriban 60 BK

    lakini hakuna mtu awezaye kuufuga ulimi. Ni uovu usiotulia, umejaa sumu iletayo mauti.

  23. Yakobo 3:9takriban 60 BK

    Kwa ulimi tunamhimidi Bwana, yaani Baba yetu, na kwa huo twawalaani watu walioumbwa kwa mfano wa Mungu.

  24. Yakobo 3:10takriban 60 BK

    Katika kinywa kile kile hutoka baraka na laana. Ndugu zangu, haistahili kuwa hivyo.

  25. Yakobo 3:11takriban 60 BK

    Je, chemchemi yaweza kutoa katika tundu moja maji matamu na maji ya chumvi?